Ni jambo la kushangaza sana kuona tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi TZ, vyama vya upinzani vimekuwa vikididimia wakati CCM ikizidi kushamiri na "kushinda" kila uchaguzi kwa vishindo.
Inashangaza ikiwa utachukulia wingi wa kura wanazopewa CCM kama ishara ya kushukuriwa kwa mazuri waliyoyafanya kwa nchi na wananchi na maendeleo waliyoyaleta katika kipindi walichopewa jukumu la kuongoza(miaka mitano). Kwa maana nyengine wananchi huwaambia CCM endeleeni kutuongoza na kutenda mambo ambayo mmekuwa mukitufanyia.
La kushangaza zaidi ni kuwa wananchi wengi unaokutana nao wanasikitika sana kuhusu hali ya maisha, hali ya nchi kudumaa,viongozi wanaochota na kujikusanyia mabilioni ya pesa bila ya kukamatwa na kufungwa, viongozi wasiojali kabisa maslahi ya nchi na shida za wanyonge. Viongozi hao hao ndiyo wamekuwa wakichaguliwa kila uchaguzi unapofanyika na kurudishwa tena madarakati waitafune nchi.
Katika nchi nyengine, wananchi hutumia kura kama fimbo ya kuwapigia viongozi wabaya na kuwafukuza madarakani na viongozi wapya wanaochaguliwa huwa wanajua kuwa wakiboronga basi fimbo inawasubiri.
Sasa ni kwa nini wananchi walio wengi TZ wanakubali kuwa nchi iendelee kuongozwa na watu hawa? Mimi sijapata jawabu ya kitendawili hiki. Ni kweli kuwa uchaguzi wenyewe si safi na mizengwe inakuwepo, lakini mimi naamini kabisa kuna WaTZ wengi (hasa bara) ambao wako tayari kufa kuihami CCM.
Ni nini siri kubwa ya CCM?
Nimejaribu kuwauliza baadhi ya wataalamu wanasema ni kwa sababau waTZ wengi ni mbumbumbu. Hawaelewi ni nini kinaendelea. Huamini uongo wanaoambiwa majukwaani bila ya kuchambua ukweli wa mambo.Mtu atateswa miaka nenda miaka rudi lakini ikifika uchaguzi hata akialikwa pilau tu akapewa na fulana moja ya njano au kijani basi husahau madhila na dhulma zote na huwa mstari wa mbele kuitikia CCM juju,juu, juu zaidi !!
Wengine wanasema kuwa watu waliharibiwa akili kwa kasumba na propaganda wakati wa mfumo wa chama kimoja na wengi mpaka leo wanahisi kama ni "uhaini" kukipigia kura chama cha upinzani.
Kama ni kasumba, sasa itatuchukua miaka mingapi wananchi kuamka na kuona kuwa nchi imeshikwa na watu wachache ambao kila uchao,wanaitafuna, wanaendelea kuwa matajiri wa kufuru wakati wananchi wanazidi kuwa maskini.
Ni mpaka lini tutaendelea kuwaweka madarakani viongozi ambao pamoja na kuwa TZ imejaaliwa kuwa na kila aina ya utajiri (ardhi,madini, mito, maziwa, bahari, n.k) wamefanikiwa kuihujumu nchi na kuiweka ya pili kutoka ya mwisho duniani(nadhani tumewapita wasomali) kwa umasikini.? Ni mpaka lini CCM itaendelea "kushinda" kwa vishindo?
Dalali
Ni mpaka lini tutaendelea kuwaweka madarakani viongozi ambao pamoja na kuwa TZ imejaaliwa kuwa na kila aina ya utajiri (ardhi,madini, mito, maziwa, bahari, n.k) wamefanikiwa kuihujumu nchi na kuiweka ya pili kutoka ya mwisho duniani(nadhani tumewapita wasomali) kwa umasikini.? Ni mpaka lini CCM itaendelea "kushinda" kwa vishindo? Dalali
Jamani wagombea kiti cha Urais toka kambi ya Upinzani bado siyo "convincing candidates" kwa wapiga kura wetu. Msidhani Wa TZ ni wajinga kama mnavyowafikiria, wanamacho na masikio. Wanaangalia hawa wagombea wetu na kuwapima kisha wanaishia "kheri jini likujualo" Kama nchi inataka mabadiliko ya kweli, wagombea urais toka kambi ya upinzani wawe ni watu wanaokubalika. Siyo hii timu iliyogombea toka mfumo wa vyama vingi uanze, wanashindwa kila chaguzi ila hawataki kuachia wengine maana wamefanya vyama kuwa kama kampuni zao binafsi. UPINZANI... WAKATAENI WAGOMBEA WENU WALE WALE. Hapo tutaona mabadiliko ya kweli, laa sivyo sijaona mgombea urais toka upinzani anayeweza kuing'oa CCM.

bado hatujapanuka kimawazo ,tunadanganyika na vitu vidogo ,mchele ,sukari ,mafuta,khanga na kuuza haki yetu ya msingi ambayo ingetusaidia kufanya mabadiliko,wananchi bado hatuna mwamko
Kuna sababu nyingi tu nitataja chache
1.Upinzani haujafanya kazi ya kutosha
2.Wapiga kura wetu hawaeleweki..sorry kwa kusema haya
3.CCM ni wezi wa kura
4.Watendaji wa Serikali kushughulika na chaguzi..
5.Kutokuwa na tume huru ya uchaguzi
6.Wasomi hawajitikezi kupiga kura n.k

Na wale wapiga kura wa jimbo la Ubungo je? Nao ni pilau na sukari? Maana hilo jimbo ndilo lina vyuo vingi lakini nako CCM wanashinda tu.