Kwa speed hii CHADEMA tutashindwa kufika

SACO

JF-Expert Member
Jul 25, 2011
1,139
2,000
CHADEMA NA DEMOKRASIA

Leo kulikucha vibaya sana. Siku nzima ilikuwa imetandizwa na wingu jeusi kwa wapneda siasa za Mitandaoni.

Hali ya hewa imechafuka kutokana mwenendo wa kikao cha uchaguzi wa ndani na mtokeo ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa.

Nikiwa kama mwanachama na Mwananchi wa kanda ya Nyasa nilijikuta ninabamizwa na upepo Mkali unaovuma kufuatia matokeo hayo.

Sehemu kubwa ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa akiwemo kaka yangu Moses Klaut Kyando wanaona kilichofanyika Mbeya hakikuwa sahihi kwa Chama kinachojipambanua kuwa ni chama cha kidemokrasia.

Wanasema Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa aliwashawishi au kuwalazimisha wajumbe wa mkutano wa kanda waliokusanyika kufanya uchaguzi wa M/kiti CHADEMA kanda ya Nyasa, Kumchagua Kamanda Peter Msigwa kuwa mwenyekiti wa Kanda.

Malalamiko ya Makamanda wengi yamejengwa kwenye msingi wa kuwa pamoja na sababu zozote ziwazo zile hawajapendezwa na namna zoezi zima lilivyofanyika. Wadau wanasema imekaa vibaya sana pale ambapo wagombea wengine wanne akiwemo Makamu mwenyekiti wa Taifa BAVICHA bwana Patric Ole Sosopi kuenguliwa jina lake kwa ule mtindo maarufu wa CCM wa KUKATWA.

Wajumbe wanaomuunga Mkono Sosopi na wale ambao wanapenda kuona ukuaji wa demokrasia ndani ya CHADEMA wanaamini kabisa kuwa Bw. Sosopi ndio alikuwa chaguo sahihi la kuwa Mwenyekiti wa Chama kwangazi ya kanda.

Mimi Nina mtizamo Tofauti, na ninatofautiana na wote wanaosema aidha Msigwa anafaa na wale wanaosema Sosopi pia alifaa.

Kwanza ninapata shida sana ninapoona kiongozi wa nafasi ya kuchaguliwa na wananchi kama Mbunge anapogombea tena nafasi za uongozi ndani ya Chama.

Katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 nilikuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimboni Makete kupitia CHADEMA. Nilichokiona ni kuwa kutokana na viongozi wengi wa Chama kuwa wagombea wa nafasi za Ubunge chama kilijikuta hakina kiongozi wa kukiendesha wakati wa uchaguzi. Karibu viongozi wengi ambao tulikuwa tunawategemea kwa mawazo, ushauri na hata kwa maamuzi walikuwa bize majimboni kwao kwa kampeini za kugombea Ubunge.

Kwa kuchaguliwa Peter Msigwa Mbunge kuwa mwenyekiti wa Kanda ninaona Chama changu CHADEMA hakijaliona tatizo hili. Tutakapofika kwenye uchaguzi Mkuu mwaka 2020 Tutahitaji sana Busara za mwenyekiti kanda kwenye kusimamia kanda, Matokeo yake Msigwa hatakuwepo maana atakuwa Busy na kampeini za kuomba kuchaguliwa Kuwa Mbunge wa jimbo la iringa Mjini.

Mwenykiti wa Kanda ni mtu Muhimu sana kuwa na nafasi wakati wa uchaguzi Mkuu. Experience niliyopata wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ni kuwa hakuna jimbo ambalo baada ya kura za maoni hali ilikuwa Shwari. Majimbo karibu yote ya Mkoa wa Mbeya na Njombe wanaCHADEMA waliingia kwenye uchaguzi wakiwa wamegawika vipande vipande.

Team za wagombea walioshindwa kwenye Kura za maoni waliendelea na harakati za kuhujumu mwenendo mzima wa kampeini, watia nia walioshindwa kwenye kura za maoni walifanya kampeini za kuhakikisha yule aliyeshinda kura za maoni anashindwa kwenye uchaguzi mkuu. Majimbo yote ya Lupembe, Njombe Mji, Mbeya, Mbeya Vijijini, makete nk yalifanana kwenye suala hili la Migogoro.

