Wewe ni kilaza wa hali ya juu. Vitambulisho vya taifa ni zoezi la milele, mtanzania yoyote akiwa na miaka 18 au zaidi anaweza kuomba na akapewa. Baada ya muda fulani kila mtanzania atalazimika kuwanacho apende asipende. Matumizi yake ni haya; 1. kujiandikisha elimu zote za juu ni lazima ukionyeshe. 2. Huwezi kusajili mali zako (gari, nyumba, shamba au akaunti ya banki) bila ya kuwa na kitambulisho cha taifa. 3. Kila unapotembelea kunapotolewa huduma za serikali kama uhamiaji, hospitali, mahakamani n.k ni lazima kuonyesha kitambulisho cha taifa kabla hujahudumiwa. 4 ukitaka kuajiliwa au kusajili biashara yoyote kitambulisho cha taifa ni lazima. Je, unaweza kuwa na maisha bora bila ya mambo tajwa hapo juu? Hili siyo swala la kisiasa ni la kitaifa.