Elections 2010 Kwa nini JK hajatoa ahadi ya kuuza mashangingi kuboresha hospitali, n.k.?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Nimekuwa nasikiliza kampeni za wagombea urais mbali mbali kunadi watakachokifanya kuboresha hali za Watz walio masikini, lakini sijamsikia mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete akiahidi kwamba akichaguliwa tena safari atayapiga mnada mashangingi ya maafisa wakuu wa serikali ili kuboresha huduma mbali mbali za jamii zilizozorota kama vile afya, elimu n.k. Nilimsikia Dr Slaa na Lipumba kwa nyakati tofauti wakitoa ahadi hizo.

Jee JK anaogopa nini kutoa ahadi kama hiyo iliyo bora? Hata kama ni ahadi tu, kwani ahadi nyingine alizotoa si za kipuuzi kabisa? Au kama kawaida yake, anaogopa kususwa na mafisadi wanaombeba ambao kazi yao kubwa ni kuboresha maisha yao kuliko yale ya wengine wengi walio masikini?
 
sasa atatembelea nini yeye na familia yake?hujui ndo maana anang'ang'ania kurudi mjengoni?
 
mashangingi hawezi kuuza ila atanunua baja 400 kwa jili ya akina mama wajawazito
 
mashangingi hawezi kuuza ila atanunua baja 400 kwa jili ya akina mama wajawazito
Machozi ndani ya daladala

Nikiwa kati ya WATU waliohudhuria mikutano ya kampeni hasa ya urais,nimeona mengi,nimesikia mengi,ahadi kemkem,tam,nzuri na zenye kuvutia na kama JK,SLAA au LIPUMBA mmoja wo akishinda na kutekeleza ahadi zake basi TANZANIA itakuwa kama Boswana au kama sio kuifikia Afica kusini. Sina sababu ya kuzitaja ahadi kwani wengi wenu mwazijua.

Ni saa 12:30 za jioni siku ya ijumaa,natoka ofisini kwangu JMOO nakwenda posta ili kupanda gari la kuelekea mbezi nyumbani kwangu(mbezi ya kimara).Abiria ni wengi kama kawaida,wezi wamo,ila kuna magari ya kwenda mbezi ya buku(elfu moja) naingia na muda si mrefu gari inajaa na kuondoka,wote tumekaa,foleni ni kama kawaida kwani inaanzia faya na uku gari ikiwa imewekwa radio moja ya chama tawala.Watu tupo kimya na aliyesimama ni konda tu.

Mara hiyo radio ikaanza kutangaza sera za mgombea uras wa chama tawala,ahadi nyingi,kile mara iki najua mwazijua sina shida ya kuzitaja ila ni moja tu ambayo nitaitaja ambayo imenipelekea kuandika UJUMBE huu kwenu,ni ile ya KUNUNUA BAJAJI 40 KWA WAMAMA WAJAWAZITO,hapo ni saa 1:30 za jioni na hatujavuka magomeni.

Mara baada ya huyo mgombea kutaja iyo ahadi,nikasikia sauti kuoka nyuma ya gari ikisema "ZIMA RADIO YAKO AU BADILISHA STESHENI"ni sauti ya kike tena mwanamama mjamzito.Dereva alizima radio,tukawa kimya kila mtu nahisi alikuwa anajiuliza kwanini huyu mama kasema radio izimwe au ibadilishe stesheni,ukimya ulitawala kama dk 15.Tukiwa tunaanza foleni ya ubungo pale mahakama ya ndizi au bigbrother, na ikiwa ni saa 2:07 za usiku,nikasikia sauti ya mwanamama mwingine(sio mjamzito) ikisema "KAMA MIMBA ZINGEKUWA ZINABEBWA KWA ZAM HUYU KIKWETE ASINGETAMKA MANENO HAYO"nikashtuka nikageuka nyuma nikakutana uso kwa uso na yule mama mwenye mimba,mimba yake ilikuwa ni kama ya miezi nane tena ilikuwa kubwa(namaanisha tumbo ni kubwa sana).