Sasa unapokuwa tena na Mwenyekiti ambaye ni Mbunge na ana nia ya kuwania ubunge tena unategemea nini? Kama CHADEMA tupo serious kwa uchaguzi wa 2020 basi tuna haja ya kubadilisha gia majini, wabunge wasishike nafasi za juu za chama, sana sana wawe wajumbe wa vikao kama kamati kuu n.k.

Kitu kingine nilichokiona kutokana na uchaguzi wa mwaka 2015 ni Viongozi wengi wa chama wa ngazi za mikoa na kanda walienda kugombea ubunge kwenye Majimbo. Wengi mtakumbuka mzozo wa Jimbo la Njombe Mjini, Mgombea na viongozi wake wa chama hakukuwa na kuelewana kutokana na ukweli kuwa viongozi wa Chama wa ngazi ya Mkoa na wilaya walikuwa watia nia ya nafasi ya Ubunge kwa maana hiyo aliposhinda mwanachama mwingine uwiiii, hawa jamaa walikataa kata kata kumpa support mwenzao ashinde.

Nenda mikoa yote utaona hali hii ilikuwa hivi hivi, viongozi wa mikoa na wilaya walisababisha migogoro isiyo ya lazima kwasababu ya kutaka wateuliwe kuwa wagombea ubunge, shida ilikuja pale wanachama walipowakataa, na wao walilipiza kisasi kwa kutowaunga Mkono wagombea waliopitishwa na wanachama.

Twende kwenye nafasi ya uongozi wa kanda. Kanda ya Nyasa ndio ilitia fora ambapo Mratibu wa kanda kamanda Frank aliingia kwenye Mgogolo mkubwa na mgombea wa Ubunge wa Mbeya Vijijini kutokana na Mratibu wa kanda kuwania nafasi ya Ubunge na yeye kuenguliwa kwenye kura za maoni.

Kila mtu anajua kuwa majimbo ya Mbeya vijijini, majimbo ya Lupembe, Njombe Mjini, hayakuwa ya kuyapoteza, kama wanachama, Viongozi tungekuwa na mshikamano na wagombea wetu tulikuwa tunashinda tena kwa ushindi mkubwa sana.

Embu fikiria ikija kutokea katika uchaguzi wa mwaka 2020 Sosopi akatia nia ya kugombea ubunge Iringa Mjini (kwao Iringa Ismani kwa Lukuvi) alafu wanachama wakampitisha kwenye kura za maoni akimuangusha Peter Msigwa, Unadhani kamanda Msigwa atampa Support Sosopi kushinda Jimbo la iringa?

Kutokana na sababu hizo sioni kama ilikuwa sahihi kumchagua Kaka yangu kamanda Msigwa kuwa mwenyekiti wa Chama ngazi ya kanda.

Tukirudi kwa kaka kamanda Sosopi, yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (BAVICHA). Nafasi aliyonayo Kamanda SOSOPI kitaifa ni kubwa mno, nafasi yake inampa wajibu mkubwa sana kwa jamii, kwa chama na nchi kwa ujumla.

BAVICHA ndio wanahusika na usalama wa wanachama, viongozi na mali za Chama. kazi hiyo peke yake ni kubwa ambayo kama ningepewa mimi hata nisingefikiria kuomba uenyekiti wa mtaa tena kuongeza kwenye huo wajibu.

BAVICHA ndio wanaoandaa mikutano, sasa hivi kumepoa hakuna mikutano iwe ya ndani au ya nje kwasababu BAVICHA hawajafanya kazi yao sawa sawa. kama BAVICHA wakasema tunataka Mkutano sehemu fulani na kama watadhamiria kweli hakuna kiongozi ndani ya CHAMA atakayekataa mkutano huo.

Mikutano inahitaji maandalizi, kutafuta kumbi, kuchomeka Bendera, kuhamasisha watu wafike kwenye Mikutano nk. Wajibu huu peke yake ni Mkubwa mno, ukiwa kiongozi wa hii branch ya vijana huwezi kuanza kudream kugombea uenyekiti wa kanda.

Nimesoma historia ya aliyekuwa kiongozi wa Youth League huko South africa, Chris Hani aliyeuwawa na makaburu 10 April 1993. Huyu amekuwa kiongozi wa Youth League ya SA wakati wa Struggle kwa muda mrefu, baadaye ndio alikuja kuwa founder na kiongozi wa Armed Struggle "Umkhonto we Sizwe". Chris Hani alikuwa mwiba kwa utawala wa makaburu wa Africa Kusini lakini hakuwahi hata siku Moja kufikiria kung'ang'aniana vyeo ndani ya chama na wanachama wengine. Soma pia habari za Steve Biko.

