Kwa wajuzi wa Tractor za Massey 290 au 385 ipo bora kwa kulimia

Shukran
 
385 ni kubwa kuliko 290? Unaangalia nn? Hizo namba au. Haupo sahihi. So ww unataka kuniambia 365 ni kibwa kuliko 290 sio
 
385 ni kubwa kuliko 290? Unaangalia nn? Hizo namba au. Haupo sahihi. So ww unataka kuniambia 365 ni kibwa kuliko 290 sio
Katika picha za tractor zilizotumwa humu na alieleta hii mada umeona wapi hiyo 365? Kuna sehemu umeona nikiongelea hiyo 365? Sijaangalia namba. 290 MF ni horse power kati ya 75 hadi 78 hivi bila kujali kama 2wd au 4wd(humu imewekwa picha ya 2wd), 385 MF ina hp kati ya 80 hadi 85 bila kujali pia kama ni 2wd au 4wd(humu imewekwa ya 4wd). Kwa vigezo hivyo nadhani utajua ipi ni kubwa.

Sijui kuhusu hiyo 365MF ila, 360MF hp ni 60. So kati ya 290 MF na 365MF(ambayo siijui) nadhani 290 itakua kubwa. Nasema nadhani kwasababu siijui kabisa hiyo 365 ila kwa kufuata series ya 360s itaifanya 365 kuwa ndogo
 
Ukubwa wa trekta mimi huwa siangalii body appearance. Naangalia horse power. Nimejibu kulingana na ninavyofahamu.
 
Nilikua nawazo la kutafuta trekta na bajeti yangu iliku mill 20
Ntafanikiwa?
 
Umenena vyema.
 
Nakupa siri ya Massey ambayo wengi hawaijui. Yaliyosemwa hapo juu yote ni sahihi kuhusu MF. Ugonjwa mkubwa wa MF ni Hydraulic system yake (mikono ya kuinua jembe) inachoka mapema na ikichoka haina dawa...
Mkuu shukrani sana kwa maelezo yako, naomba kujua kuhusu Newholland za Suma ni za kutoka nchi gani ?pia zipi changamoto zake?
 
Mkuu shukrani sana kwa maelezo yako,naomba kujua kuhusu Newholland za Suma ni za kutoka nchi gani ?pia zipi changamoto zake?
New holland za Suma nyingi ni TT75.
Engine maker: IVECO.
4 CYLINDERS.
LIQUID COOLED.
FUEL: DIESEL
ENGINE MODEL: BOOMER SERIES CASE DX
4WD or 2WD.
Ni wewe unataka ya HP ngapi.
New Holland ni trekta simpo sana kwa maana ya vipuli na service. Oil yake haifiki 100,000. Filter zake ni cheap ukilinganisha na John Deer. Vifaa vyake ni vingi ila sema uwe makini na fake hasa unapofanya overhaul.

Cylinder head gasket kit. Cone bearing,main bearing na piston rings uwe makini nazo uzichukue kwa trusted supplier. Ukihitaji trekta naweza kusaidia ukapata trekta zuri New Holland ukafurahia maisha.
 
New holland za Suma nyingi ni TT75.
Engine maker: IVECO.
4 CYLINDERS.
LIQUID COOLED.
FUEL: DIESEL
ENGINE MODEL: BOOMER SERIES CASE DX...
Ubarikiwe kwa maelezo mazuri. Kuna New Holland TT 65 inauzwa na kampuni ya CMC Motors au pia wanajiita Hughes Agriculture Ltd,naomba maelezo kidogo kama hautojali, pia kama una ABC ya New Holland za hawa jamaa
 
Nilikua nawazo la kutafuta trekta na bajeti yangu iliku mill 20
Ntafanikiwa?

Huwezi kupata trekta ya maana kwa milioni 20. Ingawa unaweza kupata trekta ndogo MF135 kwa 14 Milioni. Lakini hiyo ni trekta ndogo sana na haiwezi kuvuta jembe la disc 3. Mara ya mwisho niliyakuta pale roundabout junction ya Kawawa Road na Kigogo. Kama unatokea Ilala, ukifika Roundabout shuka na barabara ya kulia inayokwenda shule ya msingi Darajani. Utayaona upande wa kushoto.

Kuhusu MF385, Uingereza hawajawahi kutengeneza MF 385. Zote hizo zimetoka pakistani. Kuhusu MF 290, ukiliona jipya, basi ujue limetoka pakistani. Ukiliona limezeeka lakini zima, hilo limetoka UK.
 
Mkuu vipi kuhusu URSAS hizi za NDC
 
Ukikwama sehemu tushirikishe pia. Tuendelee kusaidiana kadri tuwezavyo
Blacksamurai, nimekuelewa sana ndugu nimekua nikikuatilia juu ya ufafanuzi wako kiukweli nimepata elimu zaidi kupitia wewe umenipa nguvu ya kuwa na shauku ya kununua mashine ya kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…