Kwa nini Shilogile asijiuzulu?

Kwa nini Shilogile asijiuzulu?

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,578
KUMEKUWA na sauti mbalimbali za watetea haki za binadamu, wanasiasa na baadhi ya wananchi wakimtaka kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, ajiuzulu kupisha uchunguzi dhidi ya jeshi hilo.

Hii ni baada ya kujeruhiwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, ambaye ndugu zake wanadai amepigwa risasi na askari wa jeshi la polisi katika harakati za kumkamata.

Sheikh Ponda alijeruhiwa Agosti 11 mjini Morogoro, tukio lililoelezwa na Shilogile kuwa lilitokea wakati askari wakiwa katika harakati za kutaka kumkamata kutokana na madai ya kutoa maneno ya uchochezi akiwa katika moja ya misikiti visiwani Zanzibar.

Ikumbukwe kuwa kabla ya tukio la Sheikh Ponda tayari kulikuwa na sauti zilizokuwa zikihanikiza kamanda huyo ajiuzulu kwa heshma yake, au afukuzwe kazi kwa ajili ya kulinda heshma ya jeshi la polisi inayozidi kupotea mioyoni mwa wananchi wengi kutokana na matukio mbalimbali yenye utata.

Hii ni baada ya mauaji yenye utata ya Ally Singano "Zona", aliyekuwa akiuza magazeti jirani na kituo kikuu cha mabasi mkoani Morogoro wakati polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 27, mwaka jana.

Kiuhalisia hakukuwa na sababu ya msingi ya kupelekea hata Zona kufa katika tukio lile kama Shilogile angeweka unazi wa kisiasa pembeni na kufanya kazi kwa taaluma yake ya uaskari, hii ni pamoja na kufuata Katiba kwa sababu maandamano ni haki ya msingi ya Kikatiba kwa kila Mtanzania na jukumu la polisi ni kuyalinda na kuhakikisha vurugu hazitokei.

Nimeanza na haya katika makala yangu hii ya kutaka RPC Shilogile, ajiuzulu au afukuzwe kazi kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo na kusababisha madhara mbalimbali katika jamii.

Kuthibitisha kuwa kamanda huyu anawajibika kujiuzulu, hapa tuangalie mambo ya ajabu yaliyotokea chini ya uongozi wake kuanzia alipokuwa kamanda wa polisi mkoa wa Ilala.

Kati ya Aprili na Juni 2011 askari wawili waliovaa kiraia wakiwa katika gari ambalo Shilogile alipewa namba yake walimvamia dereva teksi eneo la Tabata Magengeni.

Dereva huyo alikuwa anamsubiri abiria ampeleke Ubungo ambapo askari hao walifyatua risasi mbili hewani wakimtuhumu kuwa alikuwa amepakia nyama ya ng'ombe katika buti ya gari.

Wananchi waliokuwa kituoni muda huo walipata hofu juu ya hali hiyo na wakafikiri watu wale ni majambazi wakatoa taarifa ya moja kwa moja kwa Shilogile tena kwa wakati.

Jambo la kusikitisha hakukuwa na hatua ya dharura ya kuhakiki kama ni majambazi au ni askari mpaka ilipofika saa 11 jioni ya siku hiyo, ndio askari wakapiga simu kwa mtoa taarifa wakiulizia mazingira ya tukio ili wafanyie kazi.

Licha ya kuelezwa mazingira ya tukio zima pia walielezwa juu ya kuwapo kwa maganda ya risasi katika eneo la tukio.

Mategemeo ya wananchi yalikuwa askari wafike na kuanza uchunguzi wao, lakini hawakufanya hivyo na baada ya siku tatu Shilogile alitoa kauli kuwa askari walikuwa kazini.

Alishindwa kuainisha kama askari wake walikuwa na haki ya kurusha risasi hewani kumdhibiti mtuhumiwa aliyefanya fujo au kukimbia!

Kwa nini hawakumkamata na kwa nini polisi wale ambao walitambulika baadaye wasitoe maelezo ya kina ya kufikia hatua ya kutishia raia kwa risasi tena wakiwa wamelewa?

