Kwa Nini CCM Inashinda Chaguzi "Kwa Kishindo"? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Nini CCM Inashinda Chaguzi "Kwa Kishindo"?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dalali444, Feb 15, 2010.

 1. D

  Dalali444 Member

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni jambo la kushangaza sana kuona tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi TZ, vyama vya upinzani vimekuwa vikididimia wakati CCM ikizidi kushamiri na "kushinda" kila uchaguzi kwa vishindo.

  Inashangaza ikiwa utachukulia wingi wa kura wanazopewa CCM kama ishara ya kushukuriwa kwa mazuri waliyoyafanya kwa nchi na wananchi na maendeleo waliyoyaleta katika kipindi walichopewa jukumu la kuongoza(miaka mitano). Kwa maana nyengine wananchi huwaambia CCM endeleeni kutuongoza na kutenda mambo ambayo mmekuwa mukitufanyia.

  La kushangaza zaidi ni kuwa wananchi wengi unaokutana nao wanasikitika sana kuhusu hali ya maisha, hali ya nchi kudumaa,viongozi wanaochota na kujikusanyia mabilioni ya pesa bila ya kukamatwa na kufungwa, viongozi wasiojali kabisa maslahi ya nchi na shida za wanyonge. Viongozi hao hao ndiyo wamekuwa wakichaguliwa kila uchaguzi unapofanyika na kurudishwa tena madarakati waitafune nchi.

  Katika nchi nyengine, wananchi hutumia kura kama fimbo ya kuwapigia viongozi wabaya na kuwafukuza madarakani na viongozi wapya wanaochaguliwa huwa wanajua kuwa wakiboronga basi fimbo inawasubiri.

  Sasa ni kwa nini wananchi walio wengi TZ wanakubali kuwa nchi iendelee kuongozwa na watu hawa? Mimi sijapata jawabu ya kitendawili hiki. Ni kweli kuwa uchaguzi wenyewe si safi na mizengwe inakuwepo, lakini mimi naamini kabisa kuna WaTZ wengi (hasa bara) ambao wako tayari kufa kuihami CCM.
  Ni nini siri kubwa ya CCM?

  Nimejaribu kuwauliza baadhi ya wataalamu wanasema ni kwa sababau waTZ wengi ni mbumbumbu. Hawaelewi ni nini kinaendelea. Huamini uongo wanaoambiwa majukwaani bila ya kuchambua ukweli wa mambo.Mtu atateswa miaka nenda miaka rudi lakini ikifika uchaguzi hata akialikwa pilau tu akapewa na fulana moja ya njano au kijani basi husahau madhila na dhulma zote na huwa mstari wa mbele kuitikia CCM juju,juu, juu zaidi !!

  Wengine wanasema kuwa watu waliharibiwa akili kwa kasumba na propaganda wakati wa mfumo wa chama kimoja na wengi mpaka leo wanahisi kama ni "uhaini" kukipigia kura chama cha upinzani.
  Kama ni kasumba, sasa itatuchukua miaka mingapi wananchi kuamka na kuona kuwa nchi imeshikwa na watu wachache ambao kila uchao,wanaitafuna, wanaendelea kuwa matajiri wa kufuru wakati wananchi wanazidi kuwa maskini.

  Ni mpaka lini tutaendelea kuwaweka madarakani viongozi ambao pamoja na kuwa TZ imejaaliwa kuwa na kila aina ya utajiri (ardhi,madini, mito, maziwa, bahari, n.k) wamefanikiwa kuihujumu nchi na kuiweka ya pili kutoka ya mwisho duniani(nadhani tumewapita wasomali) kwa umasikini.? Ni mpaka lini CCM itaendelea "kushinda" kwa vishindo?

  Dalali
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,464
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu ya upumbavu wa wapiga kura walio wengi nchini mwetu ambao wakishapewa sahani ya pilau, beer mbili au soda, fulana za kijani na njano, gunia la mahindi au mchele na shilingi 10,000 wanajiona wameuchinja sana na kusahau kabisa haki zao katika kuhakikisha wanatumia haki zao vizuri. CCM kwa kutumia vyombo vya dola huwanyanyasa, kuwatisha na hata kuwapiga wanachama na viongozi wa vyama vya upinzani. Ubinafsi wa hali ya juu uliojaa katika vyama vya upinzani ambavyo havitaki kuungana ili kuunda chama kimoja chenye nguvu ili kuiondoa CCM madarakani. Angalia CHADEMA chama ambacho kiliwapa matumaini makubwa Watanzania sasa wanagombana hadharani na hata kuondoa imani kubwa waliyoijenga miongoni mwa Watanzania kwamba wanaweza kuchukua madaraka. Sasa hivi wanafukuzana na kuadhiriana hadharani pamoja na kuwa imebaki miezi michache kabla ya uchaguzi wa 2010. Vyote hivi vinachangia sana katika kuipa CCM ushindi wa kishindo.
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  bado hatujapanuka kimawazo ,tunadanganyika na vitu vidogo ,mchele ,sukari ,mafuta,khanga na kuuza haki yetu ya msingi ambayo ingetusaidia kufanya mabadiliko,wananchi bado hatuna mwamko
   
 4. K

  Koba JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 180
  Wapiga kura wengi ni peasants,rushwa,wizi wa kura na utemi wa vyombo dola
   
 5. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,375
  Likes Received: 1,519
  Trophy Points: 280
  Habari zenu wana ukumbi, nimekuwa kwenye benchi kwa miezi kadhaa. Hvyo nawasalimuni wote.

