Kwa wamiliki wa gari, trekta , mashine , generators pita hapa uone jinsi utakavyoboresha biashara

usalama kwanza

JF-Expert Member
Oct 3, 2012
386
158
Habari.

Kwa karibu mwaka mmoja sasa tumekuwa tukitoa huduma ya security systems kama GPS tracker , security cameras , electric fence , access control systems. Leo nimeona niongelee kuhusu huduma GPS tracking/ Car tracking/ Asset tracking tunayoitoa na nitakupa mifano jinsi huduma hii inavyoweza kufanya upate faida zaidi kupitia kwenye gari au mashine yako. Nitajaribu kukupa mifano michache ili uweze kuelewa ni jinsi gani unaweza pata faida zaidi kwenye chombo chako.

Mteja A

Yeye ana gari lake lipo moshi linalobeba vifusi, kokoto , mchanga . Anawalipa wafanyakazi wake mshahara na posho kila siku. Ili aweze kupata faida kwa uhakika basi yeye ameamua ya kuwa awe anapokea email notification kila gari linapoingia sehemu ya machimbo au sehemu wanapobeba kokoto , mchanga , au vifusi kwa hiyo ana uhakika wa kujua gari lake limefanya trip ngapi na kila trip bei ya ubebaji inafahamika kwahiyo anao uhakika wa kupata hela kwa kila trip gari inayoenda.

Mteja B

Yeye analo gari la maji taka maeneo ya mwanza . Yeye anahitaji kujua tu gari lake limeenda kumwaga maji machafu mara ngapi kwasababu malipo hutegemea na ufanyaji kazi wa gari , huyu naye amechagua kupata ujumbe kwa njia ya email na sms ikiwa gari litafika sehemu husika kwahiyo anao uhakika wa kupata hela kila gari lake linapofanya kazi.

Mteja C

Yeye yupo tanga anamiliki na kukodisha excavator. Hana haja ya kuwa karibu na mashine/mtambo huu , yeye anapoambiwa kuwa kazi imeisha na excavator limezimwa basi yeye hulidisable kabisa lisiwake na linapoanza kazi basi huliwezesha liwake hivyo hana wasiwasi kuhusu muda ambao mashine yake imefanya kazi na malipo anayokuwa ameyapata.

Mteja D.

Huyu ni msambazaji wa bidhaa yupo , anamiliki Suzuki carry nyingi kiasi. Yeye hutumia system hii kuangalia ikiwa magari yamefanya kazi na kama yamefanya kazi ni kwa muda gani , limeendeshwa kwa umbali gani. Muda uliotumiwa kupaki gari na maeneo gari lilipopita na pia kwa ajili ya usalama wa magari yake.

Mteja E

Huyu yupo njombe , yeye anachohitaji ni ulinzi wa gari lake , hivyo yeye ameweka alarm kama basic function , ikiwa gari litaguswa , au kufunguliwa milango au kuwashwa basi king’ora kitalia lakini pia amefunga kwa ajili ya tracking , akiwa yupo mbali na gari lake basi anao uwezo wa kujua lilipo na linafanya kazi gani . Wapo ambao pia wamefunga kwenye bajaj, pikipiki na magari mengine binafsi.

Mteja F

Yeye ni mmiliki wa malori ya usafirishaji anachohitaji ni kujua matumizi ya mafuta ya magari yake, yeye amechagua kupata taarifa za wizi wa mafuta , kila kunapotokea wizi wa mafuta basi hupata taarifa kwa njia ya email na pia kupitia web account .Sasa hana wasiwasi wa juu ya wizi wa mafuta.

Mteja G

Huyu yeye ni mmiliki wa trekta mkoani morogoro na yeye ni mkazi wa Dar es salaam. Yeye hana wasiwasi juu ya matumizi ya trekta , jembe la trekta linapoanza kufanya kazi basi yeye hupata taarifa , hujua muda ambao jembe lake lilima anao uwezo wa kuangalia lilima eneo lipi , kuhusu network hilo sio tatizo kwake hata kama haipo basi mara linaporudi sehemu yenye network basi hupata taarifa zote wakati trekta likifanya kazi.

Nimekupa mifano michache ili uweze kujua jinsi mbalimbali ambazo nawe unaweza kutumia kifaa hiki ili kuboresha biashara yako ya usafirishaji na usimamizi wa magari/ Vifaa/ mashine zako. Vifaa hivi tunao uwezo wa kuvifunga kwenye majenereta , fridge , tractor, magari madogo , makubwa, mitambo na mashine mbalimbali na mengineyo.

Kifaa hiki kinakupa uwezo wa kujua mwendo kasi na kufanya kazi kama speed limiter pia. Unaweza kuset speed mfano kutoka ubungo mpaka mbezi speed iwe ni 50 basi ikiwa itaover speed basi utapata ripoti ya over speed kwenye eneo hilo na pia unaweza kuchagua kuwa kama gari imezidisha mwendo basi tracking device ifanye kazi kama speed governor (speed gavana).

Karibu tuongee ni jinsi gani tunaweza kukuhudumia .

Kwa demo ya kutrack gari ingia kwenye website yetu www.isecure.co.tz , kisha bonyeza sehemu pameandikwa track device na tumia user name isecure na password isecure. Account hii ni kwa ajili ya demo pekee na hutaweza kutuma command yeyote zaidi ya kupokea riport

Kwa mawasiliano 0714890018 au email: info@isecure.co.tz
 
Ipo vizuri hii gharama zipoje mkuu
Kama hii ya kwenye bajaji matumizi binafsi alarm n.k
 
Ipo vizuri hii gharama zipoje mkuu
Kama hii ya kwenye bajaji matumizi binafsi alarm n.k
Gharama ya installation ni Tsh 300,000/- , unaweza kuchagua kutokulipia au kulipia service ya kila mwezi ya tsh 20,000/- . Utakapolipia utapata Web accont, application kwenye simu , usipolipia utapata taarifa zote kupitia simu ya mkononi
 
Karibu ujipatie huduma zifuatazo kutoka isecure technology
  • CCTV camera systems repair and installation
  • Fire alarms systems repair and installation
  • Access control systems
  • Video intercom systems
  • Automatic gates. Repair and installation
  • Car tracking systems installation
  • Electric fence
  • Time attendance systems

    tupigie 0677178169 , email: info@isecure.co.tz
 
Karibu ujipatie huduma zifuatazo kutoka isecure technology
  • CCTV camera systems repair and installation
  • Fire alarms systems repair and installation
  • Access control systems
  • Video intercom systems
  • Automatic gates. Repair and installation
  • Car tracking systems installation
  • Electric fence
  • Time attendance systems

    tupigie 0677178169 , email: info@isecure.co.tz
 
Karibu ujipatie huduma zifuatazo kutoka isecure technology
  • CCTV camera systems repair and installation
  • Fire alarms systems repair and installation
  • Access control systems
  • Video intercom systems
  • Automatic gates. Repair and installation
  • Car tracking systems installation
  • Electric fence
  • Time attendance systems

    tupigie 0677178169 , email: info@isecure.co.tz
 
Karibu ujipatie huduma zifuatazo kutoka isecure technology
  • CCTV camera systems repair and installation
  • Fire alarms systems repair and installation
  • Access control systems
  • Video intercom systems
  • Automatic gates. Repair and installation
  • Car tracking systems installation
  • Electric fence
  • Time attendance systems

    tupigie 0677178169 , email: info@isecure.co.tz
 
Back
Top Bottom