CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 855
Haina maana kuwa yeye ndiye binadamu bora kuliko wengine, la hasha, Tundu Antipas Lissu ni sawa na binadamu wengine kwa sababu anachukia, anapenda anafurahi, anakasirika na sifa zinginezo tulizonazo wanadamu.
Nilipopata taarifa ya kushambuliwa kwake, niliumia sana roho, na nilipata taarifa hii kupitia rafiki yangu aliyenipigia simu...siku hiyo ya tarehe 7/9/2017.
Moja ya sababu kuu inayofanya nimuombe Mungu amsaidie Lissu ili aweze kurudi kwenye majukumu yake ya kawaida, ni pamoja na kuwa mstari wa mbele kupigania haki za wanyonge. Tundu Antipas Lissu kwa taaluma yake ya sheria na kama mwanasiasa, ndiye mtu pekee aliyesikika akisema na kupigia kelele suala la mafao ya wafanyakazi kwa mifuko ya jamii. Lissu kupitia vyombo vya habari aliwahi kunukuliwa akisema, suala la mafao ya wafanyakazi kwenye mifuko ya jamii litapelekwa mahakamani ili haki ipatikane.
Kwa sasa kila mtu aliyefukuzwa kazi anaonja joto ya jiwe mitaani kutokana na serikali kupitia mifuko ya jamii kuzuia fedha zake. Watu hatuna kazi, tunashindwa kujiajiri kwa kukosa mitaji ambayo kimsingi serikali imezuia kupitia mifuko ya jamii, halafu eti unaambiwa usubiri mpaka miaka 55 au 60 ndipo uje kuchukua fedha zako. Kweli serikali inafanya haya kwa kutujali au kutukomoa? Unanambiaje niishi mpaka miaka 55 au 60 ndipo nije kuchukua mafao yangu ilihali unajua hakuna 'unemployment benefit' plan Tanzania? Unanambiaje nitachukua mafao yangu mpaka ntakapokuwa nimefikisha umri wa kustaafu wakati sina kazi na kazi hazipatikani kutokana na waajiri kupunguza wafanyakazi kila leo?
Mimi leo hii, nikiugua napataje huduma za afya ilihali sina fedha mkononi? Naishi nyumba ya kupanga, nalipaje kodi ya nyumba? nakula nini? navaa nini? Je, hii serikali sikivu inataka kuona NAKUFA pale ntakapokosa tiba hospitali kutokana na ugonjwa, iwapo nitaugua? Je, hii serikali ya wanyonge na sikivu inataka kuona vyombo vyangu mwenye nyumba anavitupa nje kwa sababu ya kushindwa kulipa kodi ya nyumba? Je, hii serikali sikivu na ya mtetezi wa wanyonge inataka kuona nikikamatwa kwa kuhisiwa 'mzururaji'? Je, hii serikali sikivu na inayotetea wanyonge inafanyaje ubaguzi kwenye kutoa mafao, kwamba anayepunguzwa kazini apewe ila anayefukuzwa asipewe? Kwa hali hii kweli tusipaze sauti?
Ee Mungu nakuomba kwa imani yangu umsaidie Tundu Lissu apone, arejee kwenye majukumu yake ili suala la mafao kwa wafanyakazi aweze kulipigania. Tunaishi kama mbwa koko mitaani wakati pesa zetu zimeshikiriwa kwa nguvu na serikali kupitia hii mifuko ya jamii, kwa sababu ambazo hazina msingi wowote.
[HASHTAG]#PrayForTunduLissu[/HASHTAG]