Kwa Nini CCM Inashinda Chaguzi "Kwa Kishindo"?

Kuna mwaka CCM walishinda Ubungo lini ni ubungo kwa CCM ni sawa na uchaguzi wa Zanzibar

Mbona kila mwaka CCM wanashinda Ubungo? Ni Mrema na Lamwai tu waliwaweza Ubungo.

Tatizo nionavyo mimi sio wananchi kutokuelewa bali ni upinzani kushindwa kuelewa wananchi wanataka nini.
 
Sababu nyingine - CCM wamefanikiwa kujenga na kudhibiti mfumo wa kifisadi ambao unawafaidisha wachache katika ngazi zote: toka vijijini hadi Ikulu na kuwapa matumaini wajinga wengi (kunradhi) kuwa ipo siku nao wataambulia kitu - kama hadithi ya fisi na mkono wa mtu. Kama ilivyo kwa matapeli professional, wamehakikisha wameua mifumo sahihi ya vipato halali kwa wengi na kukamata hisia ya tamaa ya asili ya binadamu (greed) kutaka kujihakikishia ridhiki kwa njia yoyote. Hapo uchaguzi kwa mwananchi unabakia mmoja tu: jiunge nasi (CCM)ufaidi (angalau mlio tu wa shilingi) au kaa nje upigwe na baridi kali. Bila ukombozi wa nafsi hata elimu ya darasani haisaidii kitu.
 
Maoni yangu ni kuwa pale CCJ itakapojikita kwenye uchaguzi ndio mwisho wa CCM.

Ninayasema haya kwa mtazamo huu.

Katika chaguzi zetu wagombea/vyama wanapangwa katika ascending order. Na kila mara CCM inakuwa ya kwanza (Chanzo cha Nambari One CCM). Sasa kitakapoingia CCJ kitakuwa cha kwanza katika list. Hapo ndio muanguko wa CCM.

Logically, hata mtu ambaye si mpambanuzi au hajui kusoma mara nyingi katika list anachagua kile kilichotangulia. WaTz wengi ni wavivu wa kusoma na kufuatilia, hivyo basi wanaona ni heri kuchagua kile cha kwanza.

Ni Mtazamo tu, akili kumkichwa!
 
Ni sera nzuri za ccm zinazokubaliwa na wananchi kwa ujmla na umadhubuti wa kutekeleza ilani yake.

Hili la sera nalo linahitaji mjadala wake. Wengi hawajui sera ni nini. Eti kujenga barabara za lami kati ya makao makuu ya mikoa yote, kuhakikisha kila mtu anapata maji safi; kila mtoto anaenda shule; kuhakikisha hiki kinakuwa kizazi cha mwisho kufa kwa malaria; blablabla!. Hizo sio sera, hayo ni malengo ya maendeleo ambayo kila mwanasiasa mwenye akili timamu lazima awe nayo. Sera ni jinsi gani unatimiza malengo hayo?

Wengine sera yao ni kutumia zaidi mapato ya serikali (kodi na mirahaba ya rasilimali za taifa) kufanya hayo; wengine ni kuvutia zaidi watu binafsi kujenga na kutoa huduma hizo; wengine ni kutegemea misaada ya wafadhili 100%! Nchi nyingine barabara nyingi ni biashara ya watu binafsi (toll roads) wakati kwingine hiyo haikubaliki. Hizo ndizo tofauti za sera. Sio kile akina Makamba wanachodai kuwa wapinzani wanaiga sera nzuri za CCM!

Kwa kadiri wananchi na viongozi watakavyoendelea kuwa na ujinga kuhusu SERA, hawa jamaa wataendelea kutoa kauli zisizo na kichwa wala miguu kama hizo. Na hii iko hata upinzani-wengi hawajui kufafanua sera zao.
 
Sidhani kama ni kweli JK ana personality kuliko Lipumba, au opposition hawajasimamisha mtu mwenye kuweza kuwaconvince. Ukiwa kapi ukigombea kupitia CCM utashinda tu, ukiwa profesa ukigombea kupita TADEA utashindwa tu, unless uwe na bahati na connection na constituents, ukija kwa sera au logic hakuna utakachopat. Ni kweli kuwa watanzania wengi bado tuko kwenye lepe la usingizi, tunadhani kuwa CCM ndio baba na ndio mama. Tunaona kuwa CCM ni muhimu zaidi kuliko Tanzania, tunaacha Tanzania iwe hatarini, inavurugwa na inaibiwa lkini tunalinda wale wanaoiibia kisa ni kuwa wako CCM. Tatizo liko kwetu watanzania wapiga kura hasa ambako hakuna elimu. Tunahitaji watanzania wenye uchungu kwenda kwenye kila jimbo au kila kata kuwaambia ndugu zetu kuwa tunaibiwa na tunatumiwa.

Kama tukitegemea watanzania wapate mwamko wa kubadilisha chama wa ballot box, itachukua miaka 200. Tunahitaji watanzania wachache tu kubadilisha mambo juu, asilimia 70 watafuata upepo. Kasanga Tumbo aliwahi kusema hayo, Mtikila aliwahi kusema hayo, Mrema alisema wote walionekana wehu, lakini ukweli umeonesha kuwa hawakuwa wehu, walijua ni nini wanasema, imetuchukua miaka 15 kujua kuwa walichokuwa wanasema ni kweli.
 
