Kwa waliosoma Biomedical Equipment Engineering Habari

JAMBONIA LTD

JF-Expert Member
Jan 22, 2014
576
263
Habari kama kuna member yoyote aliyesoma hii kozi kuna kijana anaomba ushauri anataka kuapply pale DIT, au hata kama unamjua aliyesoma ,je ni kozi yenye future nzuri?
 
*MAMBO YALIYOJILI KWENYE KIKAO CHA RMO/DMO DODOMA 13-18/08/2018; Kama mwakilishi wenu niliyanoti inbrief*
1.Ikiwa mtumishi alienda kusoma kwa kuruhusiwa na mamlaka husika na pindi anaenda alishapanda ngazi kadhaa za madaraja hivyo anaporudi na kufanyiwa categorisation inatua kwenye ngazi ya mshahara ya chini aliyokwisha ivuka awali inatakiwa afisa utumishi amwandikie barua katibu mkuu utumishi,inaitwa barua binafsi kumuombea mtumishi kupewa madaraja ya mbele kwa kadri inavyofaa.
2.Maabara 10 nchini zimepata hisabati ya kitaifa, 33 zinanyota 1-4. Tuna jumla ya hospitali 28 za mkoa kati ya hizo tisa hazina nyota hata moja. Kuna maabara itajengwa mabibo dsm itakuwa na hadhi ya nyota tatu.
3.Mnashauriwa kutumia mfumo wa kununua reagent kwa kampuni husika ambayo itakuletea mashine bure, hili litapendeza sana baada ya equipment standardisation kukamilika
4.Halmashauri 34 hazitoi taarifa ya damu salama, mkoa wa Dodoma unaongoza kwa utoaji taarifa ya damu salama.
5.Kwenye ubora wa utoaji huduma (star rating), mkoa wa Kilimanjaro unaongoza hasa wilaya ya SIHA yenye zaidi ya asilimia 80 ya vituo vina nyota tatu na zaidi,ikiongozwa na kituo cha Shante
6.Mtetezi mkuu na wa kwanza kwa mtumishi wa afya ni DMO/RMO na wala sio DED/RAS.
7.Hakuna mtu mwenye haki ya kutawala milele hivyo viongozi tuwatumikie wananchi ipasavyo
4.Kwasasa tuna hospitali za wilaya 77
8.Zitajengwa hospitali 67 mpya za wilaya nchi nzima
9.MUHAS wataanza kutoa mafunzo kwa madereva na wahudumu wa ambulance nchi nzima hivi karibuni
10.Kila kiongozi ni lazima aisome na kuielewa miongozo inayomuhusu kwenye eneo lake
11.Hivi karibuni wataajiliwa Biomedical engineers hadi ngazi ya halmashauri ili kukabiliana na service za mashine hospitalini.Vituo vya afya wataajiliwa Biomedical technician.Kwasasa halmashauri ambazo hawana Biomedical technician,ziombe wizarani watapatiwa,kalakana zake zitajengwa kila halmashauri yenye Biomedical technician
12.Vyuo vifuatavyo vitaanza kutoa course za Biomedical services i.e MUHAS, ST JOSEPH na UDSM
13.Asilimia 70 ya marejesho ya NHIF yanaenda private na hiyo inayobaki ndio inabaki serikalini
14.Lengo la CHF ni kuhudumia asilimia 80 ya kaya maskini nchini
15.CHF iliyoboreshwa itaanza rasmi kutumika tarehe 30/09/2018
16.Mamlaka ya uteuzi na utenguzi inaangalia pia ukusanyaji wa mapato kwenye eneo lako la utawala
17.Matibabu ya kutegemea pesa ya papo kwa papo ni dalili mbaya kwa maendeleo ya mwananchi hivyo tuwaamasishe wananchi kutumia hizo bima za afya
18.Manunuzi ya dawa,vitendanishi kwa mshitiri bila idhini ya MSD,na pia kutumia pesa cash ni miongoni mwa vitu vinavyoleta hoja ya ukaguzi
19.Jumla ya halmashauri 181 zilikaguliwa na mkaguzi mkuu CAG,kati ya hizo ni halmashauri 167 zilipata hati safi na halmashauri 14 zilipata hati za mashaka
20.Kila mtumishi inabidi athibitishwe kwenye nafasi aliyopewa baada ya miezi sita
21.Kuacha kazi ni haki ya mtumishi hata kama amesomeshwa na mamlaka husika
22.Kila kituo cha kutolea huduma kitakuwa na website yake,template yake itatolewa.
23.Ili mtumishi awezekupata mafao ya mfuko wa hifadhi lazima awe amechangia si chini ya miaka 15, ikiwa umepata ajali na ulishachangia kwa miaka mitatu,utapata mafao ya elemavu hadi utapofikia miaka 55, ukiwa na watoto (mchangiaji aliye fariki) watalipwa hadi wakifikia umri wa miaka 18 na ikiwa wanasoma hadi miaka 21
24.Ocean Road Cancer Institute ni hospitali ya tano duniani kuwa na mashine za kisasa
25.Asilimia 80 ya vituo vya kutolea huduma Dar Es Salaam ni watu binafsi hivyo viongozi tusuwatenge hao,wote ni wetu
26.Kila hospitali itakuwa na huduma za dharula utaofadhiliwa na bank ya dunia, na muongizo wa huduma unakuja
27.MRDT is the best test for malaria proved by WHO
28.Katibu mkuu kiongozi ndiye mwenye mamlaka ya kutoa kibali cha kumwajili mtu aliyewahi kuajiliwa na kuacha kazi
29.Wizara inaziondoa ADO,AMO na Nurse paedriatric course mwaka huu 2018 hivyo hazita ajirika tena
30.Unaweza kumbadili mtumishi tabia yake kwa kumbadilishia majukumu yake mfano,kuna hospitali X mtumishi mmoja alikuwa anaongea na anadai sana,alipewa jukumu la kudai madeni sugu tanesco,hatimae hospitali ilinufaika vivyo hivyo mtumishi mchelewaji mpe jukumu la kuangalia wachelewaji kazini.
31. *Kiongozi bora hana mda wa kulalamika bali hutafuta ufumbuzi wa matatizo na changamoto kwenye eneo analolisimamia na kwa watu waliochini yake.Kiongozi wa kweli akiongea watu humsikiliza na kumfuata*

