Kwa Nini na kwenye elimu iwe hivi?

Lundavi

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
327
320
Habari wanataaluma!
Nilikuwa najaribu kulinganisha jinsi Sekta nyingine zinavyotoa huduma na jinsi sekta ya elimu inavyotoa huduma.
Ukiangalia utaona walimu ambao ndio wadau wakubwa katika utoaji wa elimu kunawakati tunabebeshwa mizigo ambayo imeepukwa katika sekta nyingine.

Kwamfano ukiangalia katika muhimili wa mahakama kumekuwa na uendeshaji wa kesi kulingana na uzito wa kesi husika. Kwamfano kuna kesi zinafaa kusikilizwa kwenye mabaraza ya usuluhishi yaliyopo kwenye kata,nyingine mahakama za mwanzo, nyingine mahakama Za wilaya na nyingine zinaenda mpaka mahakama kuu.

Katika sekta ya afya pia kuna kitu kinaitwa rufaa, ambapo kuna wagonjwa wanaopaswa kutibiwa kwenye dispensari, wengine wanapelekwa kwenye vituo vya afya vya kata, wilaya, mkoa na wengine hushauriwa kupelekwa hospitali kuu kama vile Muhimbili, na ikishindikana hapo utasikia kapelekwa India n.k.

Kwa kuangalia mifano hiyo kuna ulazima wa serikali kufahamu kuwa hata katika sekta yetu ya elimu tunawanafunzi ambao uwezo wao wa kumudu masomo hasa ya sekondari ni mdogo kiasi kwamba wanahitaji rufaa. Mfano nijikite kwa wanafunzi tunaoletewa sekondari, kwanza tunaletewa karibu wote kutoka Shule za msingi, then tunaambiwa tuhakikishe wote wanafaulu kuanzia daraja la kwanza mpaka la nne. Tumesahau kunawanafunzi wanaugonjwa(akili) ambao haupaswi kutibiwa sekondari. Kwa tuliosoma zamani kulikuwa na mchujo mkali sana kuanzia shule za msingi thus why tuliokuwa tunaenda sekondari tulikuwa bright, na hata waliokuwa wanashindwa kujiunga na masomo ya sekondari uwezo wao ulikuwa juu kiasi cha kufanya vizuri mtaani.

Kwa kweli Mimi naona sio lazima kila mwanafunzi asome sekondari, jambo la msingi hapa ni turudi kwenye misingi ya elimu yetu ya kuhakikisha wenye sifa ndio ajiunge sekondari, na akifika sekondari apimwe kikamilifu hasa kidato cha pili. Saizi kuna utaratibu wa kuwavusha kidato cha pili kwenda cha Tatu kwa division. Kuna watoto wanavuka kwa kupata daraja la C(45%) kwa somo moja tu, na ukigawa kwa masomo Tisa ni wastani wa 5, then unataka huyo huyo afaulu kwa lazima akifika kidato cha nne.

Kwahiyo naomba kuwe na rufaa hata kwenye sekta ya elimu kwani kunaakili za wanafunzi hazifit kabisa nondo zinazotolewa sekondari. Wamalize darasa la saba, kwa watakao faulu kweli waje sekondari na watakao feli kuanzia shule ya msingi na sekondari hasa kidato cha pili waende wakajifunze kushona, kufuga, kulima, kujenga, useremala, ususi n.k. Sio lazima kila mtu asome sekondari wakati akili yake sio ya sekondari.
 
Back
Top Bottom