  Tatizo la Afrika na hasa Tanzania , hakuna tatizo kubwa bali kuna tatizo kidogo sana na mara nyingi tatizo dogo huwa ni tatizo kuliko tatizo kubwa, maana tatizo kubwa linakuwa limekalibia ukomo wa kukuwa wakati tatizo dogo linakuwa ktk mchapuko.

  Tatizo lenyewe ni mentality tu.
   
 6. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Katika huo utajiri hukutaja rasilimali watu. Hadi hapo tutakapokuwa na watanzania wanaojiamini, wanaoweza kusimama na kutoa hoja hata mbele ya mataifa mengine. Watanzania wanye uelewa wa nini ni haki yao na nini ni upendeleo. Watanzania wanaoelewa nini wajibu wa serikali na vyombo vyake kama polisi mahakama n,k.
  Watanzania wenye kuweza kuhoji pale panapokwenda ndivyo sivyo. Wasomi wasiojikomba kwa wanasiasa na watawala. Watanzania waliotayari kuujenga mfumo wa uongozi na sio utawala kuanzia ngazi ya kijiji hadi serikali kuu.

  Hapo ndipo watanzania watakuwa na fursa ya kupima hoja na sera za wagombea kujipatia viongozi wanaowafaa. Vinginevyo, itokee hali chungu kama vile 'hamadi' unakabiliana na chui, huwezi tu kumuacha akurarue bila kujaribu kujitetea (ambayo hii ni nadra kutokea)!
   
 7. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  umewahi kulisikia lile jiwe lililokuwa likitumiwa na majambazi, FATUMA? ni kwa sababu ya wizi, na mabavu ,,,,,,,ikumbukwe ZANZIBAR mwaka 1995
   
 8. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,143
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ni kwa sababu ya umaskini na ukosefu wa elimu. Hayo ndiyo mambo makubwa yanayoibeba CCM daima. Na ninafikiri itaendelea kuhakikisha wananchi wanabaki masikini na wajinga ili wakitishiwa kwamba vyama vya upinzani vitaleta vita basi waogope, wakiambiwa CCM ni chama cha Nyerere basi waheshimu, wakidanganyiwa tshirt za kijani, khanga na suruali nyeusi basi watetemekee. Ukifanya tathimini utagundua hata baada ya miaka miwili tangu uchaguzi upite, watu wanaendelea kushindia hizo sare za CCM. Huo ni ushahidi tosha kwamba CCM inawaokoa sana kimaisha kwa kuwapa angalau Tshirt za kushindia. Tuwe realistic, hakuna namna yoyote ya kubadilisha ushindi wa CCM pasipo kuwapa elimu wananchi. Elimu ninayoiongelea hapa ni elimu bora na si hii ya yeboyebo ambayo ni maalum kwa ajili ya masikni na ambazo ni maalumu kwa ajili ya kampeni. Tutwaona kwenye kampeni kila mtu atasema CCM imejenga shule za yeboyebo, ilihali ni wananchi waliojinyima ili kuzijenga. Ni vigumu kubadilisha mfumo huu kama wananchi hatutajielimisha.
   
 9. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tume ya uchaguzi ndo chanzo kikuu cha hayo wananchi wanaelewa sana na wanawapigia wapinzani lakini kura zinaibiwa mchana kweupeee na tume ..tatizo tume

  Polisi na state organs zina intimadite wananchi wanaofanya upinzani hasa vijijini mwenyekiti wa kijiji anaweza kufanya maisha yako kuwa miserable sembuse polisi utafia jela/polisi bila dhamana who can dare to opposse
   
 10. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,375
  Likes Received: 1,519
  Trophy Points: 280
  Swahili tunasema ukitaka kusaka nyoka aliyejificha uvunguni nyakati za usiku anza kwanza kupiga tochi kuanzia miguuni mwako yani uliposemama na ndipo uendelee kupiga tochi uvunguni na ktk kona za nyumba .Lakini point of reference lazima iwe pale miguuni kwako.
   
