Katiba ya nchi na Sheria ya vyama vya siasa inaonesha vyama vya siasa ni vyama vya hiyari mali ya umma.
Katiba zote za vyama vya siasa havijaweka kipengere cha kuzuia mtu akihama asirudi tena kwenye chama husika kwa kuwa itakuwa ni kinyume cha Katiba na sheria za nchi.
Ila vyama vyote vina kanuni ya kuwaangalia waliorudi kabla ya kuwapa madaraka ndani ya vyao.
Vyama vya siasa ni mlango wazi, anayetoka huwezi kumzuia asitoke na anayeingia huwezi kumzuia asiingie.