Kati ya Juni na Julai mwaka huo huo likafanyika tukio lingine la mtu aliyekuwa katika gari kurusha risasi hovyo katika eneo la Tabata Bima kisa kikiwa ni kutofautiana na mwendesha pikipiki, hili nalo Kamanda Shilogile hakuweza kulifanyia kazi zaidi ya kusema yuko likizo na atafutwe mtu aliyeachiwa nafasi yake kwa wakati huo ambaye alimtaja kwa jina la Sada.

Machi mwaka jana baada ya utafiti wa muda juu ya ongezeko la watu wanaojiuza katika eneo la Buguruni gazeti hili lilibaini kuwapo kwa watu wanaowatumia kama kitega uchumi sharti likiwa ni kupeleka kiasi cha fedha kwa baadhi ya askari kupitia kwa wakala wao mmoja na wanaposhindwa kufanya hivyo huadhibiwa kwa vipigo na kila aina ya udhalilishaji.

Hali hii ilimuibua binti mwenye umri wa miaka 26 wakati huo Wilhelmina ambaye alidai kuingizwa chupa sehemu za siri na hao mawakala wanaokusanya fedha kwa machangudoa. Alitoa taarifa polisi akapewa RB akatibiwa hospitali.

Alikuwa na vyeti na polisi waliviona na wahusika walikamatwa lakini mmoja wa maofisa wa polisi aliwakingia kifua na kesi haikupelekwa mahakamani, taarifa zilipofika kwa Shilogile alisema atafanyia kazi.

Baada ya wiki mbili Shilogile alimshambulia kwa maneno mwandishi aliyekuwa akifuatilia suala hili kwa kumtuhumu kuwa amehongwa na machangudoa ili alichafue jeshi.

Alitoa kauli hii mbele ya maofisa wenzake ndani ya jeshi. Hakufikiria maumivu aliyoyapata mlalamikaji, wala hakumpa thamani ya utu wake na akamuweka katika mizani ya uchangudoa dada aliyelalamika kutokutendewa haki.

Kamanda huyu akaahidi kumfuatilia mwandishi ajue amehongwa kiasi gani badala ya kufanyia kazi malalamiko dhidi ya watendaji walio chini yake.

Akiwa mkoani Morogoro mbali na matukio hayo mawili ya Zona na Sheikh Ponda yaliyozua utata, bado Shilogile alishindwa kutimiza wajibu wake katika kazi kuchunguza na kuchukua hatua sahihi katika suala la Boniface Mgwao (37) anayedaiwa kuuawa na askari wa kituo cha polisi Mikumi.

Katika maelezo yake Shilogile anasema kijana huyo baada ya kukamatwa na kupakiwa katika pikipiki aliruka akiwa njiani na kisha kupata majeraha kichwani.

Anaongeza kuwa baada ya kupata jeraha alianza kuwarushia mawe askari na wananchi waliomkamata kabla ya kukamatwa tena na kufikishwa kituoni.

Hatuambii kama askari wake walimpeleka kupata matibabu kuanzia siku hiyo ya Julai 8 waliyomkamata hadi mauti yalipomkuta.

Anasema polisi wake hawahusiki na tukio hilo. Hajafanya uchunguzi, kapokea taarifa tu hajiulizi wala hawaulizi watu wake maswali rahisi walifanya nini baada ya kuona mtuhumiwa ana jeraha.

Huyu ndiye kamanda wa mkoa wa Morogoro ambaye kwa matendo haya anayo sababu ya kuendelea kutumikia watu kwa nafasi yake?

Chanzo: Tanzania Daima
 
Mie ninavyomfahamu Shilogile, kama vyeo vya polisi vingekuwa vinajali morals za mtu, hata u-koplo asingepewa. Lakini Polisi Tanzania ukiwa angalau na ka-degree au ka-diploma kamoja basi wewe umeula, wala hawajali uwezo (capability) na busara (rational thinking) kama kiongozi wa polisi. Ndio kina Shilogile waliojiunga na Polisi wakiwa na advanced Diploma toka Mzumbe neema zikawafungukia.

