Kwa nini computer yangu haiwezi ku save files? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini computer yangu haiwezi ku save files?

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by tizo1, Jul 30, 2011.

 1. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Habar wataalamu!Nina Programu ya Pinnacle studio 10 kwenye PC yangu.Tatizo kila ninapofanya project fulani inashindwa ku save files ambazo zipo tayari kama kazi.Badala yake inaweka ka alama kadogo ka duala ambako kamekatwa na mstali katikati.Je ili niweze ku save kazi zangu nipitie hatua zipi?
   
 2. Osaba

  Osaba JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 1,720
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Angalia drive C kama kuna space ya kutosha maana files nyingi za hiyo pgm huwa zinasave kwenye hiyo drive kama ni ndogo ifungue na uifunge upya angalia kwenye option ya kusave files uisave kwenye drive yenye GB nyingi
   
 3. IT Guru

  IT Guru JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 616
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kwenye pinnacle demo version ndio haiwezekani kusave file. Kwani hiyo yako demo version mkuu?
   
 4. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Mkuu hajajieleza vizuri, hiyo application program unai-run kutoka kwenye media gani? Hard Drive(internal au external), flash au optical drive? Kama hiyo program haiko installed kwenye drive C: ya komputa yako basi komputa itakuwa na wakati mgumu wa kujuwa hizo file zako ziwe saved kwenye file extension ya application program hipi! Matokeo yake itakataa kusave kazi yako. Tatizo lingine kama huna enough space kwenye drive C: utashindwa kusave kazi yako lakini mimi naona kwako hilo alipo kwani kumputa yenyewe ingekueleza kwamba"No enough space on drive C: please delete some files" kitu kama hicho. Kwa kumalizia naona tatizo litakuwa nililo eleza hapo mwanzo na husisahau kwamba kuna aina ya virusi vya komputa vinavyo weza kudisable command ya kusave files, keyboard hata movement ya mouse cursor - so beware.
   
 5. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Mkuu sijaona popote ambapo muomba ushauri amesema kwanba application program yake ni DEMO version. Hivi kweli Demo version inaweza kweli kuruhusu primitive zake(objects) ziunde Project nzima, alafu anapotaka kusave inakataa! Nijuavyo mimi Demo version nyingi zinakubali kusave file hila ukitaka kutoa a hard copy printout itaonyesha water mark kwamba copy ni ya DEMO, I stand to be corrected.
   
Loading...