Luteni,

Naona kumbukumbu yako inapotea kidogo. Kumbuka Mrema alivyoondoka NCCR Mageuzi na kwenda TLP, angalia umati wa watu alioondoka nao kama lusifa alivyoondoka na theluthi moja ya malaika kule mbinguni. Watu wanaangalia mtu na si system. Mpeleke Lipumba CCM uone kama atashinda. NEVER.
 
Kwanza hao CCJ ndio akina nani?? Nani anawafahamu, halafu ndio unasema wakipangwa wa kwanza watawini !!! Loh, kichekesho.
 
Ni jambo la kushangaza sana kuona tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi TZ, vyama vya upinzani vimekuwa vikididimia wakati CCM ikizidi kushamiri na "kushinda" kila uchaguzi kwa vishindo.

Inashangaza ikiwa utachukulia wingi wa kura wanazopewa CCM kama ishara ya kushukuriwa kwa mazuri waliyoyafanya kwa nchi na wananchi na maendeleo waliyoyaleta katika kipindi walichopewa jukumu la kuongoza(miaka mitano). Kwa maana nyengine wananchi huwaambia CCM endeleeni kutuongoza na kutenda mambo ambayo mmekuwa mukitufanyia.

La kushangaza zaidi ni kuwa wananchi wengi unaokutana nao wanasikitika sana kuhusu hali ya maisha, hali ya nchi kudumaa,viongozi wanaochota na kujikusanyia mabilioni ya pesa bila ya kukamatwa na kufungwa, viongozi wasiojali kabisa maslahi ya nchi na shida za wanyonge. Viongozi hao hao ndiyo wamekuwa wakichaguliwa kila uchaguzi unapofanyika na kurudishwa tena madarakati waitafune nchi.

Katika nchi nyengine, wananchi hutumia kura kama fimbo ya kuwapigia viongozi wabaya na kuwafukuza madarakani na viongozi wapya wanaochaguliwa huwa wanajua kuwa wakiboronga basi fimbo inawasubiri.

Sasa ni kwa nini wananchi walio wengi TZ wanakubali kuwa nchi iendelee kuongozwa na watu hawa? Mimi sijapata jawabu ya kitendawili hiki. Ni kweli kuwa uchaguzi wenyewe si safi na mizengwe inakuwepo, lakini mimi naamini kabisa kuna WaTZ wengi (hasa bara) ambao wako tayari kufa kuihami CCM.
Ni nini siri kubwa ya CCM?

Nimejaribu kuwauliza baadhi ya wataalamu wanasema ni kwa sababau waTZ wengi ni mbumbumbu. Hawaelewi ni nini kinaendelea. Huamini uongo wanaoambiwa majukwaani bila ya kuchambua ukweli wa mambo.Mtu atateswa miaka nenda miaka rudi lakini ikifika uchaguzi hata akialikwa pilau tu akapewa na fulana moja ya njano au kijani basi husahau madhila na dhulma zote na huwa mstari wa mbele kuitikia CCM juju,juu, juu zaidi !!

Wengine wanasema kuwa watu waliharibiwa akili kwa kasumba na propaganda wakati wa mfumo wa chama kimoja na wengi mpaka leo wanahisi kama ni "uhaini" kukipigia kura chama cha upinzani.
Kama ni kasumba, sasa itatuchukua miaka mingapi wananchi kuamka na kuona kuwa nchi imeshikwa na watu wachache ambao kila uchao,wanaitafuna, wanaendelea kuwa matajiri wa kufuru wakati wananchi wanazidi kuwa maskini.

Ni mpaka lini tutaendelea kuwaweka madarakani viongozi ambao pamoja na kuwa TZ imejaaliwa kuwa na kila aina ya utajiri (ardhi,madini, mito, maziwa, bahari, n.k) wamefanikiwa kuihujumu nchi na kuiweka ya pili kutoka ya mwisho duniani(nadhani tumewapita wasomali) kwa umasikini.? Ni mpaka lini CCM itaendelea "kushinda" kwa vishindo?

Dalali

Hii zinaitwa siasa za umaskini na ujinga. Unawafanya watu kuwa maskini na wajinga kiasi kwamba jambo la muhimu kwao ni mlo wao unafuata. Na elimu unayowapa ni bora elimu siyo elimu bora itakayo wafanya waweze kung'amua mbinu zako chafu. Baada ya hapo unakuja kama mkombozi wakati wa uchaguzi na kuwapa chakula kidogo, nguo na pesa za bei nafuu na kisha watu wanakuona mkombozi wao na kukupa kura za ndio na ushindi wa kishindo.

Kuhusu vyama vya upinzani mimi nadhani hawana ajenda ya mageuzi ya kweli. Wanachotaka ni kuingia kwenye madaraka kwa mfumo huu huu uliopo ili nao wachukue chao mapema. Wanachosahau ni kuwa mfumo huu uliopo ambao kimsingi ni wa chama kimoja ulisukwa na CCM wakiwa na malengo ya kutawala milele.

Walichofanya CCM ni kuruhusu vyama vingi katika mfumo wa chama kimoja kushika hatamu. Hivyo apinzani wanapambana na siyo tu CCM bali na dola nzima kwa maana ya serikali kuu na serikali za mitaa , vyombo vya ulinzi na usalama, na hata vyombo vya habari vya umma.
 
Sababu kuu ya ushidi wa CCM ni Ujinga wa waTZ ikiwa nyinyi munaojifanya ni wasomi ni wajinga itakuwa waTZ wasio soma. CCM haishindi, inatangazwa tu na Mkereketwa Lewis M. Makame na R.R. Kiravu hii yote ni mi CCM mikereketwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom