Kwa Vitendo vya Uwizi wa Mafuta walivyofanya Marehemu Waume zao pale Msamvu Morogoro wanastahili Misaada?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,912
Mwananchi Online:

" Wajane wa waliokufa ajali ya moto Morogoro waomba msaada "

Huenda leo ndiyo ikawa Siku yangu njema kabisa ya Kuwajua Watanzania Wanafiki na wanaojifanya wana Huruma lakini hawataki Kuangalia Chanzo au Kisababishi Kikuu cha tatizo Kubwa ambalo limepelekea Umauti wa Wahusika.

Na Uchunguzi unasema kuwa 98% wa wale Waliokufa walikuwa ni Wezi wa Mafuta na 2% ni ya wale ambao hawakuwa na Hatia hiyo. Na Uchunguzi umeenda mbele zaidi na Kugundua ya kwamba hao hao Marehemu wakati wakiwa wanataka Kuiba Mafuta waliambiwa tena kwa nia njema tu kuwa wasiende lakini wengi wao wakawa wanawajibu Matusi hao Washauri na wapo ambao pia waliwapiga hadi Kuwatishia Maisha hao hao Washauri.

Eti tuwasaidie Wajane wao. Thubutu! Yaani Tusaidie Wajane wa Wezi? Katika hili wala An Eagle nisiwe Mnafiki hakuna Kusaidiwa hawa Wajane ili iwe Fundisho kwa ' Wapumbavu ' wengine kwa Siku za baadae pale wakiwa wanaonywa kutoiba Mafuta wawe wanasikia na Kutii.

Kama una Hela yako nenda Kasaidie Wajane wengine ambao kweli Vifo vya Waume zao vimetokana na Matatizo ( Magonjwa / Kiafya ) tu ya Kiasili au labda Ajali ya Bahati mbaya au zikikuwasha sana wapelekee Watoto Yatima utakuwa umefanya la maana mno na nina Uhakika hata Mwenyezi Mungu atakubariki lakini siyo kuwapa hawa Wajane ambao Vifo vya Waume zao ni vya Kujitakia.

Najua mpo mtakaonichukia kwa huu Ukweli wangu Mchungu ila tuvumiliane tu na acheni Sindano iwaingieni kisawasawa hasa.

Je, mtawasaidia hawa Wajane?
 
Kumbuka hao si wezi, bali waume zao ndio walikuwa wezi.
Je tuwahukumu wao kwa makosa ya waume zao?
 
Kumbuka hao si wezi, bali waume zao ndio walikuwa wezi.
Je tuwahukumu wao kwa makosa ya waume zao?

Na nina uhakika hawa hawa Wajane endapo hao Marehemu Waume zao wangefanikiwa Kuiba Mafuta na ama Kuyauza au Kuyatumia na Kujipatia Kipato hawa hawa Wajane wangekuwa wanaringa Mitaani, wanajivunia na hata Kumuona mwenye hilo Lori la Mafuta ni mwenye Akili za ' Kipa Katoka / Mpumbavu ' ila leo kwakuwa wameona Waume zao wameishia Kubaya ndiyo wanajifanya Kutia Huruma na Kuomba Misaada.

Watanzania acheni Unafiki wenu wapo Watu ( Wajane ) ambao kweli wanahitaji Misaada yetu / yenu ila siyo hawa. Hakuna kuwapa.
 
Hii comment imenichekesha khaa

Bila shaka kama ukimjua aliyeitoa ni Mwanaume ( huku Wewe ukiwa ni Mwanamke ) na mkaonana ana kwa ana hutoweza kabisa Kumyima Asali yako iliyoko ' Mafichoni / Upenuni ' Upande wa Kusini mwa Mwili mwako.
 
Mama yangu ni mjane wa siku nyingi, anahitaji msaada. Au wa kusaidiwa ni hao tu? Hebu watupishe
 
Eti tuwasaidie Wajane wao. Thubutu! Yaani Tusaidie Wajane wa Wezi? Katika hili wala An Eagle nisiwe Mnafiki hakuna Kusaidiwa hawa Wajane ili iwe Fundisho kwa ' Wapumbavu ' wengine


Unamhukumu asiyehusika na kosa tajwa, yawezekana hao wajane hata hawajui kama waume zao walikwenda huko, yawezekana kuna misaada mingi unatoa kwa watu wenye hatia bila wewe kujua, by the way msaada huwa si lazima kutoa, una hiari ya kukaa kimya na usitoe au ukahamasisha wengine watoe kulingana na imani yao na hasa kama haihubiri malipizi.
 
Unamhukumu asiyehusika na kosa tajwa, yawezekana hao wajane hata hawajui kama waume zao walikwenda huko, yawezekana kuna misaada mingi unatoa kwa watu wenye hatia bila wewe kujua, by the way msaada huwa si lazima kutoa, una hiari ya kukaa kimya na usitoe au ukahamasisha wengine watoe kulingana na imani yao na hasa kama haihubiri malipizi.

Hakuna Kuwasaidia bali wasaidiwe Wajane wengine na Watoto Yatima. Waume zao wamejitakia wenyewe na wala siwahurumii.
 
Hakuna Kuwasaidia bali wasaidiwe Wajane wengine na Watoto Yatima. Waume zao wamejitakia wenyewe na wala siwahurumii.


Kuwahukumu Wengine(Luka 6:37-38, -42) # 1Kor 5:12; Yak 4:11-12 “Usihukumu ili usije ukahukumiwa. #Lk 6:38; Rum 2:1Kwa maana jinsi unavyowahukumu wengine .
 
Wewe badala ya kushauri vijana wenzako wawaowe hao wajane ili kuwasetiri, wewe unawajengea chuki binafsi! Kumbuka hao siyo wezi, hata sheria haikubali kosa la mtu, kuhamishiwa kwa mtu mwingine.
 
Back
Top Bottom