Kwa picha hii, Maalim Seif alitaka kutuambia nini?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Kuna methali ya Wachina inayosema, ‘’One picture is worth ten thousand words."

Nimejaribu kuiangalia na kufikiri kwa undani (think deeply) kuhusu hii picha ya Maalim Seif aliyopiga kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Umoja wa Mataifa ambao mara nyingi viongozi wakuu wa nchi hutumia kuhutubia.

Nakumbuka wakati nikiwa shule za msingi kuna mwalimu wetu mkuu wa shule alikuwa kila mara kwenye mkusanyiko wa shule (school assembly) alikuwa anapenda kutuambia kwa lugha ya kiingereza tusome kwa bidii kwa sababu ‘’the sky's the limit’’.

Nilipofika sekondari kuna mwalimu mwingine ambaye alinishangaza aliposema ‘the limit's the sky''. Maneno yake yalinifanya nipate mtazamo mwingine kuhusu uhalisia katika maisha.

Baada ya kumaliza elimu ya juu na kuingia mitaani nikaanza kukubaliana na maneno ya mwalimu wangu wa sekondari.

Picha ya Maalim Seif imenirudisha kwenye kumbukumbu ya maneno ya mwalimu wangu wa sekondari aliyosema, ''the limit's the sky''.

Picha hii inanieleza kuwa Maalim Seif anapenda sana ahutubie katika kikao cha umoja wa mataifa lakini the limit’s the sky.

Maalim Seif ameamua mpaka kuigiza akihutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kuhutubia viti pekee ndani ya ukumbi.

Inawezekana wakati akiwa kijana mdogo alidhani ‘’the sky’s the limit’’ katika kufikia ndoto yake ya kuwa Rais wa Zanzibar ili apate fursa ya kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kama Rais wa Zanzibar lakini kwa sasa ndoto hiyo inakuwa ‘’the limit’s the sky’’.

Ndoto yake ilizidi kufifia baada ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar mnamo April 26, 1964 ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilibidi ziwe na mjumbe mmoja kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye ni Rais wa Tanzania.

Kwa sasa mlango wa Maalim Seif kuingia kama Rais wa Zanzibar kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa umefungwa mpaka pale Muungano utakapovunjika.

Hata kama Muungano ukivunjika, CCM Zanzibar hawawezi kukubali kwa njia ya kura ili Maalim Seif awe Rais wa Zanzibar.

Sitaki niwe mpiga ramli lakini mazingira ya kisiasa , kiuchumi na kijamii yanatuambia Maalim Seif dream is too little, too late.

Kwa sasa kilichobaki kwa Maalim Seif ni kuigiza tu kama anahutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa na baada ya kuigiza anarudi Zanzibar na picha zake.

ClI-fMxVAAE2HUp.jpg
 
Kuna methali ya Wachina inayosema, ‘’One picture is worth ten thousand words."

Nimejaribu kuiangalia hii picha ya Maalim Seif aliyopiga kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Umoja wa Mataifa ambao mara nyingi viongozi wakuu wa nchi hutumia kuhutubia.

Nakumbuka wakati nikiwa shule za msingi kuna mwalimu wetu mkuu wa shule alikuwa kila mara kwenye mkusanyiko wa shule (school assembly) alikuwa anapenda kutuambia kwa lugha ya kiingereza tusome kwa bidii kwa sababu ‘’the sky's the limit’’.

Nilipofika sekondari nilikuta na mwalimu mwingine ambaye alinishangaza aliposema ‘the limit's the sky''.

Baada ya kumaliza elimu ya juu na kuingia mitaani nikaanza kukubaliana na maneno ya mwalimu wangu wa sekondari.

Picha ya Maalim Seif imerudisha kwenye kumbukumbu ya maneno ya mwalimu wangu wa sekondari aliyosema, ''the limit's the sky''.

Picha hii inanieleza kuwa Maalim Seif anapenda sana ahutubie katika kikao cha umoja wa mataifa lakini the limit’s the sky.

Maalim Seif ameamua mpaka kuigiza akihutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kuhutubia viti pekee ndani ya ukumbi.

Inawezekana wakati akiwa kijana mdogo alidhani ‘’the sky’s the limit’’ katika kufikia ndoto yake ya kuwa Rais wa Zanzibar ili apate fursa ya kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kama Rais wa Zanzibar lakini kwa sasa ndoto hiyo inakuwa ‘’the limit’s the sky’’.

Ndoto yake ilizidi kufifia baada ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar mnamo April 26, 1964 ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilibidi ziwe na mjumbe mmoja kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye ni Rais wa Tanzania.

Kwa sasa mlango wa Maalim Seif kuingia kama Rais wa Zanzibar kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa umefungwa mpaka pale Muungano utakapovunjika.

Hata kama Muungano ukivunjika, CCM Zanzibar hawawezi kukubali kwa njia ya kura ili Maalim Seif awe Rais wa Zanzibar.

Sitaki niwe mpiga ramli lakini mazingira ya kisiasa , kiuchumi na kijamii yanatuambia Maalim Seif dream is too little, too late.

Kwa sasa kilichobaki kwa Maalim Seif ni kuigiza tu kama anahutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa!

ClI-fMxVAAE2HUp.jpg

sheni.jpg
 
Nikiwa nimemtembelea mama yangu alinipa album la picha, kwenye lile album kulikuwa na picha za zamani za familia yetu. Katika kuangalia zile picha nikaiona picha moja nikiwa mdogo nimekaa kwenye kiti cha dereva na huku nimezuwia usukani wa gari la baba. Hii picha ilinikumbusha kuna siku nikiwa safarini Atlanta,Georgia nikiendesha Mustang rafiki yangu alinipiga picha nimezuwia usukani wa hio gari.(Maalim Seif ikiwa bado yupo hai bado anaishi anaweza kuikamilisha ndoto yake kama ile picha yangu ya utotoni).
 
Back
Top Bottom