Kwa nini usiamue sasa

TAECOLTD

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
1,051
1,835
Unajua watu wengi hudhani mpaka uwe na mamilioni ndio uweze kufanya biashara...
Je unatambua hata shilingi elfu kumi (10,000) inaweza kuwa kianzio kizuri cha biashara kwako?!
Najua unapinga au unasubiri kujua ni kiaje inawezekana just kwa buku kumi tu..
Zunguka mtaa wako wote tafuta bar ambayo inauza au ina wateja sana kisha tengeneza ukaribu na meneja na mhudumu wa kaunta...mkabidhi mzigo wako akuuzie, mzigo gani huo?!

Sigara inalipa sana na kwa kuanzia unaweza kuinuka hapo. Nunua pakti za Sigara
1)Embassy pakti moja ni 2,500
2)SM pakti moja ni 2,300
3)Sports pakti moja ni 2,300 Nunua mbili itakuwa 4,600
Jumla kuu hapo itakuwa 9,400 hivyo unabakiwa na chenchi 600.
Embassy pakti ikiisha inazalisha Jumla 4,000 faida ikiwa 1,500
Sports na SM pakti ikiisha inazalisha 3,000 faida ikiwa 700 zidisha kwa tatu itakuwa faida 2,100 jumlisha 1,500 itakuwa faida kuu ni 3,600.
Hivyo basi kwa shilingi 9,400 tu ina uwezo wa kukuingizia faida ya 3,600 bado unalia lia mtaani huna ajira?!
Ukiwa na laki moja kisha ukasambaza katika bar kumi tofauti tofauti maana yake utakuwa unapata faida ya 36,000 ndani ya siku moja hadi mbili. Bado tu unahitaji ufafanuzi wa namna gani?! Tatizo sio ukosefu wa ajira bali ni ukosefu wa kipimo cha kufikiri kwa kina kabisa na kubuni aina mbalimbali za biashara. Kwa leo niishie hapa ila natumaini itawasaidia wajasiriamali wenzangu...
Niwatakie jumatatu njema
Mtenga Gerald
TAECO LTD
www.facebook.com/TAECO2012
 
Back
Top Bottom