Kwa waliofungua shule za chekechea (Nursery schools)

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
7,377
9,297
naomba mchanganuo kwa wale walio na shule za awali procedure za usajiri shule,,, vitu/ dhana za shule n.k vilivokuwa vinahitajika kabla ya kwenda kwa msajili mashule.
 
naomba mchanganuo kwa wale walio na shule za awali procedure za usajiri shule,,, vitu/ dhana za shule n.k vilivokuwa vinahitajika kabla ya kwenda kwa msajili mashule.
Muhtasari wa shule Malengo na madhumuni, sheria ya serikali- Eneo itakapokuwa ukubwa Eka 2 na nusu na miundo mbinu husika changamoto ambayo wengi wanapata shida- wanafanya njia ya mkato majengo n.k ukiondoa Kiwanja kuna ada na ushuru wa stempu, mmiliki kwa majina. Kwa maswali, uzoefu,changamoto_Ongeza uelewa kimataifa elimu ya awali wanafanya nini kupitia. www.omepworld.org. Na email yangu hansmunis@gmail.com
 
Chuo chao kipo wapi na entry requirements ni zipi? Samahani ningependa kufahamu.

Jaribu kupitia kitu kinaitwa "Early Childhood Education"

Kwa hapa Tanzania kuna vyuo vichache wanatoa Certificate na Diploma.

Ingawa kibongo bongo kuwa mwalimu wa Nursery ni kujua kiingereza tu, ndo maana shule nyingi zimejaa Wakenya na Waganda kwa sababu za kiingereza tu.
 
Asante sana mkuu.
 
Asante sana, syllabus yao nimeipenda imezingatia play as part of learning process, hiyo ni muhimu kwa chekechea

Sasa ukisoma hiyo syllabus na ukaja kwenye uhalisia utakuta ni shule chache sana zinafata huo mfumo, kama ilivyo kawaida yetu wabongo kuchakachua mitaala.

Shule chache sana zina hizo playgrounds, games za watoto, swimming pools etc, hizi utakutana nazo chache ambazo nazo bei zake hazisemeki. Hizi zingine za mil 1-2 hazina hivyo vifaa na hata walimu ni wale wa kujua kiingereza tu.
 
Yah wengi wanapopeleka business proposal inakuwa ya kusadikika na afisa anaekuja kukagua hali halisi anapewa chai. Kwa kweli kwa toys na michezo ya watoto China wameteka soko la dunia. Ila tatizo wao pia wanauza vitu bora kulingana na urefu wa pesa yako. Hata nchi za magharibi wanategemea the majority of children games from China. Nchi zilizoendelea zimepitisha kuwa kila nursery mkuu wa shule awe na degree ya elimu ya awali. Hata kama hao wengine watakuwa na diploma na certificate, na kama hana lazima aajiri mtu mwenye degree. Hii ni kuipa kipaumbele elimu ya awali. Utashangaa kuona kama unamwalimu mzuri hapa ndipo unagundua kipaji cha mtoto kama ni uchoraji, kucheza mpira, kuandika, ingawa hawasisitizi kufundisha mwandiko na hesabu lakini kucheza na crayons kunabuild up motor skills zitakazomsaidia katika kuandika na pia kuanza kujumlisha na kutoa idadi ya vitu kama matunda kwenye picha.
 
Muhtasari wa shule Malengo na madhumuni, sheria ya serikali- Eneo itakapokuwa ukubwa Eka 2 na nusu na miundo mbinu husika changamoto ambayo wengi wanapata shida- wanafanya njia ya mkato majengo n.k ukiondoa Kiwanja kuna ada na ushuru wa stempu, mmiliki kwa majina. Kwa maswali, uzoefu,changamoto_Ongeza uelewa kimataifa elimu ya awali wanafanya nini kupitia www.omepworld.org na email yangu hansmunis@gmail.com
good idea asante.
 
Back
Top Bottom