Kwa hali ya siasa ilivyo hapa nchini ni mawazo yangu binafsi kuwa ni lazima kati ya haya yatokee katika uchaguzi Mkuu ujao:
1. Mkuu wa nchi ajaye atatokea upande wa UKAWA. Na hii inawezekana kama elimu kwa wananchi kuhusu maslahi na haki zao itakuwa imeeleweka. Kwa watu ambao hawafungamani na itikadi za chama chochote, basi tunasema uwezekano wa kufanikiwa hapa ni asilimia 50-65%.
Kwa nini isiwe asilimia 100%?
Jibu ni kuwa je wapiga kura wangapi kutoka kundi la vijana watajiandikisha na kweli kuhakikisha wanapiga kura zao pamoja na kuzilinda. Ni wangapi wameipata hiyo elimu kama ilivyokuwa inafundishwa na vyama vya upinzani. Hapa bado haileweki. Ndiyo maana nasema ukiongezea na sababu zingine zitakazo tokana na mbinu za chama tawala ni vigumu kusema kwa asilimia 100 kuwa Mkuu wa nchi ajaye atatokea UKAWA.
2. Idadi ya wabunge wa UKAWA katika uchaguzi Mkuu ujao. Hapa mimi nikiwa kati ya wale wapenda mabadiriko ya nchi yetu kwa manufaa ya wengi, na hasa bila kuangalia itikadi za vyama basi ninaona hapa kuna nafasi kubwa ya kutimiza malengo kwa asilimia zaidi ya 80%-90%.
Ni ukweli usiopingika kuwa kama UKAWA wasipopata idadi zaidi ya wabunge basi lawama iende moja kwa moja kwa UKAWA. Hapa nikiwa na maana kuwa nafasi ya kufanya vizuri ipo na inabidi IWEPO. Hapa ndipo pa kukusanya nguvu hata ile ambayo iko kibindoni. Ni lazima wabunge wapatikane na UWEZO wanao na muda bado upo wa kurekebisha mbinu kutokana na upepo unavyo vuma.
Hapa ni mahali pa kuonyesha umoja na mshikamano wa hali ya juu.
Hapa tulio wengi tutashuhudia wapiganaji wa kweli na wale wa mpito. Ninasema UKAWA hatutakuelewa kama idadi ya viti ya wabunge haitaomgezeka katika uchaguzi Mkuu ujao. Na hakuna sababu ya kutopata idadi kubwa! Kazeni mwendo kwani upepo bado ni MWANANA KWA wapenda mabadiriko kwa faida ya wengi.