Right Marker
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 194
- 625
Kwanini ujitoe uhai wako?
Duniani hauko pekee yako. Hebu washirikishe watu wako wa karibu jambo ambalo linakusumbua, hakika utapata majibu kwa sababu wewe sio wa kwanza kukumbwa na hilo jambo.
• KUHUSU CHANGAMOTO:
Changamoto yoyote ya maisha inapokukumba inakuja na hatua tatu. Hatua ya kwanza ni KUKUPA HOFU, wakati huu ambao changamoto inakupa hofu unapaswa kuwa mtulivu, lakini pia unapaswa kujichanganya na wenzako. Hatua inayofuata ni KUKUPA UZOEFU, hapa unaanza kuizoea na kuona ni changamoto ya kawaida kama changamoto zingine. Hatua ya mwisho inayofuata ni KUKUPA NJIA AU MAJIBU ya kutatua changamoto yako, kama ni ugonjwa usiotibika utapata majibu kuwa kuugua sio kufa na si wewe pekee yako kukumbwa na ugonjwa huo.
Sikiliza; wakati wewe unahisi una matatizo, kuna wenzako wana matatizo makubwa zaidi yako lakini wanadunda mtaani na wanatafuta hela.
• MADENI:
Kwanini ujiuwe kwa sababu ya madeni? Kuna wenzako wasipokuwa na madeni wanakosa raha. Wafanyabiashara wengi hawatumii pesa zao kufanyia biashara, wanatumia pesa za mikopo. Unakuta mtu anadaiwa MILIONI MIA lakini kwenye akaunti yake ya benki ana salio la MILIONI MIA TANO, hiyo ndio akili ya biashara - usibebe mayai yote kwenye kapu moja.
• MAPENZI:
Kwanini ujiuwe kwasababu ya mapenzi? - Kuna wenzako ambao awali waliteswa sana na mapenzi kuliko wewe. Lakini sasa hivi wanapendwa na kila mrembo mpaka wanaona kero kupendwa. Kwanini wewe ujiuwe kwasababu ya kutopendwa na mtu mmoja wakati Tanzania kuna watu zaidi ya milioni 60.
• UGUMU WA MAISHA:
Kwanini ujiuwe kwa sababu ya ugumu wa maisha? - Kwani ushawahi kutafuta maisha sehemu nyingine mbali na hapo unapong'ang'ania? Hii nchi ina maeneo mengi na mikoa mingi ambayo wenzako walikwenda kutafuta maisha na wameyapata.
• UGONJWA:
Kwa nini ujiuwe kwasababu ya ugonjwa? - Kuna wenzako washavuka miaka 10 tangu wagundulike kuwa na ugonjwa kama wa kwako, na wanaishi maisha ya furaha.
NB: Kujitoa uhai kwa sababu ya changamoto ya maisha ni sawa na kuvunja pagala la nyumba kwa sababu ya tofali moja lililokaa vibaya.
BY: Right Marker
Dar es salaam
Sept 27, 2024