Kwa Sasa, Mwenge una Madhara kwa Jamii Kuliko Faida.Ufutwe.

Toosweet

JF-Expert Member
May 27, 2012
2,141
1,982
Kwenu,

Twakukaribisha Mwenge,
Mgeni wetu uringe,
Na wenyeji tukutuze
Huku tukishangilia

Nuru yako yaangaza,
Kuwa umeleta haki
Tena umetoa giza,
Hapa kwetu Tanzania...

Sina hakika kama nimekariri neno kwa neno kama ilivyo lakini najaribu kukumbumbuka malengo na faida za Mwenge wakati ule nikiwa Shule ya Msingi Mzumbe, Morogoro. Tulihimizwa kukariri nyimbo na ngonjera za kuutukuza Mwenge. Tuliaminishwa kuwa Mwenge utamulika mabepari na wasaliti(watu waliopinga 'fikra sahihi za Mwenyekiti' na itikadi ya chama).

Wakati ule ilionekana ni uasi kuacha kuchangia mbio za Mwenge na kukesha sehemu ambazo Mwenge ulilala.
Kwa sasa tunaambiwa kuwa Mwenge unafanya kazi kubwa ya kuhimiza na kuzindua miradi ya maendeleo. Tena unajenga uzalendo.

Kumekuwa na rai nyingi na malalamiko kupinga tabia ya watu kukesha , kulewa na kufanya 'uhuni' mwingi usiku wa mkesha wa Mwenge. Wanaopinga Mwenge wameambiwa kuwa hawana uzalendo.

Siku ya tarehe 28 Septemba, 2018,katika mkesha wa mwenge wilayani Siha mkoa wa Kilimanjaro kulitokea mambo ya hovyo. Wanafunzi wa sekondari za Boma na Siha wapatao 17 wali**kwa na kula**tiwa. Taarifa zisingejulikana kama mmoja wa wasichana waliokuwa wahanga asingesema. Wahusika wametajwa kuwa madereva wa boda boda na bajaji. Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Kangi Lugola ameagiza uchinguzi ufanyike na sheria kuchukua mkondo wake.
Pengine hili ni tukio lililosikika zaidi kwa kuwa lilifika mpaka kwa Waziri mwenye dhamana na Usalama wa Raia. Vipi matukio mengi ya nyuma?

Kuna wakati mkimbiza Mwenge anatoa matamko kwenye uzinduzi wa miradi, kana kwamba yeye Ana cheo kikubwa na mtaalamu katika nyanja husika inayohusu mradi.
Hivi bila Mwenge miradi ya maendeleo itakwama? Fedha za miradi zitakosekana?

Kwa sasa Mwenge hauna maana wala faida kwa Watanzania.
Labda tukiambiwa ni maalumu kwa kuwa ni tambiko au hirizi ya Taifa.

TS.
 
NASIKIA JUZI KATI WATOTO WAMELAWITIWA KWENYE MKESHA WA MWENGE
ZINAA,ULEVI PAMOJA NA UASHERATI NI SEHEMU YA MIKESHA YA MWENGE
AFU HIKI PIA NI CHANZO CHA KODI ZETU KUPOTEA BURE,KUNA HAJA YA KUUFUTA HUU MOTO
 
NASIKIA JUZI GANI WATOTO WAMELAWITIWA KWENYE MKESHA WA MWENGE
AFU HIKI PIA NI CHANZO CHA KODI ZETU KUPOTEA BURE,KUNA HAJA YA KUUFUTA HUU MOTO
si kulawitiwa tu , bali pia wameambukizwa Ukimwi , ikumbukwe kwamba wakimbiza mwenge wengi na wahudhuria mikesha karibu wote wameungua .
 
Kwenu,

Twakukaribisha Mwenge,
Mgeni wetu uringe,
Na wenyeji tukutuze
Huku tukishangilia

Nuru yako yaangaza,
Kuwa umeleta haki
Tena umetoa giza,
Hapa kwetu Tanzania...

Sina hakika kama nimekariri neno kwa neno kama ilivyo lakini najaribu kukumbumbuka malengo na faida za Mwenge wakati ule nikiwa Shule ya Msingi Mzumbe, Morogoro. Tulihimizwa kukariri nyimbo na ngonjera za kuutukuza Mwenge. Tuliaminishwa kuwa Mwenge utamulika mabepari na wasaliti(watu waliopinga 'fikra sahihi za Mwenyekiti' na itikadi ya chama).

