Kwa tabia hizi za viongozi wetu EAC haitaweza kuwa jumuiya imara,mizozo na migogoro haiishi

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,373
34,587
Maraisi wa wa hizi nchi zinzounda umoja wa Afrika Mashariki hawaishi kuzozana,kugombana na kutupiana maneno tangu zama za akina Mwalimu Nyerere,Iddi Amini,Kenyataa,Daniel Arap Moi na Museveni.

Kwa sasa kumekua na mizozo tangu kipindi cha akina Benjamini Mkapa na Pierre Buyoya, Jakaya Kikwete na Paul Kagame,Yoweri Museven na Paul Kagame,Yoweri Museven na Moi,Mwai Kibaki,Uhuru Kenyatta,Paul Kagame na Pierre Nkurunzinza,basi mambo ni shaghala bagala,sasa najiuliza ni ipi hatma ya EAC?,na je tutaweza kusimama na kuwa jumuia imara kama jumuia ya EU? au ECOWAS?

Viongozi wenyewe hawaelewani kutwa kucha ni kutumiana maneno ya vitisho tu.wanaelekea wapi? watafikia malengo waliyojiwekea ,kibiashara na uchumi?

Wanafikia hata hatua ya Ugomvi wa viongozi wanauhamishia kwa wananchi ,wanawekeana hadi vizingiti kwenye biashara na uchumi,wanafanyiana Umafia,kila siku mizozo ya viongozi.

Ni mwendo wa kuvizian hadi hata kutaka kuhujumiana kisiasa,narudia tena kuhujumiana kisiasa,
Watatufikisha kweli?

Hii Jumuiya itaendelea kweli?au ni jumuiya ya kwenye makaratasi tu?
 
Back
Top Bottom