Kwa muda mrefu wasomi hawakutaka kujiunga na polisi, na wachache waliojiunga kama kina Shilogile waliingia kwa ajili ya kuona katika jeshi la polisi lisilo na wasomi kuna nafasi za kujinufaisha kibinafsi. Wao sio dedicated policemen. Ndio maana utakuta viongozi wengi wa polisi ambao walipanda sana vyeo kwa kuwa waliingia polisi na ka-degree au ka-diploma wanafanya mambo ya ajabu kabisa, na lolote wanaloambiwa na CCM wanatii, kwa kuwa wapo pale kulinda maslahi yao binafsi na ya wanasiasa ambao watawapandisha vyeo ikiwa watatenda kulingana na wanachoamriwa, na katu lengo lao si kulinda usalama wa Watanzania.

Kazi za kulinda usalama wa raia zinafanyika kama jambo ambalo inabidi wafanye kwa sababu wao ndio polisi, lakini haliko katika mioyo yao (superficial commitment to safeguarding civilian rights and safety)

Hata siku moja usidhani kwamba watu kama kina Shilogile na mapolisi wenzake wengi tu wako pale kwa ajili ya kuwatumikia wananchi kama lengo la kwanza. Usalama wa raia ni jambo la mwisho kabisa katika ajenda zao.
 
Kuna ukweli katika hili. Wanaoitwa wasomi walienda polisi kwanza kwa kukosa ajira na pili ilionekana ndiyo taasisi ambayo haina wasomi kwa hiyo ukifika tu na kadigrii ama kadiploma unapewa nyota ama staff sergeant. Wasomi wengi walioingia polisi si kwa wito, bali wasaka tonge. Ndiyo sababu baada ya kuingia kwa wasomi mambo yameharibika zaidi. Jeshi la polisi linahitaji watu wa kujituma zaidi kuliko watafuta vyeo. Na mifano ipo mingi. Wengi ya wanaokataa rushwa ni polisi wa chini, mbona hatujawahi kusikia maafisa wakikataa rushwa??? Hawapewi? Makamanda polisi na rushwa, napo inabidi kwenda Takukuru, kufanya nini wakati ushahidi upo. Ni matajiri wakutisha.
 
You nailed it! umetisha..kwani na CHAGONJA nae ana ka diploma ama degree? nae si Division Zero/ form four leaver?
 
WanaJF huyo Kamanda hawezi kujiuzulu maana hakuna tabia ya kuwajibika kwenye jeshi la polisi nchini.
Matamko ya polisi kwenye tukio hilo yanaonyesha kuwa hakuna wa kujiuzulu ila Shilogile anasubiri kupata utumishi uliotukuka kama Kamuhanda.
Hakuna utawala Bora jeshi la polisi.
 
Akijiuzulu, na aliyemtuma inabidi ajiuzulu. Cha kujiulizwa alitumwa na nani kwa malengo gani?
 
KUMEKUWA na sauti mbalimbali za watetea haki za binadamu, wanasiasa na baadhi ya wananchi wakimtaka kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, ajiuzulu kupisha uchunguzi dhidi ya jeshi hilo.

Hii ni baada ya kujeruhiwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, ambaye ndugu zake wanadai amepigwa risasi na askari wa jeshi la polisi katika harakati za kumkamata.

Sheikh Ponda alijeruhiwa Agosti 11 mjini Morogoro, tukio lililoelezwa na Shilogile kuwa lilitokea wakati askari wakiwa katika harakati za kutaka kumkamata kutokana na madai ya kutoa maneno ya uchochezi akiwa katika moja ya misikiti visiwani Zanzibar.

Ikumbukwe kuwa kabla ya tukio la Sheikh Ponda tayari kulikuwa na sauti zilizokuwa zikihanikiza kamanda huyo ajiuzulu kwa heshma yake, au afukuzwe kazi kwa ajili ya kulinda heshma ya jeshi la polisi inayozidi kupotea mioyoni mwa wananchi wengi kutokana na matukio mbalimbali yenye utata.

Hii ni baada ya mauaji yenye utata ya Ally Singano “Zona”, aliyekuwa akiuza magazeti jirani na kituo kikuu cha mabasi mkoani Morogoro wakati polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 27, mwaka jana.

