Kwa wabunge wa CHADEMA... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wabunge wa CHADEMA...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jackbauer, Feb 9, 2011.

 1. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kwanza kabisa natoa pongezi nyingi kwenu kwa kuchaguliwa au kuteuliwa ili muweze kutetea maslahi ya wananchi wote wenye itikadi mbalimbali.
  Baada ya wananchi kuridhishwa na kazi iliyofanywa na wabunge wachache wa chadema miaka mitano iliyopita waliamua kuongeza idadi yenu wakitarajia mambo makubwa zaidi kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
  Hakuna ubishi kwamba CDM ni chama cha siasa kilichojijengea heshima na uaminifu mbele ya watanzania kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.kutokana na ukweli huu CDM imeongeza idadi ya maadui wakiongozwa na CCM ambaye ni adui hatari aliyejeruhiwa.kuna mambo matatu ambayo CCM kama majeruhi anaweza kufanya:
  1.FEAR-hili ni jambo la kwanza lilotokea/linaendelea kutokea.
  2.FIGHT-hili ni jambo la pili linaloweza kutokea iwapo CCM inaamini kuwa uwezo wa kupambana na CDM upo.
  3.FLIGHT-hili litatokea pale CCM itakapoona kuwa CDM is like a giant na hivyo kuamua kujiweka pembeni/kukimbia kama kunguru.

  Nionavyo CCM watatumia reaction ya pili,wataamua/wameamua kupambana.ni haki yao kupambana tena kwa kutumia mbinu zote(pamoja na coalition zisozokuwa rasmi) kabla ya kuamua kukimbia.

  Hivyo waheshimiwa wabunge wa CDM mko kwenye vita kali sana huku mkiwa na vifaa duni lakini mnayo SILAHA moja nayo si nyingine ni 'spirit' ya wapenda mabadiliko ambao ni wengi na wanaendelea kuongezeka.
  Mpigane kufa na kupona bila kutumia panga au ngumi bali hoja thabiti zinazogusa maslahi ya umma wa watanzania.waacheni wengine waendelee na 'mipasho' wakati nyinyi mkitoa lyrics za ukombozi.

  Asanteni kwa kunielewa.
  MUNGU IBARIKI TANZANIA!!
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!

  [​IMG]


  22.JPG

  525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

  Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

  Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

  Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

  Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

  Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

  Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

  Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

  Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

  Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

  (1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

  (2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

  (3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

  Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kafulila ni kijana mdogo anayehitaji counselling!
  Nilimsikia akitoa porojo pale bungeni,sijui kwa nini anataka kulazimisha coalition hata pale demokrasia inapokataa kufanya hivyo.chama chochote kinaposhinda kwa 60% hakihitaji kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwani kitakuwa na uwezo wa kuunda serikali na uwezo huo wanapewa na wananchi(60%).
  sielewi kwa nini anashindwa kuimbia CCM bara kuunda serikali ya umoja wa kitaifa badala yake anakomalia CDM kuungana na vyama vingine.
   
 4. k

  kigumu twawala Member

  #4
  Feb 9, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kitu kingine ambacho wanatakiwa hawa cdm ni kuwa makini sana katika kila wanachofanya na kuchangia bungeni. ccm, spika naibu wake na wapinzani mamluki wanatumia character assassination kwa kuwalenga baadhi ya wabunge wa cdm na matendo ya cdm, kutaka kuionyesha jamii ubaya wa cdm, sasa cdm wanatakiwa wajue hilo na walipatie dawa.
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ndio maana nasisitiza wabunge wa CDM wapigane kwa kutumia hoja.wengi wa wabunge wa CCM ni bogus,wavivu wa kutafuta facts na ni watu wa mipasho na ndio mzee.kiufupi CCM imezeeka na haina mvuto kwa vijana(hata kikwete kathibitisha hilo),vijana ndio wapiga kura wa 2015.

  "HE ALONE WHO OWNS THE YOUTH GAINS THE FUTURE" aliwahi kusema Adolf Hitler.
   
 6. kinja

  kinja Senior Member

  #6
  Feb 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Watu wema hufikiria kuwa pamoja na kuungana kwa wema ili kuleta maendeleo ya demokrasia kwa watz. Watanzania wengi tunakosa uzalendo wa nchi badala yake tumeweka mbele zaidi maslahi binafsi, chama hata dini wakati mwingine. Nilipendezwa sana na timu ya upinzani katika bunge lililopita ambao mh. 6 alilijengea heshima.
   
 7. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Wakati wa ukombozi umewadia. Cdm ijipange kisawasawa kuna mengi zaidi ya hili la kambi ya upinzani. wategemee challenges nyingi sana.
  maana ccm wamejipanga haswa kuwatibua. na sisi tunawaunga mkono msikate tamaa wabunge wetu
   
 8. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kusema katika kutafuta kushika dora Chadema na wabunge wake wasitegemee mtelemko toka CCM wajue wanayepambana naye bado anakitaka hicho kiti kwa hiyo atafanya kila hila ili abakie madarakani, vitendo wanavyofanyiwa CDM sitaki kuvitetea lakini naamini ni changamoto tosha kwao.

  Kama mwanzisha mada alivyosema CCM sasa imejawa na hofu imekuwa kama mnyama, na mnyama akijawa na hofu matokeo yake ni kung'ata chochote kilicho karibu yake. CCM imejeruhiwa sasa inataka kuonyesha kuwa bado ina makucha.

  Mara nyingi watawala wakiishiwa hoja na wakiona siku zao zinakaribia silaha yao ya mwisho ni kutumia nguvu, baada ya Mubarak kuona hana hoja dhidi ya wananchi wa Misri akaona atumie nguvu ambayo ni silaha ya mwisho lakini sijui kama atafanikiwa.

  CCM ya leo si ile ya 1977 imepoteza mvuto kwa wananchi silaha yao iliyobaki ni kutumia nguvu za wazi CDM wasijidanganye CCM wataona aibu kwa hilo kama walivyobadili kanuni Arusha na jana tumejionea wakibadili kanuni, silaha hii wakiona haifanyi kazi itakayofuata ni kutumia dora na jeshi kuwatisha wananchi. So CDM SHOULD BE PREPARED FOR THAT.
   
 9. z

  zamlock JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  sisi kama wanachadema tuko pamoja mpaka kieleweke atutarudi nyuma tutazidi kuwaunga mkono na kuwapa moyo
   
 10. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ni vizuri picha halisi imeshajionesha, kuanzia spika,naibu wake mpaka wabunge wa ccm na vibara wao wamewakamia wabunge wa cdm. Kinachotakiwa sasa ni chadema kujipanga jinsi ya kusepa mitego yao na kujenga hoja za nguvu. Wafanye mambo yote kwa busara. Wakati wenzao wakiendeleza siasa bungeni, wao wapeleke na kuchangia hoja kwa maslahi ya taifa na si maslahi ya chadema.

  Tunasubiri kwa hamu operation ilitotangazwa kufanyika nchi nzima hasa vijijini.
   
Loading...