Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Rais Magufuli amedumu madarakani kwa zaidi ya siku 100. Mambo aliyofanya nadiriki kusema kuwa ni makubwa na yamewashangaza wengi. Wengi wamebaki midomo wazi na kwa hakika Watanzania wanazidi kumpenda na kumkubali Rais wetu.
Upande wa pili wa shilingi, hali ya upinzani inazidi kuwa dhoofu. Pengine kinachowapa nguvu kidogo kwa sasa ni hali ya kisiasa Zanzibar. Nina hakika baada ya Machi 20, wapinzani watapotea kabisa kwenye siasa za dhahiri ( Active Politics).
Mahala pekee ambapo angalau unaweza kunusa harufu ya upinzani ni Bungeni. Labda kwa vile wengi wao wanapenda sana kuuza sura kwenye Runinga. Hata hivyo, ukichunguza kwa makini, hoja nyingi zinazotolewa na wabunge wa upinzani ni za kutaka tu kuuza sura na si kunusuru upinzani.
Fikiria mbunge anasimama eti kung'ang'ania bunge lioneshwe Live! Ona Eti mbunge anasimama na kusema Mwakyembe ametumia zaidi ya bilioni 260 kununua mabehewa feki. Alipotakiwa kutoa ushahidi ameshindwa mwisho wa siku kaambulia aibu ya kutohudhuria vikao viwili
Kwa sasa wapinzani wapo likizo. Tuonane tena mwezi Aprili wakati Bunge la Bajeti litakapoanza vikao vyake.
Jumamosi njema