Kiuhalisia hakukuwa na sababu ya msingi ya kupelekea hata Zona kufa katika tukio lile kama Shilogile angeweka unazi wa kisiasa pembeni na kufanya kazi kwa taaluma yake ya uaskari, hii ni pamoja na kufuata Katiba kwa sababu maandamano ni haki ya msingi ya Kikatiba kwa kila Mtanzania na jukumu la polisi ni kuyalinda na kuhakikisha vurugu hazitokei.

Nimeanza na haya katika makala yangu hii ya kutaka RPC Shilogile, ajiuzulu au afukuzwe kazi kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo na kusababisha madhara mbalimbali katika jamii.

Kuthibitisha kuwa kamanda huyu anawajibika kujiuzulu, hapa tuangalie mambo ya ajabu yaliyotokea chini ya uongozi wake kuanzia alipokuwa kamanda wa polisi mkoa wa Ilala.

Kati ya Aprili na Juni 2011 askari wawili waliovaa kiraia wakiwa katika gari ambalo Shilogile alipewa namba yake walimvamia dereva teksi eneo la Tabata Magengeni.

Dereva huyo alikuwa anamsubiri abiria ampeleke Ubungo ambapo askari hao walifyatua risasi mbili hewani wakimtuhumu kuwa alikuwa amepakia nyama ya ng’ombe katika buti ya gari.

Wananchi waliokuwa kituoni muda huo walipata hofu juu ya hali hiyo na wakafikiri watu wale ni majambazi wakatoa taarifa ya moja kwa moja kwa Shilogile tena kwa wakati.

Jambo la kusikitisha hakukuwa na hatua ya dharura ya kuhakiki kama ni majambazi au ni askari mpaka ilipofika saa 11 jioni ya siku hiyo, ndio askari wakapiga simu kwa mtoa taarifa wakiulizia mazingira ya tukio ili wafanyie kazi.

Licha ya kuelezwa mazingira ya tukio zima pia walielezwa juu ya kuwapo kwa maganda ya risasi katika eneo la tukio.

Mategemeo ya wananchi yalikuwa askari wafike na kuanza uchunguzi wao, lakini hawakufanya hivyo na baada ya siku tatu Shilogile alitoa kauli kuwa askari walikuwa kazini.

Alishindwa kuainisha kama askari wake walikuwa na haki ya kurusha risasi hewani kumdhibiti mtuhumiwa aliyefanya fujo au kukimbia!

Kwa nini hawakumkamata na kwa nini polisi wale ambao walitambulika baadaye wasitoe maelezo ya kina ya kufikia hatua ya kutishia raia kwa risasi tena wakiwa wamelewa?

Kati ya Juni na Julai mwaka huo huo likafanyika tukio lingine la mtu aliyekuwa katika gari kurusha risasi hovyo katika eneo la Tabata Bima kisa kikiwa ni kutofautiana na mwendesha pikipiki, hili nalo Kamanda Shilogile hakuweza kulifanyia kazi zaidi ya kusema yuko likizo na atafutwe mtu aliyeachiwa nafasi yake kwa wakati huo ambaye alimtaja kwa jina la Sada.

Machi mwaka jana baada ya utafiti wa muda juu ya ongezeko la watu wanaojiuza katika eneo la Buguruni gazeti hili lilibaini kuwapo kwa watu wanaowatumia kama kitega uchumi sharti likiwa ni kupeleka kiasi cha fedha kwa baadhi ya askari kupitia kwa wakala wao mmoja na wanaposhindwa kufanya hivyo huadhibiwa kwa vipigo na kila aina ya udhalilishaji.

Hali hii ilimuibua binti mwenye umri wa miaka 26 wakati huo Wilhelmina ambaye alidai kuingizwa chupa sehemu za siri na hao mawakala wanaokusanya fedha kwa machangudoa. Alitoa taarifa polisi akapewa RB akatibiwa hospitali.

Alikuwa na vyeti na polisi waliviona na wahusika walikamatwa lakini mmoja wa maofisa wa polisi aliwakingia kifua na kesi haikupelekwa mahakamani, taarifa zilipofika kwa Shilogile alisema atafanyia kazi.

