Kwa Nini CCM Inango'ka?

Nitakuwa sijakutendea haki kama nikipita kimyakimya Ocampo four wewe ni jembe la ukweli, na katika mabadiliko ya nchi hii na wewe utakuwepo kama shujaa uliyeyapigania..
Hongera sana.
 
Last edited by a moderator:
Sijawahi changia hata siku moja hapa jamvini lkn nimekuwa msomaji sana wa mada mbali mbali. Lkn hii ya leo nafsi inanisuta nisipotoa HESHIMA KWAKO Big up sana
Ndo mana hujawahichangia kwa maana huna hoja. Hiyo analysis haina lolote kwani kama mnataka mabadiliko kutoka wapi! Kwa mamvi au Sumuye. Hamjui kuwa wagombea wawili wenye nguvu wote ni wa ccm.
 
...maisha ni mabadiliko na mabadiliko ndio maisha...twende na UKAWA kwenye mabadiliko...
 
Mnaweweseka tu hakuna kama Magufuli. Hawa wengine ni wasindikizaji.

Magufuli hauziki Mkuu, Chama anachokisimamia hakiuziki kwa sasa Mkuu... Infact, ni ngumu sana kwa Magufuli kushinda....

Hili wimbi la mabadiliko ni ngumu sana kulizuia. Nchi nyingi zilijaribu ila walishindwa. Vyama vingi vilijaribu ila vilishindwa....
 
Magufuli hauziki Mkuu, Chama anachokisimamia hakiuziki kwa sasa Mkuu... Infact, ni ngumu sana kwa Magufuli kushinda....

Hili wimbi la mabadiliko ni ngumu sana kulizuia. Nchi nyingi zilijaribu ila walishindwa. Vyama vingi vilijaribu ila vilishindwa....

Hata mimi sasa naamini kuna vuguvugu kubwa mno la mabadiliko kwa kile nilichokishuhudia jana Mbeya Vijijini.

Ni akina mama katika majadiliano yao kwenye kikundi fulani nikagundua wana ari kubwa sana na wamemuelewa Lowassa. Nimeshangazwa.

Na Ocampo umefanya kazi kubwa wengi wenye akili zetu tumeona, tutakuombea.
 
1. November 2, 1991 wananchi wa Zambia walimchagua Ndg. Chiluba ambaye alimshinda aliyekuwa rais kwa zaidi ya miaka 27 na mpigania uhuru wa nchi hiyo Mzee Kaunda; pamoja na sababu zingine ila kubwa zaidi, wananchi hao walihitaji "Mabadiliko".


2. Dec. 2002 chama kikongwe Africa cha KANU chini ya Rais MOI (M o One) kilishindwa vibaya sana na muungano wa NARC chini ya Mwai Kibaki kwa sababu wananchi walihitaji "Mabadiliko"...

Africa hakuna chama kilichokuwa na nguvu kubwa kama KANU. KANU ilisifika kwa kujenga nchi mpaka wimbo maalum wa kitaifa ulitungwa kwa ajili ya kuisifu KANU... "KANU yajenga Nchi".... Ila wananchi walihitaji mabadiliko wakaziba masikio na kufumba mambo...

3. Sep. 2011 Michel Sata pamoja na uzee wake alimshinda Rupia Banda kwa sababu wananchi walihitaji "mabadiliko".....

Ukisoma kitabu cha Dambisa Moyo "Why Zambia" anakueleza vizuri sana jinsi Banda kipindi akiwa rais alijitahidi sana kujenga miundombinu (hasa barabara) mpaka vijijini.

Ila kwa bahati mbaya wananchi hawakuona haya yote kwa sababu ndani ya mioyo yao walisukumwa na hitaji kuu ambalo ni "Mabadiliko"


4. 2012, Macky Sall alishinda uchaguzi wa Senegal na kumbwaga mkongwe wa siasa za Africa Abdoulaye Wade mtu aliyekaa madarakani zaidi ya miaka 20. Kwa hakika haikuwa jambo jepesi wala kazi nyepesi lakini kwa kuwa wananchi walihitaji "mabadiliko" Rais Sall alishinda kwa zaidi ya asilimia 65%....


5. 2015 pamoja na kutukanwa juu ya umri wake, afya yake, na familia yake Ndg. Buhari aliibuka mshindi na kumgaragaza rais aliyekuwepo madarakani (sitting president) G. Jonathan kwa sababu wananchi walihitaji "mabadiliko"..

Nakumbuka Gavana wa Itiki Ndg. Fayose alizunguka nchi nzima ya Nigeria akimtukana Buhari na kusema haifiki siku ya uchaguzi Buhari atakuwa amekufa. Ila leo hii tunashuhudia rais mpya wa Nigeria ni Buhari....


6. Pagan Amum (SG) wa SPLM, South Sudan aliwahi kusema kwamba, inafikia kipindi mabadiliko katika nchi yoyote ile hayakwepeki. Wananchi wanapodai mabadiliko haijalishi umewafanyia mazuri kiasi gani au mabaya kiasi gani ila kikubwa kwao ni kupata mabadiliko.....

Wananchi wanapotaka mabadiliko haijalishi na hawaitaji kujua yatakuwa mabadiliko ya namna gani, ila kikubwa kwao ni kupata mabadiliko...

Wananchi wanapohitaji mabadiliko hawahitaji kujua kama yatakuwa positive kwao au negative kwao wenyewe wanachokijua kwa wakati huo ni kupata mabadiliko....

Wananchi wanapohitaji mabadiliko alyways wanaziba masikio na kufumba macho... Ukiwa chama dola hata uwambie nitakuletea maziwa mlangoni kwako kamwe hawezi kukusikia.... Na akiwa kijana hata ukimuahidi kumpatia msichana mzuri sana kama Cinderela au Cleopatra hawezi kukuelewa... Kikubwa kwake ni kupata mabadiliko...

NB:.. Ndugu zangu CCM inango'ka kwa sababu wananchi wanahitaji mabadiliko. Tumechoka!....

Kama nimekuelewa vizuri mkuu ocampo, unamaanisha kuwa kuna hali ya kuchoka kisaikolojia ambayo inaonekana hata kwenye siasa pale mazingira yanapokuwa hayohayo kisiasa na watu watatafuta sababu yoyote kuyabadilisha. Nadhani pia ndio maana wenzetu wamarekani na waingereza sikuzote kuna vyama viwili ambavyo karibu vina nguvu sawa, ili wakichoka wanatoa hiki wanaweka kile, inatokea automatically lakini inanguvu sana, ndio maana nasisi ni lazima tuweke ukawa kiwe chama cha pili kwa nguvu nchi hii.
 
Back
Top Bottom