Kwa wale wadada wanaotoa mimba someni hii

Kwa wale wadada wanaotoa mimba someni hii

mkali kwanza

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
1,301
Reaction score
1,187
KUTOA MIMBA

Mama mmoja huku akiwa anawasiwasi alienda kwa daktari wa magonjwa ya akina mama na akamwambia
" mwanangu hajafikisha hata mwaka mmoja na mimi nimepata ujauzito tena"
Daktari akamwambia
"ni sawa, kwa hiyo unataka mimi nifanyeje?"
Mama akasema
"nakuomba unisaidie kutoa hii mimba na ninakutegemea mno daktari tafadhali nisaidie"
Daktari baada ya ukimya mfupi na kufikiri kidogo akamwambia yule mama
" Nadhani ninao msaada mzuri zaidi na ambao hautakuathiri kwa kwa namna yoyote kiafya"
Mama huyo huku akiwa na furaha na matumaini ya kusaidiwa vizuri zaidi pasipo hatari kwa afya yake kama alivyoomba, alitabasamu na kuendelea kumsikiliza daktari,
daktari akasema
"unajua, ili usipate shida ya kulea watoto wadogo hivi wawili kwa wakati mmoja, hebu tumuue huyu ambae umempakata. Kwa msaada huo utapata muda wa kupumzika kabla ya kuanza kulea tena hadi huyu azaliwe na pia hii haitathiri afya yako, napia kumuua huyu ni rahisi zaidi kuliko aliyeko tumboni" Mama akamwangalia daktari kwa hasira na kwa ukali na kumwambia
"he! Haiwezekani daktari, hivi wewe unaakili timamu, unawezaje kufanya hivyo, kwanza ni kosa kisheria kuua mtoto!"
Daktari kwa upole akamjibu
"ni kweli ni kosa nafahamu hilo lakini inaonekana kwako siyo tatizo kuua mtoto wako mmoja wapo, na ndiyo maana nilidhani kumuua huyu uliyempakata ingekuwa rahisi kuliko huyo tumboni, kwanza kumuua huyo wa tumboni anaweza akasababisha kifo chako pia"
Daktari huku akiwa anafuraha kuwa somo limeeleweka akamwambia mama yule
" hakuna tofauti kati ya kuua mtoto ambae ameshazaliwa na yule atakayezaliwa baadae, yote ni makosa kisheria na ni dhambi inayolingana".
Daktari akamwambia tena "usitoe uhai wa mtoto aliyeko tumboni kwaajili ya maisha mazuri ya mtoto aliyekwisha kuzaliwa au kwaajiri ya kupenda kupata muda wa kupumzika wewe mwenyewe. "
Kama unakubaliana na msimamo huu wa daktari watumie watu wengine ili wasirahisishe utoaji mimba eti tu kwa sababu mtoto yule hajazaliwa na hawezi kujitetea
 
Dah, kweli nimeamin JF kuna watoto...
Hivi unadhan kutoa Mimba ni issue ngum kiivo?
Btw hakuna daktar mpumbavu namna hiyo
Pili ; unadhan kulea watoto kwasababu Tu yai limerutubishwa ni kaz rahis Kwa maisha ya leo?
Ndo maana kuomba omba hakutuishi...
 
mkuu umesoma na kuelewa au umekuja mbio mbio na kuanza kumwaga povu?
 
Kutoa Mimba ni dhambi na Mungu atadai uhai wa huyo mtoto siku ya hukumu.
 
Dah, kweli nimeamin JF kuna watoto...
Hivi unadhan kutoa Mimba ni issue ngum kiivo?
Btw hakuna daktar mpumbavu namna hiyo
Pili ; unadhan kulea watoto kwasababu Tu yai limerutubishwa ni kaz rahis Kwa maisha ya leo?
Ndo maana kuomba omba hakutuishi...
Wakati ukiamini JF kuna watoto wengine wanaamini kuna wakubwa wajinga wengi sana.
Hayo maswali uliyouliza ungeelewa mantiki ya hii mada usingeuliza hivyo.
Ulichoelewa wewe na ukubwa wako ni kwamba kilichoelezwa kimetokea hospitali fulani hapa nchini kati ya daktari fulani na mama mmoja hivi.
Halafu kwako wewe ugumu wa maisha husababishwa na watoto wengi , wangapi wako single kutwa nzima wanaomba jero ya chakula tu?
 
kwa majibu haya hiyo AVATAR huitendei haki. inaonekana wewe ni mhanga.
 
Wakati ukiamini JF kuna watoto wengine wanaamini kuna wakubwa wajinga wengi sana.
Hayo maswali uliyouliza ungeelewa mantiki ya hii mada usingeuliza hivyo.
Ulichoelewa wewe na ukubwa wako ni kwamba kilichoelezwa kimetokea hospitali fulani hapa nchini kati ya daktari fulani na mama mmoja hivi.
Halafu kwako wewe ugumu wa maisha husababishwa na watoto wengi , wangapi wako single kutwa nzima wanaomba jero ya chakula tu?
Hospitali yenye wajinga wa namna yako labda...
Nilitamani nikueleweshe uhusiano was moja Kwa moja wa umasikini na watoto wasio na mpange.. Ila kwakuwa unaonesha ujuaji ..Pambana na Hali yako
 
Back
Top Bottom