Kwa TAKUKURU mkoa wa Dodoma

Kufa c mwiko

JF-Expert Member
May 26, 2013
744
312
kwa niaba ya wananchi wa mtera niombe kuwakumbusha kufika na kushughurikia malalamiko yetu dhidi ya viongozi wa kijiji ya matumizi ya zaidi ya shilingi mil 25 na kukausha kabisa akaunti ya kijiji siku ya ijijumaa tarehe 8-4-2016 tuliwatuma wawakilishi wetu wawili hapo ofisi ya mkoa wakatuletea majibu kwamba mtawapa taarifa takukuru mpwapwa waje kuchunguza lakini mpaka leo kimya matokeo yake wale viongozi tunaowatuhumu wanaandaa mkakati wa kuwafungulia kesi ya kubambikiza wale wote waliohoji matumizi ya hiyo fedha mil25 na walishafanya hivyo siku za nyuma na kufanikiwa kuwafunga tunaomba mfike hata nyie ofisi ya mkoa kutatua tatizo letu.
 
  • Thanks
Reactions: Mss
kwa maoni yangu takukuru mfike mtera na kuitisha mkutano mkuu wa kijiji kisha serikali ya kijiji isome mapato na matumizi ya hizo milioni 25 zilivyotumika na kubaki laki moja tu ndio mtajua kuwa kuna watu hawatambui kama nchi hii inaongozwa na katiba isitoshe muhujumu mkuu na mkongwe ni mtendaji wa kata kwa sasa huyu jamaa kesha hamishwa na kurudishwa kijiji hiki sasa ni mala ya tatu akiiba anahamishwa anakaa miaka michache anarudisha alianza hujuma hapa kijijini mwanzoni mwa mwaka 2000 mkuu wa wilaya miaka hiyo akaamulu aondolewe akarudi baadae baada ya mkuu huyo wa wilaya kuhama akaiba tena mil 1.5 za mradi wa maji akafikishwa kituo cha polisi mpwapwa ilikuwa2009 kama sijakosea tukasikia ameamrishwa kurudisha zile fedha kisha kahamishwa miaka ya hv karibuni karudishwa tena ndio hiyo milioni ishirini na tano imepukutishwa binafsi naamini kuna mtu anamlinda wilayani kwani kuna eneo la kijiji kaliuza kwa mfanyabiashara mmoja wa mafuta mpwampwa bila woga kachangisha michango ya baabara hajawai kusoma mapato na matumizi hata siku moja aliposikia tangazo kuwa rais kasitisha michango kashukuru hata mafundi walioanza ujenzi wa maabara hajawalipa tafadhari takukuru mchunguzeni mtendaji kata huyu ni zaidi ya jipu.
 
niwashukuru sana takukuru dodoma kwa kuanza kulifanyia kazi swala hili hongereni sana kwani mmewapa imani kubwa sana wananchi na serikali hii ya awamu ya tano ya hapa kazi tu tunawaahidi ushirikiano popote mtakapotuhitaji kwani hujuma za viongozi wa kijiji wananchi wote tunazifahamu kazi njema.
 
Nimecheka sana kuna mtu mmoja wa karibu na hao watuhumiwa(baadhi ya viongozi) eti wanapita kwa wafanya biashara wakubwa kukopa fedha ili wakahonge takukuru kweli siku ya kufa nyani wanajua ndio zama zile ngoja tuone mwisho wao
 
Back
Top Bottom