Kwa uvccm-tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa uvccm-tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jethro, May 11, 2010.

 1. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Nimetafakari kwa ukaribu na nikakuta UVCCM ndio umoja wa vijana hapa nchi ambao una vijana wengi waliojiunga katika ummoja huo, na ndio kama inavyodaiwa na CCM ndio wapiganaji wao katika shughuri esp za kampeni katika chaguzi nyingi tu hapa nchi kutokea shina mpaka taifa.

  Kuna mambo machache tu nilipenda kujua na kuuliza katika umoja wa vijana UVCCM ni wangapi wametanguliza nchi(COUNTRY FIRST) nikiwa na maana gani kuwa katika umoja wao huo ndio unakuta vijana wana dhamana kubwa ya kumpitisha mgombea ambae wao wanaona anafaa na yuko kwa ajili ya wananchi(Kimaendeleo zaidi na sio Kisiasa).

  Je ni idadi yenu ni ngapi ?ya wagombea katika nafasi zozote tokea shina mpaka Taifa eg Ubunge?

  Je ni idadi ngapi ya wazee waliogembea au wanaoshika nyadhifa hizo tokea shina mpaka taifa na nafasi zingine zikiwemo Ubunge?

  Kwa ummoja wenu huo huo wa UVCCM kama vijana kweli mmeweka nchi kwanza? KAULI MBIU YENU YA UVCCM NI IPI (2010 -2015)? kwa ajiri ya maendeleo maana vijana huu ndio muda wetu. mfn nikitizama tokea 1980's up to now 2000's ambako nakumbua kulikiwa na viongozi mpaka leo wapo eg S. Sitta,Kingunge hata kabla sijazaliwa na wengine mtawataja.

  Je nia asilimia ngapi ya vijana nchi ni wapiga kura? nikiwa na maana hii kama UVCCM ndio wapiganaji wakuu katika kuimarisha watu kumchagua mtu fulani kuwaongoza wananchi wa eneo fulani husika inakuwaje wao washindwe kushauri vijana wenzio kuchaguo viongozi bora na wenye siasa safi na walipo kimaendeleo zaidi na wazalendo wakiwemo vijana wenyewe?.

  Nikiangalia kwa haraka tuuu nadhani ni asiliamia 0.5% au 1% ya viongozi vijana walioko katika nyadhifa mbalimbali ktk serikali au bungeni na uwaziri.

  Sasa leo UVCCM mkiwa kimya tutawatambuaje nanyi ndio wayataka hayo madaraka yajayo? kivipi tuwape kama hatuwaone mkiweka mikakati yenu hadharani? nakumbuka Nape alijaribu kunyanyuka na kuweka misimamo sikuona hata vijana wengine kujitokeza wengi wao wakanywea kimyaaa nkajua tu hawa ni bendela fuata upepo hakuna lolote. Hii ni kumaanisha UVCCM hamuna LUGHA MMOJA WAL SAUTI MMOJA hamko wote kwenye chungu kimoja.

  Napenda Quote falsafa aliyoisema Nahodha Vua “Yuko mwanafalsafa mmoja wa zamani, aliwahi kusema maneno haya: ‘Tutakapokufa msitutafute katika makaburi yetu yaliyotengenezwa vizuri kwa chokaa bali mtutafute katika nyoyo za watu tuliowasaidia’. Ninawashauri vijana wenzangu walioko katika UVCCM au serikali na vyama tuitumie sana busara ya mwana falsafa huyo,”


  Je UVCCM nyie mwajiandaa vipi? Japo wananchi waweze kusimulia vizazi vijavyoooo.

  NB: Nimewaza pia na kujiuliza ile speach ya Majuzi ya JK iliyo wafanya TUCT kusitisha mgomo je Hiyo iliandaliwa na nani mpaka JK akafika na kuisoma kwa Jaziba na masuto mengi kama yale? ni Kijana au mzee aliyo iandaa?

  Naomba tu niwakilishe ujumbe wanguu huuu kwa UVCCM na kama kuna wachangiaji tafudhali karibuni na kuchangia machache.
   
 2. m

  magee Senior Member

  #2
  May 12, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hakuna hata mmoja anayejali maslahi ya nchi........wote wanajali kuonekana,kupata umaarufu,kujitengenezea ajira siku zijazo,na kubwa wakumbukwe mbeleni......wengi njaa zao pia zinawaponza wanatumiwa mpaka viatu vinaisha soli kuwapigia debe wajanja.
  Na ndio maana hawana kauli mbiu wala sera,blabla tu zimejaa!!!
   
 3. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ume nena mkuu hapo sipangue neno wala kuliongezea neno.

   
Loading...