Kwa wale wenzangu wapenzi wa Miziki ya Kikongo hivi kuna rhumba tamu kama hizi zifuatazo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,034
Nimekuwa ni mfuatiliaji wa miziki ya Kikongo ( DRC ) tokea nikiwa darasa la Kwanza mpaka hii leo nipo katikati mwa Ujanani na Uzeeni lakini sijawahi kuvutiwa na Nyimbo hizi zifuatazo za midundo ya ' Rhumba / Taratibu ' kutoka kwa Mwanamuziki huyu JB Mpiana na Kundi lake zima la Wenge Musica BCBG.

Ni nyimbo ambazo kila siku zimekuwa kama ' Ibada ' Kwangu kwani ni lazima iwe ni asubuhi, mchana na usiku nizisikilize na huwa ' naburudika ' mno kwani zimeimbwa vizuri na kupangika Kivyombo hadi raha. Na ukitaka uzipende hizi Nyimbo tafadhali nakuomba tafuta ' Live ' zake ndipo utaelewa kwamba GENTAMYCINE akipenda ' Kitu ' huwa ni ' Kizuri ' na ' Kimebarikiwa ' hadi na Mwenyezi Mungu.

Tafadhali ewe ' Mdau ' mwenzangu wa ' Miziki ' hii ya Kongo hasa ya ' rhumba / taratibu ' hebu zitafute hizi nyimbo haraka sana upate raha moyoni mwako:

  1. OMBA aliyoiimba JB Mpiana wa Wenge Musica BCBG
  2. GRACA TOI GERMAIN aliyoiimba JB Mpiana wa Wenge Musica BCBG
  3. JEANETTE BOMBOLE aliyoiimba JB Mpiana wa Wenge Musica BCBG
  4. SANS TE TOUCHER aliyoiimba JB Mpiana wa Wenge Musica BCBG
Ukitaka kusikiliza ' rhumba ' za Kikongo zilizoenda ' Shule ' zisikilize hizo Nyimbo Nne ( 4 ) nilizoziweka hapo kwani hazitakuburudisha tu bali zitakufanya pia siku yako iwe njema na iliyobarikiwa sana kwani zina ' baraka ' fulani kwakuwa zimeimbwa pia na Mwanamuziki aliyebarikiwa na Mwenyezi Mungu Jean Bedele Tshituka Mpiana na Kundi lake zima bora si tu duniani bali hadi Mbinguni la Wenge Musica Bon Chic Bon Genre.

Ni bahati mbaya sana Wanamuziki kama Koffi Olomide na Ngiama Makanda Werrason pamoja na ' Kujitutumua ' Kwao kote kuimba lakini mpaka sasa bado hawajaweza kutoa ' rhumba / nyimbo za taratibu ' tamu kama hizo Nne tajwa hapo juu alizoziimba ' Fundi / Mtaalam / Bingwa ' JB Mpiana.

Mercy / Asante

Nawasilisha.
 
Tupia hapahap mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app

Wadau wengine watanisaidia kuziweka hapa Mkuu kwani Mimi ' Ujanja ' wangu wote humu huishia tu katika Kuandika ila kuweka ' Video ' humu JF sijajua kabisa labda kama Wewe au Wadau wengine mnajua basi nawakaribisha mnipe hiyo Elimu kwani nami huwa natamani sana kuwatupieni humu ' mivideo '.
 
Mkuu kwa Rhumba ya Kongo mkali wao ni Ferre Gola kwa sasa. Mimi naweza sema ni mlevi wa rhumba. Huwa nafuatilia sana. Ukitaka kuamini Ferre ni balaa sikiliza kilichomo kwenye hizi albums zake mbili mpya alizotoa kwa pamoja hivi karibuni Album inaitwa QQJD kuna nyimbo kama Ekoti ya Nzube ,Mea Culpa ,Jugement Panzi Likolo Nk. Hapo nimewaacha pia wakali wa rumba kama Didier Lacoste,Simaro Lutumba nk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyimbo nzuri ila mahaba yako kwa JB yamezidi ukaiacha Vita Imana na 100Ans
 
Kuna kitu kinaitwa anisa na festival kafanya koffi na youssour ndour,nikiwa na sikiriza hizi nyimbo,huku na drive ka pamba kangu kepesi,huwa najiona Nina Hera kama mzee Bakhressa,
 
Back
Top Bottom