Baada ya wiki mbili Shilogile alimshambulia kwa maneno mwandishi aliyekuwa akifuatilia suala hili kwa kumtuhumu kuwa amehongwa na machangudoa ili alichafue jeshi.

Alitoa kauli hii mbele ya maofisa wenzake ndani ya jeshi. Hakufikiria maumivu aliyoyapata mlalamikaji, wala hakumpa thamani ya utu wake na akamuweka katika mizani ya uchangudoa dada aliyelalamika kutokutendewa haki.

Kamanda huyu akaahidi kumfuatilia mwandishi ajue amehongwa kiasi gani badala ya kufanyia kazi malalamiko dhidi ya watendaji walio chini yake.

Akiwa mkoani Morogoro mbali na matukio hayo mawili ya Zona na Sheikh Ponda yaliyozua utata, bado Shilogile alishindwa kutimiza wajibu wake katika kazi kuchunguza na kuchukua hatua sahihi katika suala la Boniface Mgwao (37) anayedaiwa kuuawa na askari wa kituo cha polisi Mikumi.

Katika maelezo yake Shilogile anasema kijana huyo baada ya kukamatwa na kupakiwa katika pikipiki aliruka akiwa njiani na kisha kupata majeraha kichwani.

Anaongeza kuwa baada ya kupata jeraha alianza kuwarushia mawe askari na wananchi waliomkamata kabla ya kukamatwa tena na kufikishwa kituoni.

Hatuambii kama askari wake walimpeleka kupata matibabu kuanzia siku hiyo ya Julai 8 waliyomkamata hadi mauti yalipomkuta.

Anasema polisi wake hawahusiki na tukio hilo. Hajafanya uchunguzi, kapokea taarifa tu hajiulizi wala hawaulizi watu wake maswali rahisi walifanya nini baada ya kuona mtuhumiwa ana jeraha.

Huyu ndiye kamanda wa mkoa wa Morogoro ambaye kwa matendo haya anayo sababu ya kuendelea kutumikia watu kwa nafasi yake?

Chanzo: Tanzania Daima
Ngugu kijana kwanza kabisa naomba nikupongeze kwa ujasiri wako wa kutaka kamanda shilogile ajiuzuru.Nadhani we kijana ufahamu kwamba kwa sasa jeshi la polisi limefunga ndoa na CCM na katika hii ndoa,makamanda wote wa polisi watakao fanikisha zoezi la kuwamaliza wapinzani wa serikali yetu sikivu iliyovaa miwani ya mbao watapandishwa vyeo na kuwa makamishina wakuu au wasaidizi,tunu hii itaambatana na tunu ya utumishi uliotukuka.Rejea IGP mwema,Kamuhanda na wengine wengi.Kwaiyo basi kwa mujibu wa utaratibu huu,ndugu kamanda shilogile hatajiuzuru isipokuwa tutampandisha cheo ili aendelee kuongoza vyema vijana wetu wa jeshi la polisi ambao wanapiga raia,rejea tamko la waziri mkuu Pinda bungeni kwamba serikali imechoka,raia wapigwe tu.Mwisho kabisa naomba nikwambie kijana kwamba kwa sasa tupo kwenye msimu wa kupigwa,swala la sheikh ponda ni bahati mbaya tu jamani,tuendelee kuliamini jeshi letu la polisi.KIGUMU CHAMA CHA MAPINDUZI,ZIDUMU FIKRA ZA AMIRI JESHI MKUU.
 
You nailed it! umetisha..kwani na CHAGONJA nae ana ka diploma ama degree? nae si Division Zero/ form four leaver?

Mkuu Handsome, hao wenye Div Zero katika polisi wamemezwa kabisa na wale polisi wanaojiona wasomi. Fikiria sasa unapata nini ukichanganya hao polisi wasomi waliongia polisi kwa sababu za kujinufaisha kibinafsi, na hao wenye Division Zero waliobangaiza wee hadi wakapewa hivyo vyeo - hapo utaanza kupata picha tuna Jeshi la Polisi la namna gani!