 11. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #11
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Njaa jamani njaa! hamuoni mashati ya kijani yameshaanza kushamiri? ni ajira isiyo rasmi kwa wavivu na waganga njaa, wao ilimradi matumbo yao yajae huwa awaangalii hatma ya miaka mitano baadaye.
   
 12. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wagombea kiti cha Urais toka kambi ya Upinzani bado siyo "convincing candidates" kwa wapiga kura wetu. Msidhani Wa TZ ni wajinga kama mnavyowafikiria, wanamacho na masikio. Wanaangalia hawa wagombea wetu na kuwapima kisha wanaishia "kheri jini likujualo" Kama nchi inataka mabadiliko ya kweli, wagombea urais toka kambi ya upinzani wawe ni watu wanaokubalika. Siyo hii timu iliyogombea toka mfumo wa vyama vingi uanze, wanashindwa kila chaguzi ila hawataki kuachia wengine maana wamefanya vyama kuwa kama kampuni zao binafsi. UPINZANI... WAKATAENI WAGOMBEA WENU WALE WALE. Hapo tutaona mabadiliko ya kweli, laa sivyo sijaona mgombea urais toka upinzani anayeweza kuing'oa CCM.
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wewe unaongelea mtu wengine tunaongelea system au chama mpeleke Kikwete akagombee NLD kwa system ya chama hicho kama atashinda
   
 14. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Mkuu Mzee Kibiongo, hayo ukiyosema hapo juu ndio sababu ya ushindi wa CCM.

  Kama vyama vya upinzani vitabaki vikisubiri huruma ya wananchi ili kushinda uchaguzi, itachukua muda mrefu bila kuona mabadiliko ambayo wengi wanayatamani.

  Wananchi huchagua mgombea, sio chama. Kila ufikapo wakati wa uchaguzi, matumaini mapya hujitokeza. Inategemea ni mgombea gani anaeonyesha kuleta matumaini hayo. Ukweli ni kwamba, endapo upinzani hautakuwa makini katika kusimamisha wagombea wake, basi CCM itaendelea kushinda, na hata wakisimamisha wagombea wasio na nguvu sana, wanaweza kushinda pia.

  Matumaini ninayoyaona sasa ni kuwa, kuna uwezekano kuwa kura zitapungua sana kwa CCM mwaka huu endapo upinzani utafanya yafuatayo.

  1. Kujenga ushirikiano kati ya vyama vya upinzani katika kampeni

  2. Kusimamisha wagombea wachache katika kila jimbo ili kuepuka kusambaza kura za wapinzani

  3. Kusimamia ajenda za maendeleo na kutoa matumaini ya kupunguza umasikini, kero, na kuleta usawa kwa wananchi

  4. Kusimamisha mgombea Urais mmoja kutoka kambi ya upinzani ambae anakubalika (si mmoja wa waliokuwa wakishindwa kila uchaguzi)

  Kuhusiana na CCM kutoa t-shirts, pilau na soda. Sidhani kuwa hilo ndilo linalowafanya wananchi waipigie kura kama namna ya kuridhika nayo. Ila, inasaidia kuweka hamasa na ushabiki ambao baadae huwafanya wengi kuipigia kura na kusahau mapungufu ya siku za nyuma. Wapinzani pia wanaweza kuchapisha t-shirts nzuri ambazo zitawasaidia katika kampeni zao, nao wataweza kufaidika na kushawishi wananchi kuwa wanao uwezo wa kuwaletea neema.

  Ni dhahiri kuwa mgombea anaeonyesha umasikini na ubahili hawezi kukonga nyoyo za wapiga kura au kuteka imani zao kwake. Ni mbinu tu, kila mtu anao uwezo wa kuzitumia. Hazina copyrights.
   
 15. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 370
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni sera nzuri za ccm zinazokubaliwa na wananchi kwa ujmla na umadhubuti wa kutekeleza ilani yake.
   
 16. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #16
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kuna sababu nyingi tu nitataja chache
  1.Upinzani haujafanya kazi ya kutosha
  2.Wapiga kura wetu hawaeleweki..sorry kwa kusema haya
  3.CCM ni wezi wa kura
  4.Watendaji wa Serikali kushughulika na chaguzi..
  5.Kutokuwa na tume huru ya uchaguzi
  6.Wasomi hawajitikezi kupiga kura n.k
   
 17. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Msisitito no.3 kura za wapinzani zinachezewa kama mchezo wa karata tatu cheusi na chekundu ukiweka popote umeliwa.
   
 18. L

  Lugombo Member

  #18
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na wale wapiga kura wa jimbo la Ubungo je? Nao ni pilau na sukari? Maana hilo jimbo ndilo lina vyuo vingi lakini nako CCM wanashinda tu.
   
 19. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2010
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hapa umenikuna..ni kweli kabisa.
   
 20. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuna mwaka CCM walishinda Ubungo lini ni ubungo kwa CCM ni sawa na uchaguzi wa Zanzibar
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...