Kwa nini tunashindwa hili la kipindupindu?

Harrison Justine

JF-Expert Member
Jun 19, 2015
1,136
559
Kwa muda muda mrefu tangu 1981 tangu kipindupindu kilipobisha hodi Tanzania bado hakijatoka. Mwaka jana mlipuko wa ugonjwa huu uliripotiwa katika mkoa wa Dar es salaam na hadi sasa imeripotiwa katika baadhi ya mikoa ambako Mwanza na Mara ndio vinaoonekana kuwa vinara kwa kuwa na wagonjwa wengi.Swali nikuwa, je hatuwezi kupunguza kasi hii au kuutokomeza kabisa?
Kipindupindu ni ugonjwa unaoenea haraka na chanzo chake kikuu ni uchafu. Je hatuwezi kujisimamia kufanya usafi katika mazingira tunayoishi au mahala petu pa kazi? Jibu harakaharaka ni kuwa tunaweza, sasa ni kwa nini bado ugonjwa huu unatuzidi kasi ya kuenea? Jawabu kwa mawsali yote ni uzembe na kutokujali.
Kwa nini nasema uzembe na kutokujali? Tuna maafisa afya kata kila kona ya nchi na ninadhani ni watu wanaoelewa vyema majukumu yao ya kazi bila kusukumwa. Hawa kama watasimamia zoezi la usafi nadhani madhara ya kulipuka kwa ugonjwa huu utapungua. Pili kama hawa watatoa elimu kwa raia katika maeneo yao jinsi ya kufanya mfano; 1. kunawa mikono kwa sabuni mara ya kutoka chooni 2. kula vyakula vya moto. 3. kuepuka kula vyakula visivyooshwa kwa maji safi mfano matunda nk. 4. kuchemsha maji ya kunywa. 5. kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kabla ya kula chochote. 6.kuwa na vyoo safi vilivyo na mifuniko ili kuzuia nzi . 7. Kutokujisaidia ovyo kando au karibu na vyanzo vya maji. 8. Kuzingatia kanuni zote za afya nk.
Kama tutazingatia yote hapo juu na mengine ambayo sikuyataja basi kwa kiwango fulani tutakuwa tumepiga hatua moja , mbili ya kuutokomeza ugonjwa hu ambao sasa ni tishio kwa nchi yetu. Lakini pamoja na yote haya angalizo hili litiliwe mkazo katika baadhi ya maeneo.
1. Baadhi ya grocery au bar vyakula vinauzwa katika usalama mdogo mno wa afya. Wauzaji wengi au wahudumu hawazingatii kanuni za afya mfano kuweka chakula kuwa katika hali ya usafi kama vile kuwa ndani ya kabati safi. Nyama au chips kama ilivyozoeleka vinang'inizwa na kuachiwa nzi kutalii wapendavyo.
2.Watendaji wa afya hawapiti maeneo ya grocery au bar hizi kufanya ukaguzi na badala yake hujikita kukimbizana na wauza vyakula kwenye toroli na kina mama ntilie.
3. Maji machafu yanayotoka kwenye baadhi ya meneo haya grocery pamoja na bar hizi humwagwa ovyo na bila kuelekezwa eneo maalumu.
Mwisho ni matumaini yangu kuwa kama tutaoonyesha kujali, gonjwa hili litatoweka kabisa nasi hatutakuwa kwenye hatari tena.
 
Back
Top Bottom