G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,595
- 36,015
Kwa mujibu wa waziri wa biashara, viwanda na uwekezaji ndugu Charles Mwijage ni kuwa, serikali tayari imeagiza sukari nje ya nchi ila bado imehifadhiwa.
Akielezea utaratibu wa kuigawa sukari hiyo kupitia "radio one nipashe" leo asubuhi tarehe 20 june kupitia mahojiano maalum, waziri Charles Mwijage amewaagiza wakuu wote wa mikoa nchini kushirikiana na wakuu wote wa wilaya wafanye sensa maalum ili kujua kiasi cha sukari inayohitajika kwenye maeneo yao kisha wawasiliane na katibu mkuu wizara ya kilimo ili wapelekewe sukari wanayohitaji.
Maswali ya kujiuliza
1) Ni kina nani watakaouza sukari hiyo?
2) Mgawo utaendelea kwa muda gani?
3) Kila mtu anahitaji kununua kiasi gani kwa wastani?
4) Ni njia zipi zitatumika kuzuia hujuma?
Kwa wale ambao hawajui, huu utaratibu ulikuwepo miaka ya 1980 ambapo watu walikuwa wanapanga foleni kwenye maduka ya ushirika kununua sukari na ilikuwa "ole wako ununue sukari nyingi, utaeleza ulikoitoa hela hiyo ya kununulia sukari hiyo"