Wakati ule ilionekana ni uasi kuacha kuchangia mbio za Mwenge na kukesha sehemu ambazo Mwenge ulilala.
Kwa sasa tunaambiwa kuwa Mwenge unafanya kazi kubwa ya kuhimiza na kuzindua miradi ya maendeleo. Tena unajenga uzalendo.

Kumekuwa na rai nyingi na malalamiko kupinga tabia ya watu kukesha , kulewa na kufanya 'uhuni' mwingi usiku wa mkesha wa Mwenge. Wanaopinga Mwenge wameambiwa kuwa hawana uzalendo.

Siku ya tarehe 28 Septemba, 2018,katika mkesha wa mwenge wilayani Siha mkoa wa Kilimanjaro kulitokea mambo ya hovyo. Wanafunzi wa sekondari za Boma na Siha wapatao 17 wali**kwa na kula**tiwa. Taarifa zisingejulikana kama mmoja wa wasichana waliokuwa wahanga asingesema. Wahusika wametajwa kuwa madereva wa boda boda na bajaji. Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Kangi Lugola ameagiza uchinguzi ufanyike na sheria kuchukua mkondo wake.
Pengine hili ni tukio lililosikika zaidi kwa kuwa lilifika mpaka kwa Waziri mwenye dhamana na Usalama wa Raia. Vipi matukio mengi ya nyuma?

Kuna wakati mkimbiza Mwenge anatoa matamko kwenye uzinduzi wa miradi, kana kwamba yeye Ana cheo kikubwa na mtaalamu katika nyanja husika inayohusu mradi.
Hivi bila Mwenge miradi ya maendeleo itakwama? Fedha za miradi zitakosekana?

Kwa sasa Mwenge hauna maana wala faida kwa Watanzania.
Labda tukiambiwa ni maalumu kwa kuwa ni tambiko au hirizi ya Taifa.

TS.
Ona kwetu uwakavyo
nuru njema utoavyo
ona ushangiliwavyo
vigerere sikia

Mwenge ukitoka kwetu
uendelee Mahenge
ila mwakani upange
kuja kututembelea
 
Kwa vile kuna kesi na taarifa za watu kufanyiwa vitendo hivyo mashuleni na kanisani unashauri - shule na makanisa yafutwe????.

Ni waarifu kama waarifu wengine wadhibitiwe tu.

Kwa nini kila kilicho chetu cha asili tunataka tukifute, tuachane nacho?

Kwenye michezo ya soka- kucheza na kuangalia hawapigani na kufanyana vitendo vya ngono?- mbona hatusemi vifutwe? Fiesta n.k , mbona hatusemi vifutwe ila mwenge tu?.
 
Ona kwetu uwakavyo
nuru njema utoavyo
ona ushangiliwavyo
vigerere sikia

Mwenge ukitoka kwetu
uendelee Mahenge
ila mwakani upange
kuja kututembelea
Mkuu umenikumbusha mbali. Uko vizuri
 
Kwa vile kuna kesi na taarifa za watu kufanyiwa vitendo hivyo mashuleni na kanisani unashauri - shule na makanisa yafutwe????.

Ni waarifu kama waarifu wengine wadhibitiwe tu.

Kwa nini kila kilicho chetu cha asili tunataka tukifute, tuachane nacho?

Kwenye michezo ya soka- kucheza na kuangalia hawapigani na kufanyana vitendo vya ngono?- mbona hatusemi vifutwe? Fiesta n.k , mbona hatusemi vifutwe ila mwenge tu?.
Sikushangai mkuu, jina lako ni jibu tosha kwa nini unapenda mwenge
 
Kwa vile kuna kesi na taarifa za watu kufanyiwa vitendo hivyo mashuleni na kanisani unashauri - shule na makanisa yafutwe????.

Ni waarifu kama waarifu wengine wadhibitiwe tu.

Kwa nini kila kilicho chetu cha asili tunataka tukifute, tuachane nacho?

Kwenye michezo ya soka- kucheza na kuangalia hawapigani na kufanyana vitendo vya ngono?- mbona hatusemi vifutwe? Fiesta n.k , mbona hatusemi vifutwe ila mwenge tu?.
Nipe faida tatu tu za mwenge kwasasa?
 
Back
Top Bottom