Kwa waliowahi kupata supplementary (Sup) Chuoni.

Kuna mdogo wangu nilimwambia aniletee matokeo yake,ajamaliza bado ila kuna kozi bado kawekewa D na anasema ashasapua..hii imekaaje??
Kama kasapua basi wataibadilisha hiyo D ina maana aliipata after first seat ya UE aliyoifanya kama kasapua majibu yakitoka atakuwa na C huwa haizidi hapo hata kama ulipata A
 
Mwaka wa kwanza udsm nilikuwa na supplementary ya

EC 116 na
EC 117 nikachomoa 117 nikabeba 116

Mwaka wa pili
Suplimentary ya
EC 216
EC 217
EC 218
EC 219
Nilikuwa na gpa ya 1.6 iyo ni semester ya kwanza apo kuna coz mbili ambazo nilipiga B+ na B mana kwa semister tuna coz sita

Semister ya pili mwaka wa pili
Supplementary
EC 229

Jumlisha na carry over ya EC 116

Usiulize nilipitaje mwaka wa pili kuingia wa tatu pia usiulize nilichomoka vipi

Pia mwaka wa tatu sikuwa na carry over ata moja
Kama nikiuliza itakuwaje mkuu.
 
Picha linaanza semester ya kwanza mwaka wa kwanza nakula supp 3 kipuuzi tu. Dah nikajiuliza inamaana me nafanya nini chuo, Second semester ikaenda nikasapua zile supp. Kilichofuata baada ya hapo sijawahi pata supp mpaka namaliza mwaka wa 4...

Ila kwenye project mwaka wa nne ndio nilijuta. Mpka ilifika stage nikajiona kama hakuna nilichokuwa nafanya ile miaka mitatu...
 
Qm ukutane na dr ngasamiaku ni nouma

Course work nilikuwa na 15.5 ambayo ni automatic carry over nikaenda kumuomba 0.5 alicho nijibu sitakaa nisahau katika maisha yangu

Ila alituachia wote kwanzia mwenye 15 tufanye ue tho nilisupp
Ha ha yule Dr mzinguaji qm haiwezi anachofundisha yy mwenyewe hakielewi halafu pepa zake hatungi anagoogle kuna siku tulimuotea maana tulizingua akatoa pepa nyingine niliacha 0.5 tu

Ulimaliza mwaka gani mkuu?
 
Ha ha yule Dr mzinguaji qm haiwezi anachofundisha yy mwenyewe hakielewi halafu pepa zake hatungi anagoogle kuna siku tulimuotea maana tulizingua akatoa pepa nyingine niliacha 0.5 tu

Ulimaliza mwaka gani mkuu?

Hahaha alitufundisha differentiation alafu anatumia projector nikisanga

Semister ya pili akatufundisha social accounting matrix
 
Mwaka wa kwanza udsm nilikuwa na supplementary ya

EC 116 na
EC 117 nikachomoa 117 nikabeba 116

Mwaka wa pili
Suplimentary ya
EC 216
EC 217
EC 218
EC 219
Nilikuwa na gpa ya 1.6 iyo ni semester ya kwanza apo kuna coz mbili ambazo nilipiga B+ na B mana kwa semister tuna coz sita

Semister ya pili mwaka wa pili
Supplementary
EC 229

Jumlisha na carry over ya EC 116

Usiulize nilipitaje mwaka wa pili kuingia wa tatu pia usiulize nilichomoka vipi

Pia mwaka wa tatu sikuwa na carry over ata moja
Asee ulipambana kwel..ongerq
 
Zamani kulikuwa na msemo unaosema kutereza sio kuanguka ,msemo huu ukiuleta kwa wasomi huwa unakuja na tumaini jipya,

Maisha ya chuo yana changamoto kubwa sana mwanzo nilivyoanza nilijua ni sehemu flani simple simple ya kukutana na wadada wazuri kupiga story na kuwala ,

Semister ya kwanza ilivyoisha nilikoswa koswa lakini nilipita salama ile ya pili sasa nilikamatwa na sup alafu nilivyocreal ka GPA kalikuwa kadogo kinyama ,

Nilivyoenda likizo na kurudi nilijisemea tu hapa siyo pa mchezo mchezo nikileta mzaa cheti nitakisikia kwenye bomba nilikaza na kumaliza fresh.


Na wewe kama uliwahi kupata sup wakati ukiwa chuoni ukuje hapa.
Me nimepata supp ya somo moja tena semister ya kwanza hivi inaweza ikaleta madhara yeyote kwenye cheti endapo sitapata supp nyingine
 
Back
Top Bottom