Kwa nini Mahakakani na Bungeni kuna picha ya Raisi wa JMTZ?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,815
*Mahakamani

Siku zote tunahubiriwa kwamba nchi yetu ina Mihimili mkuu mitatu yaani Uraisi/Serikali, Mahakama na Bunge ambayo inajitegemea yaani maana yake ni kwamba hakuna Muhimili ulio juu ya mwingine!

Sasa swali langu Je, kwa nini Mahakama zote Tanzania na Bunge letu kuna picha ya Raisi wa JMTZ? Tena iko Juu kabisa kuliko Picha zote lkn Ofisi za Serikali hazina picha ya Jaji Mkuu wala Spika wa Bunge la JMTZ?
 
Umeshaambiwa ni Rais wa JMTZ......

Tena unauliza nini Sasa zaidi.........

Hivi ni lazima kuanzisha threads hata kama una cha kuhoji...........

Nakushauri Lala ni usiku kwa SAA za Tanzania......

Lkn pia ni Bunge la JMTZ, isitoshe tunaambiwa kwamba hii Mihimili yote inajitegemea na hakuna mkubwa zaidi ya mwingine!
 
*Mahakamani

Siku zote tunahubiriwa kwamba nchi yetu ina Mihimili mkuu mitatu yaani Uraisi/Serikali, Mahakama na Bunge ambayo inajitegemea yaani maana yake ni kwamba hakuna Muhimili ulio juu ya mwingine!

Sasa swali langu Je, kwa nini Mahakama zote Tanzania na Bunge letu kuna picha ya Raisi wa JMTZ? Tena iko Juu kabisa kuliko Picha zote Lkn Ofisi za Serikali hazina picha ya Jaji Mkuu wala Spika wa Bunge la JMTZ?
Kwasababu Yeye Ndiye MKUU WA DOLA ( Bunge, Mahakama na Serikali ) Na Amiri Jeshi Mkuu Wa Majeshi Ya Ulinzi na Usalama. Mtu Yeyote Ambaye Majeshi Yanamheshimu Ndo Mwamuzi

N.B Wapinzani Hawawezi Kushika Dola Kwasababu Hawana Ushawishi Jeshini.
 
Katika hii mihimili mitatu Central Government is Supreme. Hii mingine miwili inaweza ku check and balance Serikali kuu lakini Serikali kuu ni Supreme. Hayo mahubiri ya mihimili mitatu ni kisheria lakini ukweli ni kwamba Rais ndio mkuu wa nchi na anamteua Jaji mkuu na Majaji wote na Serikali kuu ndio inatoa fedha kwa mahakama na bunge ijapokuwa bunge linaidhinisha bajeti
 
Kijana hivi vitu vingune vipo kimaandishi tu,kiuhaliasia vinafanyika tofauti.

Eti kwamba rais hana sauti mahakamani na bungeni,wakati huo huo anayo kinga ya kutoshitakiwa!!!!nini maana ya hii??
 
Kinachompa nguvu rais ni haya;
1.Kachaguliwa na wananchi ambao hutegemea vyombo vyote.
2.Muundo wa utawala katika nchi zenye muundo wa jamhuri, rais ndo kawekwa juu ya jamhuri, kuna vipengele vya sheria vinampa mamlaka ya kuweza kusimama katika vyombo vingine vinavyounda jamhuri.Shortly &clear
 
*Mahakamani

Siku zote tunahubiriwa kwamba nchi yetu ina Mihimili mkuu mitatu yaani Uraisi/Serikali, Mahakama na Bunge ambayo inajitegemea yaani maana yake ni kwamba hakuna Muhimili ulio juu ya mwingine!

Sasa swali langu Je, kwa nini Mahakama zote Tanzania na Bunge letu kuna picha ya Raisi wa JMTZ? Tena iko Juu kabisa kuliko Picha zote Lkn Ofisi za Serikali hazina picha ya Jaji Mkuu wala Spika wa Bunge la JMTZ?
Inamaana hukusoma shule ya msingi wewe, hususan somo la URAIA au unaleta utani!?
Darasani tulifundishwa,,,,
>>" Bunge Lina sehemu mbili 1. Wabunge(bunge lenyewe), 2. Rais
>>" Kazi kuu ya Bunge ni ....., KUTUNGA SHERIA
>> " Sheria iliyotungwa na BUNGE haiwezi kuwa sheria mpaka,...... IPITISHWE NA RAIS.
>> " Mahakama ni idara chini ya Wizara inayoundwa na Raisi
Bado unauliza Nani MKUBWA.
 
Binafsi naamini siku zote Raisi wa JMTZ yuko JUU na ndiyo maana Picha iko Juu kwenye Mahakama na Bunge, lkn tunahubiriwa kila na Wanasheria kwamba wote wako sawa!
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza kila kitu.

Rais ni Mkuu wa Nchi na ndiyo Mkuu wa Serikali na ndiyo Mwenye Mamlaka ya juu kabisa ktk nchi.

Rais ndiyo Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Anateua Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu Tanzania Bara
 
Ok mimi naona ni uvunjivu wa katiba ambao kwa upumbavu na woga tuliojazwa kiuchakachuaji hatuhoji

Nembo ya taifa inatosha lakini hizo picha labda sijui lakini naamini hazipo kikatiba.

Ndiyo sababu kubwa utaifa ulitolewa na kuwekwa pembeni badala yake tunatakiwa kuwaabudu wenye picha zao.

Mfano rais kama atahusika na mauji au uvunjifu wa katiba si mahakama au bunge litakalohoji acha sisi wengine tunaowekwa mahabusu kwa kunyimwa dhamana kwa maagizo toka juu

Great Conforter?????????!!!!!!!!!!!!!
 
Rais wa Tanzania ana kofia Mbili
Ni mkuu wa nchi
Na mkuu wa serikali

So kama mkuu wa nchi lazima picha yake iwepo kila sehemu haya kwenye mihimili mingine
Na ya tatu mkuu wa chama

"Sitotangaza njaa kwa kuangalia nyika kavu"
 
*Mahakamani

Siku zote tunahubiriwa kwamba nchi yetu ina Mihimili mkuu mitatu yaani Uraisi/Serikali, Mahakama na Bunge ambayo inajitegemea yaani maana yake ni kwamba hakuna Muhimili ulio juu ya mwingine!

Sasa swali langu Je, kwa nini Mahakama zote Tanzania na Bunge letu kuna picha ya Raisi wa JMTZ? Tena iko Juu kabisa kuliko Picha zote lkn Ofisi za Serikali hazina picha ya Jaji Mkuu wala Spika wa Bunge la JMTZ?
Majibu unayo ila unataka yatamkwe na wengine ili lengo lako litimie
 
Kinachompa nguvu rais ni haya;
1.Kachaguliwa na wananchi ambao hutegemea vyombo vyote.
2.Muundo wa utawala katika nchi zenye muundo wa jamhuri, rais ndo kawekwa juu ya jamhuri, kuna vipengele vya sheria vinampa mamlaka ya kuweza kusimama katika vyombo vingine vinavyounda jamhuri.Shortly &clear
thank mjomba
 
Back
Top Bottom