Vijana tunapenda tutambuliwe kama wana Mapinduzi, lakini matendo yetu yanaishia kwenye matamko tu yanayotujengea umaarufu alafu baadaye our true Color reveals tunaingia kugombea madaraka.

Nilitegemea SOSOPI atakaa chini na viongozi wenzake wa BAVICHA kutengeneza mikakati kabambe ambayo itatusaidia kutuvusha 2020 tukiwa washindi.

BAVICHA wanapaswa kuja na mikakati ya wazi na ya siri ambayo inafanya Chama Chetu kizidi kushine na kukubalika mbele ya wananchi. Unapokuwa Kiongozi wa branch Kubwa na yenye nguvu ya Vijana kama BAVICHA alafu huoni majukumu yako unafikria kuomba nafasi zingine kama za kuwa kiongozi wa kanda, wewe unatia shaka kama kweli ni kiongozi sahihi wa nafasi ya makamu Mwenyekiti.

CHADEMA kazi ya kuwa Think tanks, Tumeiachia kamati kuu na Mwenyekiti Taifa ili kufikiri kwa niaba yetu. Ni kweli katiba inataka Mwenyekiti na kamati Kuu kuongoza chama, kuonyesha dira ya tuendako. LAKINI wanapaswa waonyeshe dira baada ya kuwa well informed kwenye hilo suala ambalo wanapaswa kutuonyesha dira.

Nilitegemea akina Sosopi na akina Msigwa wangekaa chini wangetafuta vijana wataalam kadhaa ambao wanakuwa na kazi ya kukusanya Data, na kufanya analysis kwenye mambo mbali mbali yanayotukabili kama taifa. Hiyo team ya researchers inakuwa ndio THINK TANK yetu kama chama.

THINK TANK wanapaswa kuwa na information sahihi na current kwa mfano za hali ya ajira, wao ndio waiambie kamati kuu na Mwenyekiti wetu kuwa hali ya Ajira nchini ipo katika kiwango hiki, na washauri way forward kwa chama, ndipo chama kitatoka na sera inayoaddress issue ya ajira kutokana na matokeo ya utafiti wa hiyo team ambao ni Think Tank wetu.

THINK TANK wetu hao wanapaswa kufanya tafiti za hali ya Afya, hali ya Elimu, mwenendo wa uchumi na kila wakati Chama kiwe kinapata current Information na kutokana na hali hiyo Chama kinaweza kutoka na majawabu. Nilidhani Sosopi kama M/M/kiti BAVICHA Taifa na Peter Msigwa kama Mbunge na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wangekuwa wanafikiria kusaidia kukiwezesha chama kufika huko na sio wao kurudi kugombea vyeo vyote.

Maoni yangu kuwa Kanda ya Nyasa imetufungua macho sasa Tunahitaji Kujisahihisha ili Chama Chetu cha CHADEMA kifike kikiwa Imara 2020 na hatimaye tukaibuke na Ushindi. CHADEMA ni tumaini la wananchi kushindwa kwa CHADEMA ni Kushindwa kwa wananchi wote wa Tanzania.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki CHADEMA.
 
sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,825
2,000
Bila shaka vigezo na masharti vilizingatiwa........vingozi CDM jitokezeni muweke hali ya hewa sawa.
 
Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,389
2,000
Mliwafukuza wenzenu kwa ubaguzi wenu sasa ni zamu yenu kufitiniana, hila hazitakuja kuwasaidia hata siku moja
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,549

Shida kubwa iliyopo ni kwamba Mbowe na Tundu lusu wanawadharau sana ninyi Wanachadema na ndiyo maana wanafanya wanavyotaka kwani wanajua kesho wakija kuwapa kuwaambia blah blah mtawaamini na kuanza kuwadekia barabara tena huku wao wakitafuna ruzuku, hawa watu wamekaa Ulaya zaidi ya wiki mbili nani amelipia hiyo gharama?
 
stigajemwa

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
449
500
Naunga mkono hoja,kwani chama kwa sasa kina wanachama wengi tena makini na wenye uchungu wa kweli wa mabadiliko hivyo ni vyema wangeachiwa nao waje walete mawazo mapya.Kwani akina msigwa na Sosopi kama wana jipya walioneshe kwenye platfom waliyonayo sasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom