Kwa nini ujiunge na chuo hiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini ujiunge na chuo hiki

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by mfukoz, May 22, 2012.

 1. m

  mfukoz Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 35
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari wana Jukwaa la Elimu:
  KWA NINI UJIUNGE NA MUGEREZI SPATIAL TECHNOLOGIES
  (MUST COLLEGE)

  Kila mtu anataka na anatamani kufanikiwa. Kijana aliyemaliza elimu ya sekondari na ambaye matokeo yake hayakuwa mazuri. Hakuchaguliwa kwenda kidato cha 5 au chuoni, anakata tamaa na kwa kweli ndoto zake za mafanikio zinafifia. Yeye na wazazi wake wanapoteza matumaini. Wazazi wanasikitika sana kwa vile wamewekeza kwa huyo mtoto kwa miaka zaidi ya12! Wamewekeza muda tangu chekechea, fedha na matumaini yao.

  Mwanafunzi akifika kidato cha 4 au cha 6 tayari anakuwa na ndoto za kuwa Fulani au kufanya kazi Fulani au Kujiunga na shirika Fulani. Basi akifeli mtihani wa mwisho huyo Fulani anayeyuka na anapotea ghafula.

  Habari nzuri ni kuwa, MUST College itakurudishia wewe kijana huyo Fulani wako na kumleta Kwako.

  Hii si hadithi au utani, kwa sababu elimu na utaalamu wa Spatial Technologies unaotolewa na MUST College unahitajika ofisi ZOTE za serikali, mashirika ya Umma, Mashirika ya Kimataifa, Mashirika ya Dini, NGOs zote, na pia unahitajika nje na ndani ya nchi. Kwa hapa Afrika Mashariki, MUST College ni chuo pekee kinachotoa elimu hii kwa vijana wanaomaliza sekondari. Nafasi za kujiajiri au kuajiriwa ni chaguo lako. Kwa kujiunga na MUST College unafungua njia ya kuishi na kufanya kazi katika nchi yoyote hapa Afrika Mashariki na kati; kama vile Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani, Zambia, Malawi, na popote pale kadri ya ndoto na mipango yako.

  MUST College inafundisha utaalamu na ujuzi unaohusika na ukusanyaji, utayarishaji, utumiaji na utunzaji wa taarifa, takwimu, ramani na kumbukumbu. Hakuna kazi wala ofisi yoyote hapa duniani kwa nyakati hizi isiyohitaji utaalamu unaotolewa na MUST College. Ili kutimiza haya, MUST College inamfundisha mwanafunzi teknolojia inayoitwa Spatial Technologies ambayo inahusisha vifaa na utaalamu wa kisasa na zinatambulika dunia nzima. Utaalamu huu unahusisha yafuatayo:

  (a) Geographic Information System (GIS): Huu ni utaalamu kwa kutengeneza mifumo ya taarifa zilizo na mahusiano na ardhi (GIS). Kwa uhakika kila taarifa duniani ina mahusiano na ardhi. Ili kupanga, kutekeleza na kusimamia mpango wowote wa maendeleo kitaifa, au kwa kampuni na hata kwa familia, ni lazima kujua nini kiko wapi, kipoje, na lini? (What is where, when and how). MUST College inafundisha wataalamu wa kujibu maswali haya.

  (b) Global Positioning System (GPS): Huu ni utaalamu wa kutumia kifaa cha GPS kutambua mahali ulipo na kukusanya taarifa za mahali hapo. Wataalamu katika fani mbali mbali wanatumia utaalamu wa GPS katika kazi zao za kila siku. Hawa wataalamu ni pamoja na wahandisi, wanajeshi, polisi, wanyama pori, mazingira, misitu, ujenzi n.k. Mwanafunzi anayepata ujuzi huu sio tu ataweza kujiariri, bali pia soko lake ni kubwa sana.

