Kwa tabia ya wabunge wa CCM mwaka 2020 upinzani utaongoza bunge

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Kwa tabia za wabunge wa CCM upinzani utaongoza bunge mwaka 2020 bunge lililopita lilikuwa na mambo kama haya lakini tulijipa moyo kuwa angalau mwaka huu kuna wabunge vijana mambo yatabadilika kidogo.

Tulifikiri hoja nyingi za kitaifa zitapewa nafasi kwa kuwa wabunge wengingi ni wapya na vijana lakini lahasha ni heri wale wabunge wa zamani wa CCM walikuwa angalau kwa mbali wanajali zaidi mambo ya kitaifa kuliko ya chama chao.

UKAWA komaeni ni heri msurudi bungeni kuliko kula haramu.
 
Yaani ukishaingia ccm huwa sijui kwa nn akili inahamia makalioni sasa na na huyu Dr tulia nikajua hata ana akili kumbe Yale yale
CCM ni ile ile na mambo yake ni yale yale! Ukishaingia unaweka akili store ipumzike; uwe ni professor, engineer, you name it; it does not matter. come 2020 wakipewa 230M plus wanarudi kwa wananchi na tulivyo wasahaulifu tunawapigia kura kwa kufikiri wamebadilika kumbe wametuduwaza kwa "vijisent" vyao na kutufanya tusiambilike. Wananchi wacha waone wenyewe na kisha wafanye maamuzi.
 
Kwa tabia za wabunge wa CCM upinzani utaongoza bunge mwaka 2020 bunge lililopita lilikuwa na mambo kama haya lakini tulijipa moyo kuwa angalau mwaka huu kuna wabunge vijana mambo yatabadilika kidogo.

Tulifikiri hoja nyingi za kitaifa zitapewa nafasi kwa kuwa wabunge wengingi ni wapya na vijana lakini lahasha ni heri wale wabunge wa zamani wa CCM walikuwa angalau kwa mbali wanajali zaidi mambo ya kitaifa kuliko ya chama chao.

UKAWA komaeni ni heri msurudi bungeni kuliko kula haramu.
CCM haihitaji kura ya mdanganyika yeyote kushinda.Haya mambo yataendelea hadi hapo wazalendo wa kweli wa nchi hii watakapozaliwa
 
lendila umekua msahaulifu sana, umeshasahau maroli yaliyokamatwa na kura feki na tume wakasema haziwahusu.

umeshasahau ya jecha salum jecha
mm kwa maoni yangu nafikiri ni kwa sababu ccm haitegemei karatasi za kura ingekuwa inategemea karatasi za kura wasingefanya mambo ya kijinga kama haya
 
Wabunge vijana wa CCM wengi ni wale waliopata chance kuingia mjengoni kwa kuwa vibaraka.

Hawana uwezo wa kusimamia haki wala ukweli, hulka hii hawana. Usitegemee kusimama na kuchangia hoja za kitaifa kwa manufaa ya nchi bali wako kikada zaidi.

2020 tunawapiga
 
Wapo wazee kama Warioba,Makecela,Salim,Msuya, Mwandosya, Bomani, Ndejebi Nk ambao wangetegemewa kusimama hadharani na kukikemea chama walichokijenga kwa nguvu zao na kinakwenda hovyo lakini wao wako kimya kulinda pension zao.
Wazee hawa wataoeleka mvi zao kaburini kwa aibu kubwa sana, kwao na vizazi vyao. Tunamwomba Mungu awape uhai hadi mabadiliko yatokee wakiona kwa macho yao
 
Back
Top Bottom