Kwa wanandoa tu.

mara ya mwisho umefika lini bongo?
au mleta mada anaishi USA au nchi nyingine zilizoendelea?
hizo monitor zinatumia mishumaa au taa za chemli?
Naishi Tanzania.hata mie nilianza kuwaza monitor za mishumaa.
 
Eneleeni kuamshana usiku wa manane kama wanga hamna jinsi mtoto anatkw alale na mama hadi miaka sita
 
Ni ngumu kidogo lkn kwa umri alio nao anapaswa kulala kitnda cha peke ake . Unajua watoto siku hizi wanaelewa vitu mapema so bora alale peke yake.
 

Aisee mimi nakumbuka mama alikuwa ananitoroka kitandani usiku na kwenda kitanda cha baba. Sijui nilikuwa na umri gani by that time; lakini as you say nafikiri ni vyema mtoto alale pekee from day one, hata infection ndogo ndogo unaweza zuia kwa separation hiyo licha ya kuzuia ajali na kumfanya ajitegemee.
 

Usizungumze kwa sauti.We wee
 
mimi naona mtoto angalau awe amefika miaka miwili na nusu ndio afundishwe kulala peke yake, mtoto wangu ana mwaka 1 na miezi 7 lakini nalala naye coz bado ananyonya, sasa ninyi mnaosema akifika miezi 6 alale peke yake na kunyonya inakuwaje! tusiwanyime watoto haki yao jamani, anaweza akalala peke yake usiku akawa na homa usijue hadi una amka asubuhi mtoto kazidiwa, lakini ukilala naye akiwa na homa tu unajua coz anakugusa au wewe mwenyewe unamgusa.

Aidha, akilala peke yake usiku kunaweza kukawa na baridi mzazi unatakiwa kumfunika mtoto, au joto kali unamvua nguo au amejisaidia unambadilisha, sasa akilala usiku kucha peke yake jamani, si utakuta choo kimegandiana mwilini mwake, kwa kweli mimi sishauri mtoto kulala peke yake ktk umri huo, subiri angalau miaka 2 na nusu si haba hata kuongea kidogo anakuwa anaweza na akihitaji kitu atakuita, hiyo ya kutolala na mtoto as from day 1 sio utamaduni wetu watanzania, acheni kuiga tamaduni zisizo wezekana katika uhalisia!
 
kitanda chako futi ngapi?maana kama ni minimum ya futi 5 mbona kinatosha sana??acheni mbwembwe
 
tunashauriwa tunaponyonyesha watoto tuwe tumeamka na tumekaa....
mimi wanangu wanalala kwa kitanda chao toka day 1 na haimaanishi sinyonyeshi. na ukiwa na mtoto mchanga unasikia kila movement ya mtoto hata kama hujalala naye kitanda kimoja.
Muda wa kunyonyesha naamka, nachukua mwanangu, nakaa naye, naanza kumnyonyesha. Kunyonyesha siyo lazima ulale naye kitanda kimoja.
kwanza akitimiza mwaka huwa anahama chumba, muda wa kunyonya ukifika namfwata huko huko chumbani kwake. na mimi huwa nanyonyesha miaka 3, sasa nilale na mtoto kitandani kwangu hadi miaka 3?
 
ha haaa, wewe ndo wale uliokuwa unang'ang'ania kulala na mama mpaka uzeeni? lol!
 

mh hiyo nayo ni shughuli nyingine jamani, kweli binafsi siiwezi, nalala na mwanangu hadi aache kunyonya, that is me!
 
mh hiyo nayo ni shughuli nyingine jamani, kweli binafsi siiwezi, nalala na mwanangu hadi aache kunyonya, that is me!
nimeipenda hapo red
ila ujue hata sisi tunaolaza watoto peke yao tunanyonyesha pia.
 
nimeipenda hapo red
ila ujue hata sisi tunaolaza watoto peke yao tunanyonyesha pia.
ni msisitizo, hiyo inaeleweka best, ila kwangu naona ni kazi kubwa kuamka uende kunyonyesha, uje ulale, hivi utaamka mara ngapi dear!
 
ni msisitizo, hiyo inaeleweka best, ila kwangu naona ni kazi kubwa kuamka uende kunyonyesha, uje ulale, hivi utaamka mara ngapi dear!
huwa nampunguzia idadi ya kunyonya usiku kadiri anavyokua.
anapokuwa mchanga ananyonya mara kwa mara maana naamini anachoka kuvuta mapema, ndo maana nalala naye chumbani kwangu.
anapokua huwa maximum kumnyonyesha usiku ni mara 3, na ndo maana nakaa ananyonya mpaka achoke na kuacha mwenyewe, then akilala nina uhakika anaweza lala zaidi ya masaa 3.
kuna siku naweza amka mara moja tu.
nb. huwa simwamshi mtoto kunyonya, namnyonyesha akiwa ameamka. mara nyingi watoto wanaamshwa na kulowa mkojo au njaa. kama kulowa tu nikimbadilisha huwa analala tena, na mimi narudi kulala
 

Na ulipokua unayashuhudia hayo ulikua unawaza nini?I would like to know!
 
haya bwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…