Kwangu mimi hitimisho langu ni moja;

Tanzania tuna Jeshi la Polisi kama vile kichaa kapewa rungu alinde watoto!

Raia wa Tanzania ndio hao watoto wanaolindwa na huyo kichaa.
 
Mnamuonea shilogile bwana hata ponda ajiuzuru kuongoza jumuia yake.
 
Mkuu Henge, hapa tunajadili suala ambalo linaenda mbali sana zaidi ya Ponda na risasi yake ya begani ambayo ilipita kwa namna moja au nyingine bila kuvunja mfupa wowote. Sasa kama upeo wako wa kuona katika hili suala unaishia kwenye issue ya Ponda ni afadhali uwaachie wengine wachangie.
 
Huyu kamanda shilogile anasitahili pongezi Kubwa sana kwa jinsi alivyoweza kuwasimamia vijana wake kupambana na gaidi hatari Kama ponda. Ponda ni gaidi la kiislaamu na chama chao cha magaidi cuf wapo nyumbani yake na Huyu ndiye aliyeratibu kuwamwagia tindikali wale watotot Kisstie na Katie Huyu ni muuaji mkubwa yaani kwa kuwa wamekuwa ni wakristo basi wanawamagia acid Mbona hawa cuf awajakutana na waandishi wa habari katika tokio mbaya Kama Hilo wanakimbilia kuongelea gaid Wao ponda kamanda wa Moro anafaa kuwa IGP na Huyu gaid ashughuliwe ipasavyo ili iwe fundisho kwa wengine Huyu ni kuuwa tu ongereni sana police mngemtwanga ya kichwa huyo gaid kwani ni osma wa Tanzania
 
Mkuu Henge, hapa tunajadili suala ambalo linaenda mbali sana zaidi ya Ponda na risasi yake ya begani ambayo ilipita kwa namna moja au nyingine bila kuvunja mfupa wowote. Sasa kama upeo wako wa kuona katika hili suala unaishia kwenye issue ya Ponda ni afadhali uwaachie wengine wachangie.

mkuu umezungumzia elimu ya shilo na kuwa unaona kama upeo wake ni mdogo sana, Anaweza kuwa na makosa yake sijakataa lakini si kila mwenyemakosa ajiudhuru tu huoni kama kunatatizo hapo? Hiv unazani elimu ni tatizo na je tutaendelea kuweka mpaka lini hao wanaoishia la saba mkuu. Lazima jeshi libadilike na huu ni mpito tu!
 
Kuna ukweli katika hili. Wanaoitwa wasomi walienda polisi kwanza kwa kukosa ajira na pili ilionekana ndiyo taasisi ambayo haina wasomi kwa hiyo ukifika tu na kadigrii ama kadiploma unapewa nyota ama staff sergeant. Wasomi wengi walioingia polisi si kwa wito, bali wasaka tonge. Ndiyo sababu baada ya kuingia kwa wasomi mambo yameharibika zaidi. Jeshi la polisi linahitaji watu wa kujituma zaidi kuliko watafuta vyeo. Na mifano ipo mingi. Wengi ya wanaokataa rushwa ni polisi wa chini, mbona hatujawahi kusikia maafisa wakikataa rushwa??? Hawapewi? Makamanda polisi na rushwa, napo inabidi kwenda Takukuru, kufanya nini wakati ushahidi upo. Ni matajiri wakutisha.
Sawa kabisa ila tusisahau kuwa hawa maafisa wa polisi ukianzia na IGP mwenyewe kwa nje wanaonekana ni polisi kwa vile wanavaa uniform za kipolisi lakini ndani ya mioyo yao hao ni MAKADA WA CCM 100%.Mweke kando huyo Shinokile mlete Kamuhanda alivyoamuru mwandishi wa habari auwawe mbele yake,akiwepo kwenye eneo la tukio na bado hakufanywa chochote mbali ya tume zilizoundwa kumtaja kuhusika na mauwaji hayo.Sina hakika lakini kulikuwa na mchakato wa kumpandisha cheo na kumhamishia makao makuu yaani DAR.Polisi hawapo kulinda wananchi na mali zao ila kazi yao kubwa ni kulinda MATUMBO YAO NA FAMILIA ZAO.
 
hili gazeti la udaku huandika vituko kweli,
hiyo mbona siyo sababu ya kufanya mtu ajiuzuru.
 
mkuu umezungumzia elimu ya shilo na kuwa unaona kama upeo wake ni mdogo sana, Anaweza kuwa na makosa yake sijakataa lakini si kila mwenyemakosa ajiudhuru tu huoni kama kunatatizo hapo? Hiv unazani elimu ni tatizo na je tutaendelea kuweka mpaka lini hao wanaoishia la saba mkuu. Lazima jeshi libadilike na huu ni mpito tu!

