Mi nafundisha chuo kikuu wale wanaofika mwaka wa kwanza huwa nawapa onyo na maadili ya kuishi chuoni nillichojifunza makundi yanaawaribu sana,kuna vijana nimesoma nao seminary niliwaacha nyuma sana walivyofika huku useminari uliishia getini wakaona kama walikua mbali na dunia,wazazi wetu wanajinyima sana kutusomesha tena katika mazingira magumu sana ila mwisho wa siku tunawaumiza vibaya kwa matendo yetu,wazazi hawazai mtoto aje kuwa kahaba,teja au apate ukimwi akiwa masomoni,wanapoteza pesa nyingi na nguvu kutafuta ada na pesa za kujikimu kifamilia ili usome uje kuwa na maisha bora na wao wajivunie na kufurahia maendeleo yako ya kuwa na kazi nzuri,uoe au kuolewa katika staha hayo ndo matukio ambayo wazazi wetu wanapenda yatokee kwetu na si kusoma kwa taabu miaka mingi na kupata ukimwi ukiwa mwishoni mwa masomo yako maana mambo yote waliyokufanyia ni sawa na kutupa pesa mtoni au kwenye moto na hii hupelekea wazazi kukata tamaa ya kuwasomesha ndugu zako uliowaacha.
pse vijana wenzangu mlioko vyuoni sasa iwe bhaaaaaaaaaaaaaaaasii!bhaaaaaaaaaassi!