Tukiwa tupo stand ya mkoa na gari likiwa limesimama na ni saa 2:45 usiku kumbuka nimetoka posta saa 12:30 za jioni.Yule mama mjamzito akasimama akaanza kusema "MIMI SITOMPA KURA KIKWETE KWA JAMBO ILI,NILIKUWA NIMPE ILA KWA JAMBO KAMA ILI SIWEZI KUMPA"uku akilia na kutokwa na machozi,yule mama mwingine aliyesema "kama mimba zingekuwa zinabebwa kwa zam huyu kikwete asingetamka maneno hayo" akaanza kumbembeleza yule mama mjamzito akimsii akae.Nilimtazama kila mtu ndani ya gari sura zilibadilika zikawa sura za majonzi.

Nikatoka kwenye daladala(kimawazo) nikaleta taswila ya BAJAJI nikamuweka yule mama nyuma na mimi nikawa dereva,nikafikiria umbali wa kilometa 50 toka kijijini kwetu kule kanyigo kuja hospital,barabara imejaa mashimo,nikawaza tumbo la yule mama akiwa yuma na uchungu na babaji ikiwa inayumba kwenye mabonde ya barabara,"NILILIA" nilishutushwa na honi nyingi za magari ambazo zilikuwa zikilipigia daladal letu kwa kutotembea, kwani kila mtu alikuwa kwenye mawazo ya yule mama(naisi) na dereva alijisahau kwa kumuonea huruma yule mama.Nilikuwa karibu na dereva nikamuuliza vp?,akajibu "WE ACHA TU"uku akitoa leso na kufuta machozi na kuanza kuendesha gari.

Ni saa 3:07 usiku tupo kimara tunaanza foleni ya kimara stopover,watu wote wapo kimya akuna aliyeshuka mpaka sasa na konda kaka kwenye mlango ameinama,kila mtu kainama,uku wengine wakivuta mafua,na yule mama mjamzito akionekana ana asira na uku machozi yakimtoka yenyewe.Nikajiuliza ina maana watu wote tunakwenda mbezi?,pia huyu mama vp mbona kabadilisha kila mtu ndani ya daladala? Katumwa nini?.Nikasikia sauti ya baba mmoja kutoka katikakti ya gari akisema shusha konda hapo,konda akasema wapi?,baba akajibu hapo hapo,Mmmmmmmmm?,"Samahani konda nilikuwa nashuka bucha nimejisahau" alisikika yule baba akisema,Mmmmmmmmm?.Ndipo nilipoona kila mtu karudi katika hari yake ya kawaida na wengine wakashuka hapo kama watu sita hivi.Nikajiuliza je walikuwa wanawaza nini? Mpaka wapitishwe kituoni?.Je walikuwa katika taswila kama yangu?,au uchovu wa kazi?

Kati ya wale walioshuka pale njiani(sio kituoni) baba mmoja akasema akimwambia yule mama mjamzito "POLE SANA MAMA NA MIMI NAKUHAIDI SITOMPA KURA KIKWETE"akatelemaka.Tunavuka stopover na ni saa 3:30 usiku,kila mtu kaanza kusema lake"KIKWETE HANA AKILI"alisikika baba mmoja,"KIKWETE NI MGONJWA" alisikika dada mmoja,"WANAIGEIZA NCHI YA FAMILIA KWANI HAPA TUNATAWALIWA KIFALME" alisikika kaka mmoja.Ni saa 3:45 nashuka kibanda cha mkaa na niliposimama nikwaambia abilia "HUYO NDIO RAIS WENU HATA KIWA CHIZI SI MLIMCHAGU WENYEWE" nikajibiwa na konda "SHUKA UKO NA NENDA ZAKO",Mmmmmmmm ata konda?

Nikiwa njiani nakwenda kwangu nikawa natafakari "JE YALE MACHOZI YA MAJI YALIYONDONDOKA NDANI YA DALADALA LEO"je ni ya bure tu?,na je "IPO SIKU YATALIPWA"?,na je "IPO SIKU YATAGEUKA KUWA NI MACHOZI YA DAM"? nisingependa ilo tafakari langu la mwisho litokee.

Je wewe unatoa machozi gani au maneno agani?,je machozi ya furaha? Au ya uzuni kama yule mama mjamzito?au maneno ya kumtukana rais wako kama wale watu kwenye daladala.Kazi kwako. Nikipata nauli kabla ya UCHAGUZI nitakwenda kanyigo nimuulize babu "JE BABU UMESHAWAI KUONA KICHUGUU CHA SENENE"?.​
 
Back
Top Bottom