KWA WALE MNAOTAFUTA KAZI

mkali kwanza

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,301
1,180
Napenda kuwapa dondoo muhimu wale vijana wenzangu ambao mnatafuta kazi mambo ya msingi ya kuzingatia ili upate/kufanikiwa kupata kazi.
1. Kufanya utafiti wa kutosha kuhusu kampuni/taasisi unayotaka kuajiriwa. Unaweza kufanya tafiti kwa kuuliza watu wanaofanya kazi,walikwishafanya kazi,kuperuzi kupitia mtandao.
2.Kuyaelewa majukumu ya kazi ambayo umeiomba.Usiombe kazi ambayo unajua kabisa hata ukiulizwa majukumu yake utashindwa fanya kautafiti kadogo ili ujue majukumu ya msingi ya kazi husika uliyoomba.
3.Mpangilio wa CV(Biodata) au resume. Waajiri wengi hawapendi sana kusoma CV zenye maelezo mengi maana huona kama ina poteza muda na maombi huwa ni mengi. Kuna aina nyingi za uandishi wa CV ambazo zinaweka maelezo na ya kueleweka ili kumvutia mwajiri,baadhi ninazo.
4.Muonekano wako.Kumbuka muonekano una nafasi kubwa sana katika kufanikiwa/kutofanikiwa kwako kupata kazi. Hakikisha unakuwa smart,umevaa mavazi ya heshima,usivae nguo ya kuchoresha mwili wako.Na usivae mlegezo au kutembea kisharobaro
5.Mwitikio wako na matendo yako.Waajiri wengi humpima mtu katika namna anavyoitikia,majibu yake na matendo yake na hapa wengi wetu kama hutokuwa makini unafeli mfano umeingia chumba cha interview hujagonga mlango umeingia tu straight unaenda kukaa pale mwajiri unakuwa ushampa maana kwamba kumbe wewe unavijitabia flani vya kitemi.
6.Wakati wa usaili inaruhusiwa kujibu maswali kama ukiwa na nyaraka za kusapoti jibu lako. Labda nitoe mfano mim wakati nafanya interview mahali flani niliulizwa kuhusu takwimu za utendaji wangu wa kazi mahali nilipokuwa nafanya nilitoa karatasi ya kurasa mbili nikawapa wakashangaa sana na ikanibeba sana nikapata nafasi.Kwa hiyo kama unaweza kufanya hili binafsi litakuongezea sifa mno na uwezekano wa kushinda usaili ukawa ni mkubwa hasa huu usaili wa ana kwa ana(oral interview)
Nimeona kwa leo nishee hii kitu kwa vijana wenzangu ila kama kuna maswali karibuni
Haya mambo niliyoyaandika ni kutokana na uzoefu wangu wa sehemu za kazi nilizopitia kwa hiyo huenda wengine mlipitia experience tofauti tunaweza kushea
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom