Kwa wanamabadiliko wote, Najua mmeumia sana lakini nawashauri mpunguze munkari. Najua hasira zenu, majuto yenu

Francis nataka Malisa aione kupitia kwako, kama ccm wana raha basi ni ya muda tu, hapa sisi wengine kwetu imekuwa fursa ya kuonyesha ule ubovu tulioupigia kelele lakini viongozi wakatia pamba. Huu ukali tunaonyesha hapa jukwaani ni ili kosa kama hili lisirudiwe. Kwa ukali huu tutapata chama imara na makosa ya kijinga kama hilo la kumpokea Lowassa halitorudiwa na wanachama wote watakuwa wakali kwani tutakuwa tumejifunza kutokana na makosa. Kwa sasa Lowassa hata asema mazuri yapi aliyoongea na Magufuli kwetu tumeshaonyesha kwamba sio chaguo letu. Na hii inafungua ukurasa wa kuweka viongozi wenye damu ya upinzani na sio hao wanasesere wa upinzani. Tunaomba sasa hata Mbowe akae pembeni kiroho safi ili chama kipate watu ambao wako tayari kufanya mageuzi ya kweli. Mbowe aendelee na biashara zake kwani anaweza kubanwa kirahisi.
mnae nyalandu huko
 
Upinzani ulikuwepo kabla ya ujio wa lowasa, ulikuwa juu sababu ya uongozi uliotukuka wa Dr slaa
Upinzani ulikuwepo kabla ya traitor Slaa na unaendelea kuwepo hata baada ya kubainika usaliti wake na kuondoka kwa aibu mpaka ikamlazimu kukimbia nchi. Aluta continua.
 
Upinzani ulikuwepo kabla ya ujio wa lowasa, ulikuwa juu sababu ya uongozi uliotukuka wa Dr slaa
Upinzani ulikuwepo kabla ya Dr Slaa, na umeendelea kuimarika hata baada yake. ni jambo la aibu kamanda kusaliti vita na kukimbilia kwa adui. huwa inaruhusiwa tu kama unakwenda kule halafu urudi tena. lakini alilofanya Dr. Slaa ni la aibu kubwa.
 
mnae nyalandu huko

Hazuiwi kuwa mwanachama wa kawaida kwani ni mtanzania mwenzetu, lakini sio sahihi kuwa kiongozi kupitia cdm kwani ana mawaa. Kama ana kashfa na alipokuwa ccm waliogopa kumchukulia hatua wakati ni sasa.
 
Back
Top Bottom