Kwa nyakati hizi za kileo usimlaumu mzazi direct kwa mtoto kuharibika.

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,311
4,018
Kwa hiki kizazi chenye mazingira yenye extreme exposure yani wazazi mtakuwa mnawaulumu bure. Sasa hivi vijana wadogo wako easily exposed na vishawishi vingi tofauti na hapo awali.

Ngoja nikupe mfano:
Mtoto wa kike akiwa likizo unamfungia ndani ya fence. Muda ule ukiwa kazini yeye huku nyumbani anatazama TV huku akiangalia chanels zenye maudhui secular kama vile nyimbo za wadada wakivaa nusu uchi wakicheza dansi na tamthilia au reality tv shows zikionesha ni namna gani binti akiwa wa mjini mjini ndio rahisi kuishi na mwanaume tajiri au yeye kujipatia utajiri kwa namana hii.

Mama nae akirudi nyumbani unakuta binti anachukuwa simu ya mama bila la mama kujua then anaperuzi huku akiona vituko vingi kwenye networks tofauti

So binti anakuwa influenced na hawa tv na social media personnels kwa kuona kuwa yeye si wa kisasa hadi hapo atapokuwa na lifestyle ile ya kuwa drama queen kama hawa mabinti anao waona kwenye tv na social media.

So, ghafla unaanza kuona mtoto anabadilika kwa namna ya kuogofya huku hamkutajalia mabadiliko hayo na nyumbani kwako mnajitahidi kumlea katika misingi mizuri.

Huo mfano ni mmoja kati ya mingi ambayo ni jinsi gani badly exposed vijana wanakuwa katika teknolojia, mitaani na vijana wa makamo yao hao hao anaokutana nao kanisani au msikitini.

So tunarudi tu pale kuwa kama wewe una muamini Mungu basi unganisha malezi yako imara na muangaza wa Mungu kwa wanao ili washinde vita za vishawishi vya aina yote.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom