Kwa wanachadema na wapenda mabadiliko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wanachadema na wapenda mabadiliko

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ALEX PETER, Apr 13, 2012.

 1. ALEX PETER

  ALEX PETER Senior Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nini hatima yetu na malengo yetu kama vijana.

  tangu ufanyike uchaguzi mkuu wa tanzania ni mwaka mmoja na miezi kadhaa sasa imepita nafikiri huu ni muda muafaka wa kukaa chini na kutathmini kipi kilifanya tushindwe kuleta mabadiliko na utawala wa haki katika hii nchi ni wengi sana wanatamani mabadailiko lakini wanashindwa kufanya kutokana na kwamba wanakosa mipango,sera na mikakati madhubuti.

  Kulingana na hali halisi ya uchaguzi wa 2010 ilivokuwa imenipelekea kungamua sababu mbili tatu ambazo ni za msingi sana na kama tukishindwa kuzifanyia kazi tutakuwa ni watu wa kulalamika na kuililia nchi yetu kama tunavokazana kuikomboa sasa hvi moja ya sababu ambayo inaweza ikatusaidia tukaleta mabadiliko ni:-

  kukosa shahada za kupigia kura kwa vijana. Hii kwangu imekuwa ni sababu nzito ambayo imenifanya nione hatuna budi kuwahamasisha vijana ili wakajiandikishe pindi daftari likianza kuboreshwa maana tutakuwa watu wa ajabu kama tunatamani mafanikio lakini hatutaki kuwa na malengo na mikakati ya kueleweka,ni vijana hawahawa ambao wamekuwa mstari wa mbele wakitaka mabadiliko lakini ni hawahawa ambao hawana shahada za kupigia kura,ningeomba chama kama chama kiandae mkakati wa kutoa elimu ya uraia kwa vijana na wananchi kwa ujumla hasa wale wanaoishi vijini maana ndiko chama tawala kinachukulia kura nyingi kutokana na wengi wao kuwa na uelewa mdogo juu ya nchi yao inavoendeshwa na jinc gani ingepaswa kuendeshwa naamini tukifanikiwa kwenye hilo basi tutakuwa walau tumepiga hatua kadhaa mbele kuelekea kwenye ushindi.


  sababu ya pili ni baadhi ya wagombea kupita bila kupingwa.

  Kwangu mie hiki kimekuwa kigezo namba mbili ambacho kilipelekea tushindwe kutimiza adhima yetu kama wananchi wapenda mabadiliko kutokana na wagombea wa chama tawala kupita bila kupingwa kwenye baadh ya majimbo imepelekea moja kuwanyima wananchi haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua mtu wamtakaye hii yote imetokana na uwoga pamoja na hofu tulizonazo watanzania naamini wangepatikana watu wa kuwapinga kwenye majimbo yao tungefanya mchuano kuwa mkali maana wananchi wangeweza kuwa na uelewa kidogo walau nchi yao imefikia wapi.

  Lakini kitendo cha kuwaacha watu wale wale wenye hoja na sera zilezile kumepelekea wananchi kuwa na mtazamo ule ule maana wamekosa fursa ya kufanya mabadiriko maana wamekosa mtu wa kuwafumbua macho matokeo yake tunawapa nafasi kubwa hawa magamba kufanya wanachotaka wanaweza wakatuchakachua maana hatuna mawakala maeneo yale.

  Nafikiri uchaguzi wa 2015 haitakiwi tuwape nafac ya kupita bila kupingwa kujitokeza kwetu kugombea ndo kunatoa changamoto kwa wananchi na pia ndo chama tunakieneza katika maeneo yale maana watu wanaweza kukifaham kupitia wagombea wetu watakaosimama eneo husika.

  sababu ya tatu,kukosekana kwa tume huru, ninaposema tume huru na maana ya tume itakayoweza kusimamia uchaguzi na kutoa matokeo bila kuingiliwa na serikali,endapo tungekuwa na tume huru inayojiweza kifedha,ambayo ina watumishi wake binafsi ambayo ina ofisi zake pamoja na magari yake binafsi nafikiri tungekuwa tunapata matokeo halali wala cyo yaliyotengenezwa na chama dora,naamini tukifanikiwa kupata katiba bora basi tunaweza tukapata na tume bora lakini tukipata katiba mpya basi tunaweza tukapata na tume mpya lakini siyo bora,

  kama kuna mapungufu mengine uliyaona unaweza ukaongezea walau tupate hitimisho lililobora na lenye manufaa kwa taifa letu na wananchi kwa ujumla
   
 2. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Chama kujitangaza Mjini na kusahau vijijini ambako magamba wanaenda kutuibia kura.
   
 3. g

  goodluck tesha Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  5.UJINGA kwa wananchi wetu wanakubali kupokea vihela,khanga,kofia,na hatimaye kuuza haki yao.
  6.UMASIKINI nao uunachangia watu wanauza shahada ili wapate shibe .
  7.MWAMKO DUNI WA WANANCHI baadhi ya wananchi wanapuuzia suala la uchaguzi
  .
   
 4. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Naamini ccm wana
  wataka wananchi
  wawe maskini ili
  wawadanganye kwa vitu vidogo, mimi kila tatizo ninaloliona nasema limeletwa na ccm. Kila unapomwona kijana mweleze matatizo yota ya nnchi hii yameletwa na ccm, nnaona wengi washaanza kuelewa.(tuanze na sala)
   
 5. w

  warea JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si busara kuwalaumu wananchi, fanya kazi ya kuwaelimisha ndo uwalaumu.
  Watawala wana mbinu chafu. Kama wanaiba kura mjini, kijijini inakuwaje?
   
Loading...