Kwa waelewa tu: Makamu rais kutii amri kwa mwasisi wa chama au kwa rais wa zanzibar?

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Wakuu samhani, naomba tutoke nje ya box tujadiri jambo hili kwa kina. Kwa mtazamo wangu baada ya uchaguzi yafutayo yanaweza kutokea.
CUF KUCHUKUA NCHI na kufanikiwa na mpango wao wa siku nyingi kuvunja Muungano. Kwa nini CUF wanaweza kuchukua nchi?

Kuna tetesi kwamba CUF wamekuwa wakishinda Zanzibar lakini wamekuwa wakipokonywa ushindi, rejea maelezo ya Mzee Moyo wa Zanzibar, CUF bado wana nguvu huko Zanzibar, hivyo uwezekano wa kushinda ni mkubwa. Katibu mkuu wa CUF mheshimiwa SEIF SHARIF HAMAD ndiye mmiliki wa chama hicho na ndiye alimteau Ndug JUMA DUNI HAJI kuwa mgombea mwenza wa CDM. Mpango huo uriratibiwa na Mhishimiwa Mbowe kwa makubaliano maalumu na Maalimu SEIF.

Pia Bara kuna uwezekano UKAWA wakashinda yafuatayo yanaweza kutokea, Rais atakuwa Mheshimiwa Edward Lowassa, ni mchapa kazi mzuri labda afya yake imletee mgogoro. Iwapo afya yake itateteleka basi kiasi kwamba atashindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za nchi, itabidi makamu wake Ndg JUMA DUNI HAJI atakuwa Rais kwa kipindi kitakachokuwa kimebaki. Hivyo basi DUNI NA SEIF wanaweza kutimiza mipango yao ya siku nyingi ya kuvunja Muungano na kutunga sheria za kuweka mipaka mipya ndani ya Bahari kuu, hivyo kuleta msuguano kama siyo vita vya Tanganyika na ZNZ kwaani nasikia kuna mgogoro ulio kimya kuhusu mipaka ya Zanzibar na Tanganyika ndani ya bahari kuu kwenye Rasilimali nyingi za mafuta na gas.

Najua wengi watjibu kuwa Rais hatakuwa na mamlaka ya kufanya maamzi peke bila kukishirikisha chama chake yaani CHADEMA, lakini kumbuka kuwa katiba yetu inasema kuwa Rais akishaapishwa hataruhusiwa kufuata maamzi ya mtu yoyote wala kuingiliwa.

Hatari kwa CDM kupokonywa Urais: ni pale ambapo Rais hatakuwa tayari kufuata maelekezo ya mwasisi wa chama Mheshimiwa Mzee Mtei, Je Duni ataamua kutii kwa mwasisi wa chama kupitia kwa Mkwe wake, au Kutii amri ya aliyempendekeza kuwa mgombea mwenza mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamadi?

Aksanteni
 
wewe unaongelea LOWASSA AKISHINDWA MAJUKUMU YAKE KWANI MAGUFURI HAWEZI KUSHINDWA NA SAMIA AKAWA NDIYE MMBADALA WAKE? JE HAPO NINI KITATOKEA?
 
Mùungano eeh.. duni akivunja Muungano umakamu wa rais utakuwaje..ila mie binafsi si muumini wa muungano so poa tu ..tunataka mabadiliko
 
Mùungano eeh.. duni akivunja Muungano umakamu wa rais utakuwaje..ila mie binafsi si muumini wa muungano so poa tu ..tunataka mabadiliko

Je mafuta na gas? kwa sababu mipaka ya Tanganyika ni mpaka mbele ya Zanzibar, huku ZNZ mipaka yake ni maili kadhaa tu kuzunguka kisiwa. Je wazanzibar watakubali hilo ay Tanganyika itakubari kuiachia ZNZ? ZNZ inaweza kuweka mambo yao sawa kupitia SEIF AKIWA RAIS ZENJ HUKU JMT AKIWA DUNI HAJI.
 
shikulaushinye,

..serikali ya Tgk ikiundwa hutasikia migogoro ktk muungano wetu.

..pia sheria za kimataifa kuhusu uvunaji wa rasilimali zilizoko ktk bahari kuu ziko wazi.

..kama kuna mgogoro kuhusu mpaka ua rasilimali basi muamuzi ni mahakama ya kimataifa.
 
Last edited by a moderator:
shikulaushinye,

..serikali ya Tgk ikiundwa hutasikia migogoro ktk muungano wetu.

..pia sheria za kimataifa kuhusu uvunaji wa rasilimali zilizoko ktk bahari kuu ziko wazi.

..kama kuna mgogoro kuhusu mpaka ua rasilimali basi muamuzi ni mahakama ya kimataifa.

Gas na mafuta hawawezi kupewa, thubutu.
 
Gas na mafuta hawawezi kupewa, thubutu.

..muungano wa mabavu hauna nafasi ktk zama hizi.

..tuitishe kura ya maoni kuhusu suala la muungano.

..mimi naamini wengi wanataka muungano. Zaidi tutamaliza mivutano ya serikali tatu,mbili, au mkataba.
 
..muungano wa mabavu hauna nafasi ktk zama hizi.

..tuitishe kura ya maoni kuhusu suala la muungano.

..mimi naamini wengi wanataka muungano. Zaidi tutamaliza mivutano ya serikali tatu,mbili, au mkataba.

Muungano wengi wanautaka lkn siyo wa kuweka mipaka upya. maana mpaka wa Tanganyika upo km 5 kutuka forodhani Zanzibar. na upande mwingine ni mbele ya Zanzibar ndani ya bahari kuu.
 
Muungano wengi wanautaka lkn siyo wa kuweka mipaka upya. maana mpaka wa Tanganyika upo km 5 kutuka forodhani Zanzibar. na upande mwingine ni mbele ya Zanzibar ndani ya bahari kuu.

..masuala yote baina ya Tgk na Znz yanapaswa kufuata sheria.

..masuala unayoyazungumzia yapo ktk sheria za mipaka ya bahari. Sheria hizo ni za kimataifa.

..katika sheria hizo kuna maelekezo na miongozi kuhusu mipaka ya baharini ya nchi zinazokaribiana kama ilivyo kwa Tgk na Znz.

..suala la mipaka ni lazima liwekwe wazi kwa mujibu wa sheria za kimataifa ili kuepusha migogoro na kuhakikisha muungano wetu unadumu.
 
Back
Top Bottom