Kwa sasa Makanisa na misikiti inatosha , ikiwa kuna taasisi inahitaji kutoa Msaada wa kujenga Kanisa na Msikiti hiyo pesa wajenge visima vya maji

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
31,636
Reaction score
81,533
Kwa Tanzania tuna misikiti Mingi na makanisa mengi Sana .

Na ukiangalia idadi ya watu wanaosali bado ni Chache Sana .

Ikiwa tutaangalia mahitaji hasa ya jamii tunaweza kubadilisha matumizi ya hizo pesa.

Mfano wafadhili ambao hujitolea kujenga misikiti na makanisa , jaribuni kufikiri hilo kuwa tunaweza kujenga Visima Vya maji , tunaweza kujenga maktaba , Shule na kusapoti huduma za Afya.


Unaweza kukuta eneo lina misikiti Kumi Ila eneo hilo hilo halina hata kisima kimoja cha Maji ambacho watu wanachota bure.

Au unasikia taasisi imejenga kanisa lenye thamani ya B-Kadhaa Ila eneo hilo hilo halina huduma za kijamii .


Kwa sasa tufanye mambo kwa kuangalia Vipaumbele.


Miaka ya nyuma nilikuwa nikienda msikitini wanaosali hawafiki 05 Ahsubui .

Ila utaona watu wanachangisha kujenga msikiti Mwingine.

Je kwanini wasichangishe kujenga kisima cha Maji , kumbuka kuna familia masikini na duni ambazo haziwezi hata kuoga kwa kukosa maji hapa nazungumzia maeneo ambayo maji yanauzwa.
 
Kuna kijiji kimoja nimeona waturuki wamejenga madipii ya maji mitaani badala ya misikiti. Kujenga msikiti ni kujisumbua tu, wataswali wapuuzi wenye iq ndogo
 
Kuna kijiji kimoja nimeona waturuki wamejenga madipii ya maji mitaani badala ya misikiti. Kujenga msikiti ni kujisumbua tu, wataswali wapuuzi wenye iq ndogo
Kwa hiyo misikiti ni iq ndogo je makanisa?
 
Sipingani na hoja yako kwani imejielekeza katika namna ya kujali na kuheshimu huduma za binadamu zenye kuleta manufaa kwa wanufaika, lakini watu hawa watakaochimbiwa visima na kuboreshewa huduma za Afya bado watakuwa na ulazima wa kuabudu, bado watakuwa na ulazima wa kutekeleza yale yote ayatakayo Mwenyezi Mungu, tunaamini uwepo wa nyumba za ibada katika sehemu husika ni kiashiria kimojawapo cha Amani katik eneo husika, sasa kwa mtazamo wangu naweza kusema kwamba tuendelee kujenga nyumba za ibada na tuendelee kuhamasishana katika kuboresha huduma za kijamii, kwani haya yote ni mambo muhimu kabisa.
 
Halafu pesa za kodi na zile za Dp world zifanye nini?
 
Kuna kijiji kimoja nimeona waturuki wamejenga madipii ya maji mitaani badala ya misikiti. Kujenga msikiti ni kujisumbua tu, wataswali wapuuzi wenye iq ndogo
Wewe Mama toka uachike kwa yule mpemba ukaamua kuichukia mpaka dini yake,
kwa hiyo wenye IQ kubwa ni wale wanaouziwa Chumvi,udongo na maji ili wawe matajiri kimiujiza?

Wewe mwenye IQ kubwa unawazidi nini kina Bakhresa,Mo Dewji,GSM...?
 

Okay vzr
 
Siyo mbaya Nyumba za Ibada kujengwa maana vyote hivyo ni muhimu.
 
Kila msikiti una huduma ya maji kwa wote hapa mtaani kwangu ,tena ni msaada mkubwa sana .

Katika sadaka zinazoendelea ni pamoja na kuweka huduma kama maji hata wapita njia wakanywa..Kwetu huku hata maji yakikata mwezi Misikiiti ni msaada ... Sijajua huko kwenu.
 
Hayo maji ya masikiti ni kwa ajili ya kutoa bure kwa jamii??

Au kwa ajili ya huduma. za msikitini
 
Sio misikiti tu hata nyumba nyingi za waislam wana hizo huduma za maji bure.

Tena sehemu nyingine maji baridi kabisa aiseee.
 
Wewe Mama toka uachike kwa yule mpemba ukaamua kuichukia mpaka dini yake,
kwa hiyo wenye IQ kubwa ni wale wanaouziwa Chumvi,udongo na maji ili wawe matajiri kimiujiza?

Wewe mwenye IQ kubwa unawazidi nini kina Bakhresa,Mo Dewji,GSM...?
huoni hao ni waasia ni asili yao? Nioneshe muislam mmbantu mweusi tii ni tajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…