Kwa pesa hii naweza kufanya biashara gani?

boy mzuri

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
287
436
Kama mnavyojua hali saivi ni tete japo sio kwa wote...
Kuna ka hela flani nmekapata sa nataka nikazalishe ili japo kupunguza njaa....

Pesa yenyewe ni 5M , mi nipo mkoani na wala sijawahi kufika dar japo nina wenyeji kibao huko ...
Nia yang kwa sasa ni kupeleka biashara dar yaani kutoa mkoani then napeleka dar,
Kwa wenyeji na wazoefu wa biashara, mnaweza kuniambia ni biashara gani ambayo itafaa na inayoweza kulipa .....ntashukuru sana kama mtanipa ushirikiano

AKSANTEN.......
 
Sikia boss!!

Biashara iko hivi... usifanye biashara kuwa SUPER RICH, fanya biashara kwaajili ya kutatua changamoto fulani. Huo ndio ujasiriamali. Kubadili changamoto kuwa fursa, kisha kubadili hiyo fursa sasa iwe biashara yenye kuingiza kipato.

Nakumbuka kipindi bado niko chuo 1st year ama 2nd year mwanzoni, niliona watu wanateseka sana pale Ubungo, Riverside. Mtu anashushwa riverside, inabidi yeye na mizigo yake atembee hadi stendi ya mabasi, yani ni mbali kinyama.

Sasa nikaona fursa ya biashara ya usafirishaji... nikaanza kufatilia. Nilichokipata ni hiki hapa kwa haraka haraka.

●Mkokoteni wa chuma kutengeneza ni 150,000 - 200,000

●Kwa siku mwendesha mkokoteni anapiga trip 15-20

●Trip 1 mara nyingi ni 1500-2000 (maelewano)

●Hivyo basi kwa siku mwendesha mkokoteni kupata 30,000 ni constant.

Mimi niliwaza hivi...

●Kama nikitumia mil 2, naweza kumiliki mikokoteni 10 yenye ubora mzuri.

●Kisha niwaconvince vjn waweze kuendesha hiyo mikokoteni, waone jinsi biashara ilivyo poa... waendeshe mkokoteni hata wiki, waone pesa watakayopiga

●so baada ya hapo ndipo inakuja business side ya hii kitu. Kila mkokoteni m1 ningeukodisha kwa shilingi 3000 kwa siku, so mwendesha kokoteni akipata elfu 30, ananipa elfu 3 tu. Kwa mikokoteni 10 kwa siku nina elfu 30. Kwa kua hii biashara haina kuchagua siku, basi kwa mwezi kupata laki 9 ni jambo linalowezekana.

●Uzuri ni kwamba hautaingia gharama kubwa za service na maintenance. Ndani ya miezi miwili na nusu pesa yako imerudi, unaanza kula faida bila jasho.

Lkn na wewe ufanye study yako, usiingie kichwa kichwa - miaka kadhaa ishapita.

Ni vile kwamba nilikua nina mambo mengi sana, hata chuo kidogo kinishinde, lkn otherwise hii kitu ningeigonga kwa mafanikio makubwa sn.
 
mazao ipo hot mpunga - mchele, mahindi- unga, maharage ,
kwa mazao ya biashara kahawa ya mbozi, pamba na dengu
ndizi za bukoba na za mshale masoko yapo kila kona ila madalali ndo habari ya town.
 
Kama mnavyojua hali saivi ni tete japo sio kwa wote...
Kuna ka hela flani nmekapata sa nataka nikazalishe ili japo kupunguza njaa....

Pesa yenyewe ni 5M , mi nipo mkoani na wala sijawahi kufika dar japo nina wenyeji kibao huko ...
Nia yang kwa sasa ni kupeleka biashara dar yaani kutoa mkoani then napeleka dar,
Kwa wenyeji na wazoefu wa biashara, mnaweza kuniambia ni biashara gani ambayo itafaa na inayoweza kulipa .....ntashukuru sana kama mtanipa ushirikiano

AKSANTEN.......
Kwa ushauri wangu mkuu kama utafanya biashara ya mazao mtafute mtu anaechukua mzigo kwenda dar ili mfanye joint venture usiagize mzingo wote bila kujua industry kwa ujumla! Ukishajua changamoto ndio umwage pesa ktk biashara! Note woga wake ndio umasikin wako! Its u time to do now! remember FailuRe is not an option! Focus on win!
 
mazao ipo hot mpunga - mchele, mahindi- unga, maharage ,
kwa mazao ya biashara kahawa ya mbozi, pamba na dengu
ndizi za bukoba na za mshale masoko yapo kila kona ila madalali ndo habari ya town.
asante sana mkuu ntafanyia kazi ushauri wako
 
Upo mkoa gan mkuu na ww umefikiria kufanya biashara gan kwanz kabla hujapewa ushauri.
 
Kwa ushauri wangu mkuu kama utafanya biashara ya mazao mtafute mtu anaechukua mzigo kwenda dar ili mfanye joint venture usiagize mzingo wote bila kujua industry kwa ujumla! Ukishajua changamoto ndio umwage pesa ktk biashara! Note woga wake ndio umasikin wako! Its u time to do now! remember FailuRe is not an option! Focus on win!
Thanks much brother, ndio uzuri wa kushea mawazo unapata vitu tofauti ....
 
Back
Top Bottom