Kwa wafugaji wa nguruwe Morogoro Mjini

man of sun

JF-Expert Member
Apr 24, 2020
331
460
Me ni mkazi wa morogoro mjini ningeomba mfugaji yeyote anaye fuga nguruwe hapa Morogoro mjini aje dm anipatie namba pia Kuna baadhi ya vitu nataka nifahamu kuhusu nguruweee kwakua Nina mtaji kwaiyo nataka nifahamu jinsi ya ufugaji pia ili nianze kufuga mara moja ndani ya mwezi huu please Niko serious naomba mfugaji ujitokeze maana unaweza faidika pia. Thanks
 
Mcheki huyu +255 677 083 905 muombe akuweke kwenye whatsapp grup la wafugaji wa nguruwe. Humo hutakosa wafugaji wa Morogoro
 
Karibu kwenye ufugaji mkuu .......zingatia kutumia nguvu kubwa wakat nguruwe bado wadogo utatumia muda mfupi sana

Mmi huwa natumia miez 4 na napga pesa
 
Nimetembelea wafugaji wengi wa Nguruwe wanakabiriwa na tatizo la Usafi.
Nakutana na Banda na Mazingira Machafu na Harufu kali na mbaya sana.
Lazima Wafugaji Nguruwe wahakikishe kwanza wanajiandaa vizuri pamoja na kuboresha mazingira ya ufugaji.
Chimba kisima cha maji mengi kwa ajiri ya Usafi, Zungushia Fensi eneo la Ufugaji.
Chimba karo kubwa la kutiririsha uchafu wa mavi ya nguruwe liwe kama lile la choo cha Binadamu na kuwekwa Bomba refu la kupaisha harufu ya uchafu hewani.
Hapo unaweza furahia hali ya Hewa ya eneo la ufugaji kwa kupata Hewa safi.
Kila asubuhi watoe Nguruwe nje ya banda na ufanye Usafi bandari huku ukitumia maji kusafisha banda na kuliacha hadi likauke kabla ya kuwarudisha tena bandari.
Zingatieni USAFI.
 
Me ni mkazi wa morogoro mjini ningeomba mfugaji yeyote anaye fuga nguruwe hapa Morogoro mjini aje dm anipatie namba pia Kuna baadhi ya vitu nataka nifahamu kuhusu nguruweee kwakua Nina mtaji kwaiyo nataka nifahamu jinsi ya ufugaji pia ili nianze kufuga mara moja ndani ya mwezi huu please Niko serious naomba mfugaji ujitokeze maana unaweza faidika pia. Thanks
Mkuu, umefanikiwa kumpata mfugaji anaefuga sasa na kukupa mwongozo wa ufugaji? kama umefanikiwa nijulishe na mimi, maana ninauhitaji kama wako.
 
Back
Top Bottom