Kwa timua timua hii wenye mikopo bank inakula kwa nani?

mziguamnguu

Member
Nov 16, 2015
52
18
Waungwana naomba msaada wa kupata ufafanuzi kwa hii timua timua ya JPM kwa watumishi wenye mikopo kwenye mabank na taasisi nyingine za kifedha deni atakalobaki nalo mtumishi mfukuzwa kazi linakula kwa nani hasa kwa wale wanaolipa mikopo kupitia mishahara!?
 
Daaah nashukuru kwa michango wadau maana kwangu naona ni figisufigisu tuu, kwa muono wangu nahisi upotevu wa pesa utakuwa mkubwa mno.
 
Waungwana naomba msaada wa kupata ufafanuzi kwa hii timua timua ya JPM kwa watumishi wenye mikopo kwenye mabank na taasisi nyingine za kifedha deni atakalobaki nalo mtumishi mfukuzwa kazi linakula kwa nani hasa kwa wale wanaolipa mikopo kupitia mishahara!?
Marazote deni ambalo muajiri analokudhamini ni lile ambalo litalipika kirahisi kwa kiwango cha mshahara wako, na hata mabenki wanazingatia hayo.
Benki haiwezi kukukopesha kiasi kikubwa cha pesa kwa dhamana ya ajira, ni lazima uweke dhamana ya mali isiyo hamishika ndugu.
Kwa maana hiyo waliodhaminiwa na waajiri, muajiri atalazimika kulipa lakini izingatiwe kuwa madeni yenyewe hasara yake hayata igharimu sana serikali kuliko sababu iliyomtimulisha kazi, nikimaanisha ufisadi au uwajibikaji
 
Mikopo yote kwa sasa ina bima. Kwahiyo bima inalipa yanapotokea hayo kama kufukuzwa kazi na vifo. Hata hivyo mabenki yanapata faida kubwa sana kwa kutoza riba kubwa.
 
Asante kwa ufafanuzi wako mwanaJF nimekuelewa ingawa kahasara kanaingia kiaina kwakuwa yawezekana mtumishi alifukuzwa kwa kukurupuka, mwajiri analipa salio ambalo kwa wakati huo mlipaji(aliyefukuzwa)hazalishi chochote.
 
Mikopo yote kwa sasa ina bima. Kwahiyo bima inalipa yanapotokea hayo kama kufukuzwa kazi na vifo. Hata hivyo mabenki yanapata faida kubwa sana kwa kutoza riba kubwa.
Mikopo ya siku hizi ina bima kwa hiyo kimsingi ni lazima ilipwe tofauti na kipindi cha nyumba ambapo kama ulikuwa mwajiri wa uma basis mwajiri wako ilimpasa kuwajibika moja kwa moja.
 
Dah!! Kwahiyo kama jipu limekomaa unataka llisikamuliwe kwa sababu lina mkopo??.
 
Jipu kukamuliwa lazima lakini ni vyema kujua kama ni jipu au uvimbe tu, niliomba ufafanuzi wakujua deni litakalobakia litalipwaje!!?
 
Back
Top Bottom