Kwa UKAWA tu

Kwa UKAWA tu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Viongozi wa UKAWA tunawakumbusha mambo yafuatayo ambayo hamna budi kuyakumbuka tena na tena na tena hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu:

1. Watu wote wanaopenda njia mbadala ya kuongozwa tegemeo lao ni UKAWA

2. CCM iko vitani tangu mwaka 1954, ina silaha na mbinu zote za kupigana na kubaki madarakani

3. UKAWA ni mbinu mpya na ya kisasa hapa nchini ambayo haijawahi kuweko hapo kabla inayotishia utawala wa CCM

4. Umoja wenu wa UKAWA uko hatarini kuvunjia kila sekunde inayopita kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, kuweni makini kwa kila sekunde na kila tukio hata kama liwe dogo namna gani.

5. Adui wa UKAWA wenu anaweza kutumia mtu yeyote, chombo chochote na sababu yoyote andani na nje ya ukawa kusambaratisha ukawa. Kaa chonjo saa mbaya! kosa moja watakula mpaka kingi yenu

6. Chungeni ndimi zetu katika kuongea na vyombo vya habari, tafuteni msemaji mkuu wa UKAWA

7. Wekeni mbele kwanza maslahi ya Taifa kabla ya maslahi ya vyama vyenu, wagombea wenu na viongozi wa vyama vyenu

8. Tunzeni siri za UKAWA sehemu salama zisivuje na kuwafikia wapinzani

9. Kubalianeni mapema namna mtakavyoiongoza nchi kama mkipewa ridhaa na wananchi kutuongoza

10. Chagueni viongozi wanaokubalika kwa makundi yote ya wanaume, wanawake, vijana, wazee, wakristo, waislamu, wafadhili, wafanyabiashara, makabila yote, kanda zote, wafanyakazi na pande mbili za muungano.

11. Wekeni mgombea anayefanana kwa sifa angalau kwa 50% na mgombea wa CCM (umri, wajihi, jinsia, taaluma, elimu, uzoefu, uadilifu, n.k)

12. Himizeni vijana wengi wakajiandikishe na hatimaye wakapige kura, na mwisho

13. Tafakarini mapema kuhusu vyanzo vyooote vya mbinu chafu kwenye uchaguzi na namna mtakavyoweza kukabiliana navyo ili hatimaye kuwe na uchaguzi na matokeo huru na haki.
14. Jiandaeni kisaikolojia kwa matokeo ya aina yoyote
 
matumaini ya watanzania yapo ukawa. hakuna mabadiliko ya kweli kupitia ccm kweli..
 
matumaini ya watanzania yapo ukawa. hakuna mabadiliko ya kweli kupitia ccm kweli..
UKAWA ndiyo nini? Hawa viongozi wa vyama vya siasa wanaosaka madaraka? Hivi muungano wa juu juu kweli ndiyo uwe mabadiliko?
 
UKAWA ndiyo nini? Hawa viongozi wa vyama vya siasa wanaosaka madaraka? Hivi muungano wa juu juu kweli ndiyo uwe mabadiliko?

Kudharau ukawa ni sawa na kuwadharau wale watanzania wote ambao wanaowaunga mkono UKAWA ambao ni wengi pia, kufanya hivyo sio busara hata kidogo, CCM kina wafuasi na UKAWA wanao pia na wote ni watanzania halisi na ni ndugu. Dunia ina macho inatuangalia iko siku itawakataa watu wenye mtizamo hasi kama huu wako. Walikuwepo akina Gaddafi, Sadam, Mubarak, Mobutu, n.k waliokuwa wanawaza kama wewe.
 
UKAWA ndiyo nini? Hawa viongozi wa vyama vya siasa wanaosaka madaraka? Hivi muungano wa juu juu kweli ndiyo uwe mabadiliko?

mkuu ukawa ni umoja wa katiba ya wananchi. kuhusu madaraka, kwani wale wagombea urais 36 wa ccm hawasaki madaraka?
 
Viongozi wa UKAWA tunawakumbusha mambo yafuatayo ambayo hamna budi kuyakumbuka tena na tena na tena hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu:

1. Watu wote wanaopenda njia mbadala ya kuongozwa tegemeo lao ni UKAWA

Hicho ndo kinaitwa kiherehere, waliounda UKAWA wako kimya wanajua muda watakapo tangaza kukubaliana kutokubalina, eti nyie mnajifanya kuwashauri. Dalili za mvua ni mawingu, nyie mlioweka tegemeo lenu ukawa mtageuka wakiwa.
 
Thread ni kwa wana UKAWA tu na wewe ni Mwana UKAWA ukisikia akili ndogo ndio hii, Unakurupuka tu hata kusoma kichwa cha habari kinasemaje. Bongo Vilaza wengi
 
mimi kura yangu ukawa,ya mke wangu ukawa,ya mtoto wangu ukawa
 
Hicho ndo kinaitwa kiherehere, waliounda UKAWA wako kimya wanajua muda watakapo tangaza kukubaliana kutokubalina, eti nyie mnajifanya kuwashauri. Dalili za mvua ni mawingu, nyie mlioweka tegemeo lenu ukawa mtageuka wakiwa.

Kisu kimekata mfupa, najua huu uzi umekuuma sana lakini habari ndo hiyo, wawe makini safari hii CCM ni vipandevipande mwaka huu
 
Hicho ndo kinaitwa kiherehere, waliounda UKAWA wako kimya wanajua muda watakapo tangaza kukubaliana kutokubalina, eti nyie mnajifanya kuwashauri. Dalili za mvua ni mawingu, nyie mlioweka tegemeo lenu ukawa mtageuka wakiwa.

Kweli mkuu waliounda UKAWA wapo kimya wala hujakosea ndo maana hata kwenye kuongezeana posho wamekaa kimya hili ni janga!RIP
 
UKAWA mbele kwa mbele mpaka kieleweke.......tumechoka na chama cha majambazi
 
Back
Top Bottom