Hapana Mkuu Henge, sina tatizo kabisa na elimu ya Shilo. Tatizo langu kubwa kwa watu aina yake ni kutoitumia hiyo elimu waliyonayo kulibadili Jeshi la Polisi, na kukubali kutumiwa kama puppets na wanasiasa. Ndio maana nikasema, watu kama Shilo tatizo lao linaanzia kwenye ukweli kwamba hawakujiunga na Jeshi la Polisi kwa kuwa walikuwa na mapenzi kuhakikisha wanalinda usalama na amani ya raia wa Tanzania, bali kwa kuwa waliona nafasi ya kujinufaisha kibinafsi.

Hawajali kinachowapata wananchi, wala uonezi unaofanywa na askari polisi walio chini yao kwa wananchi na watu wa kawaida. Kitu cha kwanza wanachofanya raia wakionewa ni kutoa matamko yenye kuonyesha kwamba polisi walikuwa na haki na raia ndio walikosea, hata kama dunia nzima inaona ukweli kwamba wanasema uongo, au inahusu mauaji ya raia wasio na hatia, au kufanyiwa uonevu wa aina yeyote ile.

Na kinachoudhi hata zaidi ni kwamba hawa wasomi kama kina Shilo ndio wamekuwa vinara wa kutumiwa na wanasiasa, na hasa chama kilichoko madarakani CCM, katika kukandamiza haki za msingi za raia, kufumbia macho kila aina ya uhalifu nchini, kutia ndani madawa ya kulevya, ujangiri, rushwa/ufisadi na hata ujambazi. Na wanajua hivi kwa kuwa wanataka kujipendekeza kwa viongozi wa siasa, ili hata wapandishwe vyeo.

Ukiwauliza watakwambia mie siwezi kupigana hiyo vita ya kulisafisha Jeshi la Polisi peke yangu kwa kuwa Jeshini unafuata amri ya Mkuu wako bila kuhoji - ikionyesha wazi kwamba wamekubali kutumika kama vibaraka wa viongozi katika kukandamiza watanzania na raia wasio na uwezo wa kifedha. Tunajua kabisa jeshini unafuata amri bila kuhoji pale tu amri hiyo ni halali na haikiuki haki ya msingi ya raia, kulingana na kapo wanachotoa.

Hivyo basi utaona ni wazi sana kwamba hawakujiunga na polisi kwa nia ya kuwatumikia wananchi, bali kwa sababu zao za kibinafsi, na ndio maana watafanya chochote wanachoambiwa na mabwana zao wa kisiasa.

Leo Shilo akiambiwa na mwanasiasa hakikiksha umemfundisha Henge adabu, basi ujue umekwisha. Sasa kama sio msomi kama Shilo ambaye anaweza kumjibu mwanasiasa kwamba mimi kiapo changu cha polisi hakiniruhusu nimfanyie vitendo vya jinai Henge, tutarajie nani atalibadilisha Jeshi letu la Polisi?

Ukweli ni kwamba Shilo na wasomi wenzake katika Jeshi la Polisi wametuangusha vibaya sana. Afadhali wasingekuwa wasomi tungeelewa, lakini kwa wasomi kama wao kutumiwa kama vibaraka na mabwana wao wa kisiasa ni aibu kubwa kwa jamii ya wasomi katika nchi hii. Pathetic.

Labda sasa imefika wakati kuwauliza polisi kama kina Shilo ili watuambie ukweli, ni kwa nini hasa walijiunga na Jeshi la Polisi?
 
Back
Top Bottom