  (c) Mobile Mapping: Utaalamu huu unatumia simu yako ya mkononi. Kwa wengine simu zinatumia hela zao. Lakini kwa mtaalamu atakayepata ujuzi MUST College, simu ni mtaji na kiwanda cha kumzalishia fedha. Mwanafunzi atafundishwa jinsi ya kutumia simu ya mkononi kutoa ushauri wa kitaalamu wa kukusanya taarifa na hivyo kupata fedha nzuri.

  (d) Satellite Image Processing: Utaalamu huu kwa sasa unatumiwa pamoja na utaalamu wa GIS na GPS. Mtaalamu atakayemaliza MUST College na utaalamu wa satellite image processing, atakuwa na uwezo wa kufanya kazi na makampuni yanayotoa ushauri wa kitaalamu katika nyanja mbali mbali, mfano mipango ya miji, utunzaji mazingira, uthamini wa majengo, kilimo, uhandishi wa habari, ulinzi, mifugo, afya, elimu, n.k.

  (e) Internet Mapping : Utaalamu huu unamuwezesha mwanafunzi kuweza kutumia Internet kutunza kumbukumbu na taarifa za kijiographia na kutengeneza ramani zinazoweza kutumiwa na watu wengi kwa wakati mmoja kwenye mtandao. Kila shirika, kampuni au mtu binafsi mwenye website au blog, ni mteja mzuri wa utaalamu huu wa Internet Mapping

  (f) Ujasiriamali: Haitoshi kumpa mwanafunzi ujuzi bila mwongozo wa kujitegemea. Kwa kuwa lengo kuu la MUST College ni kumpa mwanafunzi matumaini mapya ya kutumia fursa mbali mbali zinazotokana na utaalamu atakaoupata, MUST College itamtayarisha mwanafunzi huyu kwa kumpa uthhubutu na ujasiri wa kufanya kazi kwa kijiari na hatimaye kuajiri vijana wengine. MUST College ni zaidi ya Chuo. Ni UFUNGUO

  Kozi ya Spatial Technologies kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na sita ni ya miaka miwili na lengo kuu la MUST College ni kuleta matumaini mapya kwa vijana waliomaliza sekondari, kwa kuwapatia fani mpya katika ulimwengu wao wa dotcom. Kozi ya Spatial Technologies ni zaidi ya ICT, ni zaidi ya Programming, ni zaidi ya Database, ni zaidi ya Biashara, ni zaidi ya Uhasibu, ni zaidi ya Uhandisi, ni zaidi na zaidi ya ....... Kwa nini? Kwa sababu hawa wote wanahitaji utaalamu wa Spatial Technologies katika fani zao.

  Kutokana na maombi ambayo tayari yameisha fika ofisini za MUST College, wahitimuwanaomaliza vyuo mbali mbali (vya digrii na stashahada) na kwa fani zote, tunao mpango wa kuanzisha kozi ya mwaka mmoja kwa ajili ya hao. Wahitimu hawa wa vyuo, watafaidika na kozi za MUST College kwa vile hawa wameishakuwa na utaalamu katika fani zao, na hivyo masomo ya GIS, GPS, Mobile Mapping. Internet Mapping na Ujasiriamali yatawasaidia sana kuwa na ujuzi (practical skills) wakijiunga na masomo yetu ya mwaka mmoja.

  Waajiri kwa sasa wanatafuta wasomi wenye pia ujuzi wa Spatial Technologies.

  MUST College kwa sasa ipo Dar es salaam, Ubungo Plaza, na ina mipango ya kufungua vyuo kwenye miji mikubwa- Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma.

  Masomo ya muhula mpya yataanza tarehe 2 July 2012.
   
 2. Eghorohe

  Eghorohe JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hadanganyiki mtu na hivyo vyuo vyako vya uchocholoni Kariakoo,kwa hiyo sifa za kujiunga lazima mtu awe amefeli kwanza(kilaza) tehe tehe tehe kwanza recognition hiko kyuo kyako ni zero mnabuni biashara ili kupata pesa na hali hamna viwango.
   
 3. marthaflo

  marthaflo Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  vinasaidia
   
Loading...