scientificall
JF-Expert Member
- Jun 4, 2015
- 457
- 328
Elimu bure ndio gumzo kila kona ya Tanzania lakini Kwa uchunguzi yakinifu ulofanywa matunda yatakayotokana na elimu bure ni dhahiri kua Tanzania tunaelekea kuzalisha wasomi feki wenye vyeti lakini kichwani hamna kitu, kama leo hii mwalimu mmoja anafundisha wanafunzi 500 Kwa wakati mmoja, leo hii mwanafunzi darasa la sita anaenda shule saa 6 mchana kutokana na ufinyu wa madarasa, fikiria mtoto wa darasa la 1 na 2 ataenda saa ngapi shule. Hii ndio elimu bure.