majoto
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 2,442
- 4,325
Ni kipindi cha msiba mkubwa kwa kufiwa na watoto wetu. Nawapa pole wote walioondokewa na watoto wao Mungu awape moyo wa subra na faraja kuu.
Wewe unafikiria nini, je ni Mungu kapenda watu wafe kutokana na uzembe wetu?
Imekuwa ni tabia zetu kila inapotokea ajali hata za uzembe uzembe tu, kuhalalisha uzembe wetu na kusema Mungu amependa. Utakuta gari zinaendeshwa kizembe, hazitunzwi hazina service, madereva wanafanya uzembe, wanakimbiza magari, ajali zinatokea watu wanakufa basi tunahalalisha kwa kusema Mungu kapenda.
Ifike mahali tuache ujinga na uzembe huu katika vyombo vya usafiri tunavyotumia. Tumeona siku hizi ajali zimekuwa chache ukilinganisha zamani kwa sababu tumejaribu kudhibiti mwendo na kuviangalia vyombo vya usafiri. basi tuendelee kuwa makini na ajali zitaendelea kupungua.
Utasema Mungu ameruhusu, sasa ulitegemea nini kuendesha gari bovu, au kwa speed au uzembe wa aina yoyote halafu ajali itokeee bila vifo? Inapotokea umeumia vibaya, umepasuka moyo, umemwaga damu nyingi ni wewe umesababisha kifo sio Mungu ameruhusu. Sasa moyo umeshapasuka, damu imemwagika, matumbo yametoka nje, unataka muujiza usife?
Madaktari wanafanya uzembe, wagonjwa wanakufa, eti Mungu kapenda. Nasema hiviiiii vifo vya uzembe uzembe msimsingizie Mungu.