C & P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari kama kuna member yoyote aliyesoma hii kozi kuna kijana anaomba ushauri anataka kuapply pale DIT, au hata kama unamjua aliyesoma ,je ni kozi yenye future nzuri?
Nasoma biomedical, Ni kozi nzuri sana na ni mpya sio tu kwa Africa bali dunia nzima. Biomedical ni muunganiko hasa wa medicine (level ya kati) na electronics. Pia ni mjumuisho kidogo wa IT na mechanics. Ni kozi ngumu lakini inavutia sana. Namshauri asome tu bila wasiwasi hatajuta kivyovyote vile. Kusoma ni kuenjoy.
 
Oid mkuu
Mie tayar nimesha apply dit kwa coz iyoiyo ya biomedical science engineering axa nackilizia selection mpaka sasa bad azijatoka..?
 
Hii kozi ni majanga!! Kila halmashauri kuwa na biomedical injinia mmoja wakati watakaohitimu ni maelfu!! Wale wa mwanzo watapata nafasi ila watakaofuata ni majanga!! Kwa sasa hivi wako wahitimu Kwa mamia huko mitaani waliohitimu pale DIT na hao ndio watakaojaza nafasi zote zitakazotangazwa na si wote watakaopata nafasi!! Anayeanza Leo kozi hiyo atarajie maumivu!!!
Ni kama kozi ya petroleum Enginering! Walioanza walipata nafasi lakini wanaohitimu Leo ni maumivu!!
 
Siku manesi wa binadamu wakipungua basi na watu wa biomedical watapungua. Ni kwasababu kwa sasa kazi nyingi wanapewa mashirika binafsi hasa wahindi na wana gharama hatare.
 
Habari kama kuna member yoyote aliyesoma hii kozi kuna kijana anaomba ushauri anataka kuapply pale DIT, au hata kama unamjua aliyesoma ,je ni kozi yenye future nzuri?

asilimia 90 ya hii kozi ni umeme....sio kozi mbaya ni nzuri na soko lake liko poa
 
Nasoma biomedical, Ni kozi nzuri sana na ni mpya sio tu kwa Africa bali dunia nzima. Biomedical ni muunganiko hasa wa medicine (level ya kati) na electronics. Pia ni mjumuisho kidogo wa IT na mechanics. Ni kozi ngumu lakini inavutia sana. Namshauri asome tu bila wasiwasi hatajuta kivyovyote vile. Kusoma ni kuenjoy.
unasoma chuo kipi ndugu
 
Back
Top Bottom