Heshima kwenu wadau,
Nimesikitishwa na malumbano yanayoendelea ndani ya chama cha CUF, huu siyo mustakabali mzuri kwa vyama vya upinzani nchini. Kuna jambo nimeshindwa kulielewa, mbona tuhuma nyingi zinakwenda kwa katibu mkuu wa CUF kuwa amekaa muda mrefu ana majukumu mengi hivyo anashindwa kukiendeleza chama chake? Mbona hawamsemi Prof Lipumba, mbona naye amekaa madarakani kwa muda mrefu? Tena muda mwingi anautumia nje ya nchi kwa shughuli zake binafsi (Mfano sasa anafanya kazi ktk agency moja ya UN kwa mkataba) tena zisizo na tija katika maendeleo ya chama chake? Lipumba anaweza kukaa nje ya nchi kwa mwaka mzima, je kwa kipindi hicho nani anayekiendesha chama?
Kwa maoni yangu nadhani CUF inaelekea kufa, kwa sasa hata wakimweka nani, chama hakiwezi songa mbele. Kikubwa kwao ni kuimarisha ndoa yao na CCM.
Nawasilisha,